Pages

Thursday, 19 February 2015

TANZANIA KUSHIRIKIANA NA NORWAY KATIKA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI.


 Waziri waWizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway kwenye Mkutano uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu ( katika kati) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway, Mhe. Ola Elvestuen (kushoto) wakiwa na Balozi wa Norway Nchini Tanzania, Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (kulia) Kabla ya Mkutano wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (hayupo pichani ) kwenye Mkutano uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam.
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii zimekubaliana kushirikiana na Serikali ya Norway katika kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti kwa wingu ili kukabiliana na mabadilko ya tabia ya nchi .
Akizungumza kwenye Mkutano wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway uliofanyika Mpingo House jijin Dar es Salaam, Mhe Nyalandu amesema kwamba ushirikiano huo utaweza kuisaidia Tanzania kuendelea kuongoza kuwa nchi yenye kijani iliyo mstari wa mbele katika Mapinduzi ya Kijani barani Afrika kwa kupanda miti kwa wingi.
Alisema kwamba ushirikiano huo utakuwa endelevu kwa kuiwezesha Tanzania kupanda miti kwa wingi kwa kuendelea kuitunza misitu iliyopo kwa kuzuia ukataji miti usio endelevu hasa ukataji wa magogo pamoja na biashara nyingine za misitu zisizo endelevu.
Aidha , Mhe Nyalandu alisema kwamba Tanzania kwa kushirikiana na Norwaya wamebuni mfumo wa kulinda Mlima Kilmanjaro na Mlima Meru kwa kuendeleza uoto asili wake.
Aliongeza ,kuwa mpango huo utasaidia Barafu ya Mlima Kilimanjaro kuendelea kuwepo kwa miaka mia ijayo kwa kutouumiza Mlima huo kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayotishia uwepo wa barafu hiyo .
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway, Mhe. Ola Elvestuen amesema kwamba watashiriana na nchi ya Tanzania katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kupanda miti kwa wingi kwa kulinda na kuhifadhi uoto asili uliopo.
Mwenyekiti aliongeza kuwa wanajaribu kuangalia uwezekano wa kuisaidia Tanzania katika vita dhidi ya Ujangili wa wanyamapori kutokana na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuishinda vita hiyo.

No comments:

Post a Comment