Friday, 30 September 2016

TANZANIA KATIKA TUZO ZA UTALII ZA WORLD TRAVEL AWARDS 2016

Tanzania imebarikiwa kwa kila kitu! milima, mabonde, mito, wanyama, maziwa, bahari, visiwa, madini ya kila aina na watu wake wakarimu; yote haya yanaifanya Tanzania kusifika kwa uzuri wake huku kitovu cha amani kikiwa ndio tunu pekee ya taifa hilo.mount-kilimanjaro
Katika vipengele tisa vya Tuzo za Dunia za Mashindano ya Utalii (WTA) kwa mwaka 2016 zinazotarajiwa kutolewa Disemba 2 mwaka huu huko nchini Maldives, nchi ya Tanzania tayari imesajili vivutio vyake 10 ili kuchuana na nchi nyingine katika tuzo hizo.

Msemaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB), Geofrey Tengeneza amesema “Pazia limefunguliwa tangu Septemba 23 na litafungwa Oktoba 24. Kila Mtanzania anaweza kupiga kura kwa kuitembelea tovuti ya WTA na kupiga kura kwenye vipengele vya dunia na Afrika ili kuuleta ushindi nyumbani”.serengetiKwa uchache vipengele ambavyo Tanzania imeviorodhesha ni pamoja na nchi bora ya kuitembelea, ufukwe na kisiwa bora zaidi (Zanzibar), hoteli ya kifahari na kampuni ya utunzaji wa mazingira.

Chema chajiuza kwani uzuri wa Tanzania haufichiki, ni wakati wako sasa mtanzania mzalendo kupiga kura kupitia tovuti ya WTA ili Tanzania itwae tuzo hizi.

No comments:

Post a Comment