Friday 30 September 2016

TFS YATOA MICHE YA MITI 600 KATIKA SHULE YA SEKONDARI MAMA SALMA KIKWETE KUUNGA MKONO KAMPENI YA UPANDAJI WA MITI JIJINI DAR ES SALAAM

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akimkabidhi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina (wa pili kulia) miche 600 ya miti iliyotolewa na ofisi yake kwa ajili ya shule ya Sekondani ya Mama Salma Kikwete Jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni hatua ya kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya upandaji wa miti Jijini Dar es Salaam ijulikanyo kama “Mti Wangu” . Katika uzinduzi huo TFS imechangia miche ya miti 3,000 kati ya miche 8,000 ambayo imepanga kutoa kwa ajili ya kupandwa katika Jiji la Dar es Salaam.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina akipanda mti katika Shule ya Sekondani ya Mama Salma Kikwete, Jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya upanadaji miti Jijini Dar es Salaam iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda, Kampeni hiyo ijulikanayo kama "Mti Wangu" itazinduliwa kesho Oktoba Mosi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umechangia miche ya miti 600 katika shule hiyo na miche ya miti mingine 3,000 itatolewa kesho wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa ajili ya Jijiji la Dar es Slaam, katika awamu ya pili watachangia tena miche ya miti 5,000


 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete Jijini Dar es Salaam leo katika hafla fupi ya upandaji wa miti shuleni hapo kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya upandaji wa miti, Prof. Silayo amewaasa wanafunzi hao kuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti. Katika hafla hiyo TFS wamekabidhi jumla ya miche ya miti 600.
 Picha ya pamoja kati ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina (wa tano kushoto), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (wa sita kushoto), Msanii Jackline Wolper, Watumishi na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mama Salma Kikwete.

No comments:

Post a Comment