Saturday 10 September 2016

MAPANGO YA KITALII YA AMBONI TANGA

.
 Lango kuu la kuingilia ndani ya mapango ambapo ndani ni Kiza mithili ya usiku TORORO na nilazima muongozaji kuwa na Tochi ya mwanga mkubwa na ndani kujionea vivutio vya ajabu ambavyo huwezi kuamini.
Ndani ya Mapango hayo kuna uchochoro mwembamba uliopinda na upitapo ni lazima utembee kwa Tumbotumbo na endapo ukikwama itakuwa balaa.(Ila haijawahi kutokea, ni maajabu)
 Uchochoro ndani Pango ni ajabu. Inasemekana ndani ya Pango hilo kuna njia ambayo inatokea Mkoa wa Kilimanjaro kwa upande mmoja na mwengine unatokea Mombasa nchini Kenya.
Hili ni moja ya Pango ambalo ukichungulia utaogopa kwani huoni mwisho hata ukitupa jiwe utalisikia baada ya dakika kadhaa tena likiwa halijafika mwisho na linakuwa linagonga pembe za Pango. Waongiozaji wanashauri Pango hilo kwa Mtalii wa ndani na nje kutolisogelea kwani lina nguvu mithili ya Sumaku

2 comments:

  1. Kwa hakika simulizi za mapangi ya Amboni na sehemu zignine za kihistoria ni hazina ya urithi wa vizazi kwa karne nyingi zijazo. Changamoto ninayoiona ni kuwa na njia rahisi ya kuwafikia na kusimulia similizi hizi kwa watoto kote chini. Napendekeza tujadili mawazo haya haususan kwa kuzingatia fursa za technologi ya kisasa ya mtandao.

    ReplyDelete