Monday, 13 June 2016

KIVUTIO CHA AJABU UKEREWE, MWANZA

UTALII ADIMU KISIWA CHA UKEREWE
HANDEBEZYO HILL SEHEMU ILIYO JUU YA KILELE CHA KILIMA CHA PANGO LA BENKI YA WATEMI. ENEO AMBALO LILITUMIKA KWA AJILI YA ULINZI NA USALAMA WA KISIWA, KUONA MAADUI WANAOKUJA KUVAMIA NA KADHALIKA. UKISIMAMA ENEO HILI UNAONA SEHEMU KUBWA YA KISIWA CHA UKEREWE.

MFANO WA ENEO KUBWA UNALOWEZA KULIONA UKIWA HANDEBEZYO HILL.


KATIKA POZI MASUPER STAR WA KESHO KUTOKA KUSHOTO MELI, MTEBA, MSEKWA, NYEBHUNU, CHIFYWE NA EMMANUEL.

LIKIWA NA MVUTO WA KIPEKEE HILI NI KANISA LA KWANZA LA ROMAN CATHOLIC LILILOJENGWA ENZI ZA UKOLONI KTK KISIWA CHA UKARA WILAYANI UKEREWE.

JIWE LA MSINGI LA MAKUMBUSHO YA OLWEGO LILILOWEKWA NA ALIYEKUA MKUU WA WILAYA BW. T.A.K MSONGE KWA MAENDELEO YA TAIFA LA TANZANIA. JE! LENGO LIMEFIKIWA?

JIWE HALISI LA MSINGI LILILOWEKWA NA BW. T.A.K MSONGE.

KWA NYUMA MUONEKANO WA PANGO LA BENKI YA WATEMI WA UKEREWE MAHALA AMBAPO WATEMI HAO WALIKUWA WAKIHIFADHI MALI ZAO ZA THAMANI, VITO, FEDHA, MADINI NA KADHALIKA, NA KILA MTEMI ALIKUWA NA SEHEMU YAKE YA HIFADHI. CHINI YA ULINZI WA UHAKIKA.

MLANGO WA KUINGIA PANGO LA BENKI.

MVUTO ENEO LA MBELE BARAZANI LANGO KUU LA BENKI YA WATEMI UKEREWE.

MANDHARI YA KIPEKEE MVUTO WA KITALII PEMBEZONI MWA HIMAYA YA MAKUMBUSHO YA WATEMI UKEREWE. ENEO LOTE HILI HALINA MLINZI WALA MFANYA USAFI BALI MWANGALIZI ASIYE LIPWA.

KORIDO INAYOTENGANISHA PANGO LA HIFADHI (SEHEMU YA BENKI YA WATEMI) NA UKUMBI WA MAPUMZIKO.

Habari naALBERT G. SENGO, 

No comments:

Post a Comment