Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Kijiografia inapatikana katika Mkoa wa Mara. Kihistoria toka hapo zamani katika hifadhi hii ya Serengeti jamii ya Kabila la Wamaasai ambao ni jamii ya nilotiki ambayo kihistoria asilia yake ni Kusini mwa Sudani iliishi kwa miaka mingi pamoja na Wanyamapori katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba kipindi cha
wakati huo eneo hili la Serengeti ilikuwa ikihusisha
eneo linalofahamika leo hii kama Mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro ikijulikana kwa pamoja kama “Great Serengeti” kabla
ya eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
kutenganishwa mnamo mwaka wa 1959 na
kupelekea jamii yote ya kabila la Wamaasai waliokuwa
wakiishi eneo la Serengeti kuhamishiwa katika
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Asili ya jina Serengeti limetokana na lugha ya Kabila la Wamaasai lenye
kumaanisha uwanda mpana.
Nyumbu wahamao katika hifdhi ya taifa ya Serengeti ni moja ya maajabu 7 ya Dunia |
MAANDALIZI YA USAFIRI;
Anza na utafiti makini unaohusiana na wadau wa sekta ya utalii wanaohudumia shughuli za utalii katika hifadhi hii ya Taifa ya Serengeti. Gharama zake zikoje na zinatofatianaje vipi? Fedha zinazohitajika na upatikanaji wake. Mwisho kabisa ni mpango mkakati wa fedha na bajeti ya matumizi yenyewe ya fedha hizo katika safari ya matembezi hifadhini.

KUANZISHWA KWAKE:
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ilianzishwa mnamo mwaka wa 1951. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba mwaka huo wa 1951 ilikuwa ikihusisha kwa pamoja na eneo linalofahamika leo hii kama mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kabla ya eneo la Ngorongoro kutenganishwa na kujitegemea kutoka Serengeti hapo mwaka wa 1959.

ENEO LAKE:
Mpaka hivi sasa ukubwa wa eneo la hifadhi ya Taifa ya Serengeti ina ukubwa wa kilomita za mraba 14,763 ( au sawa na maili za mraba 5700). Hivi sasa, hifadhi ya Taifa ya Serengeti ndio hifadhi ya pili kwa ukubwa baada ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha kuongezwa ukubwa wa eneo lake na kufikia kilomita za mraba 20,380.

UFIKAJI HIFADHINI:
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inafikika umbali wa kilomita 335 (maili 208 kwa njia ya barabara magharibi ya mji wa Arusha. Seronera ndio makao makuu ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Ni umbali wa mwendo wa saa 5 mpaka 6 kutoka mji wa Arusha katika mwendo wa kawaida.

Watalii wakishangaa baada ya kutua katika uwanja wa Seronera,Serengeti |
MAUMBILE ASILIA YA KIJIOGRAFIA
HIFADHINI;
Mto Grumeti maarufu kwa idadi kubwa ya mamba, majabali ya mawe yenye mvuto wa kupendeza, Tambarare zenye nyasi nzuri zenye kupendeza.

HALI YA HEWA USAWA WA BAHARI
HIFADHINI;
Hali ya hewa kutoka usawa wa Bahari ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti inaanzia mita 950 mpaka 1850. Seronera ndio makao makuu ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni mita 1530.

VIVUTIO VIKUU VYA UTALII HIFADHINI;
Wanyamapori walao nyama kama vile simba, chui na fisi. Wengineo ni kama vile duma, mbwa mwitu, mbweha na wengineo.

Uhamaji wa Wanyamapori kwa msimu maalumu,
Tambarare zenye nyasi nzuri zenye kupendeza.
Vile vile viumbe hai ndege wa aina
mbalimbali kama vile mbuni. Hali kadhalika kuna ndege
wahamaji kutoka katika sehemu mbalimbali duniani katika msimu
husika.
WANYAMAPORI WAPATIKANAO HIFADHINI;
Wanyamapori ni wengi na wa aina mbalimbali kama vile mbwa mwitu, Tumbili (ngedere), vicheche, kuro, ngiri wanyamapori, paa, Taya, kindi, palahala, korongo, tohe, pimbi Wanyamapori, viboko, swala tomi, Kongoni aina ya cokei, nguchiro nyumbu, nyegere, digidigi, pongo, Insha, Pofu, Mhanga, Nyani, Nguruwe mwitu, Mbweha masikio, mbogo (nyati), chui, simba, swala pala, swala granti, Twiga, Tembo (Ndovu) na wengineo wengi.

Pundamilia ni moja wa wanyama wanaoambatana na nyumbu wakati wakihama hama |
UOTO WA ASILI HIFADHINI;
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inaangukia katika maeneo ya uoto wa asili wa maeneo Makame wa ukanda wa Somali – Maasai ambapo uoto wa asili wa mimea asilia ya miti ya migunga na mbabara au mturituri umetawala.

Katika ukanda wa eneo hili milimita za mvua kwa
mwaka ni milimita 300 mpaka 700. Vile vile
kuna uwanda mpana wa uoto wa nyasi (grassland).
Vile vile uoto wa asili wa msitu unaostawi
kufuata mkondo wa mto (Riverine vegetation).
WAKATI WA KUTEMBELEA HIFADHINI;
Mwezi wa Desemba mpaka Julai kuweza kuona msafara wa uhamaji wa Wanyamapori kama vile nyumbu na wanyamapori wengineo. Vile vile mwezi wa Juni mpaka Oktaba kuona wanyamapori walao nyama kama vile simba, chui, fisi, duma na wengineo wengi.

HUDUMA ZA CHAKULA;
Mambo ya kujiuliza katika safari yenu ya matembezi hifadhini, Je mtabeba vyakula vyenu wenyewe vya kujipikia? Au hakuna ulazima huo na badala yake mtapata huduma hiyo katika sehemu ambazo huduma ya chakula inapatikana.
HUDUMA ZA MALAZI AU KULALA;
Kama mtalala ndani ya hifadhi, Je mtapiga kambi na katika kupiga kambi ni lazima mbebe mahema yenu? Au kama hamtalala ndani ya hifadhi ni sehemu gani nyinginezo za huduma hiyo ya kimalazi.

Kempu ya kulala wageni Serengeti |
GHARAMA ZA USAFIRI WOTE;
Umakini katika eneo hili ni la muhimu kwa wahusika ambao ndio waandaaji wa safari ya matembezi hifadhini.
Mambo muhimu ya maandalizi ya usafiri, huduma za chakula, malazi au kulala na mengineyo. Haya yote ndio yatakayokamilisha safari ya matembezi hifadhini. Je safari yenu ya matembezi hifadhini inaendeka au haiendani? Jibu litapatikana baada ya utekelezaji wa mambo muhimu kukamilka.

MAMBO YA KUFANYA;
Dharura na matatizo mbalimbali hujitokeza katika safari ya matembezi hifadhini. Ni vema na busara kuwa na utamaduni wa kupeana mafunzo yanayohusiana na huduma ya kwanza na namna vifaa hivyo vinavyotumika.
MAMBO YA KUFAHAMU;
Mawasiliano ni ya muhimu na ni lazima yawepo kati yenu na hifadhi ya Taifa ya Serengeti au makao makuu ya Shirika la hifadhi za Taifa, Mjini ARUSHA. Je, kipindi ambacho mtatembelea hifadhi hii ni kipindi cha wageni wengi au wageni wachache? Je mnaweza kupata sehemu ya kupiga kambi au kulala hosteli? Hili ni suala muhimu la kujiandaa na kujipanga.
MAMBO YA KUCHUKUA;
Vifaa vyote muhimu katika safari yenu ya matembezi hifadhini.
HUDUMA ZA MAHITAJI MENGINEYO;
Mambo ya ziada ya mahitaji yanayojitokeza na
upatikanaji wake katika sehemu husika.

MAWASILIANO MENGINEYO:
Mkurugenzi Mkuu,
Hifadhi za Taifa, Tanzania
S.L.P. 3134, Arusha, Tanzania.
Simu; 255 – 272503471/2501930-31
Nukushi; 255 272508216
Barua pepe; dg@tanzania parks.com.
info@tanzania parks.com.
Tovuti: www.tanzaniaparks.com
Simu ya Mkononi; 0689-062 369 (airtel)
0767 – 536 140 (vodacom)
Mkurugenzi Mkuu,
Hifadhi za Taifa, Tanzania
S.L.P. 3134, Arusha, Tanzania.
Simu; 255 – 272503471/2501930-31
Nukushi; 255 272508216
Barua pepe; dg@tanzania parks.com.
info@tanzania parks.com.
Tovuti: www.tanzaniaparks.com
Simu ya Mkononi; 0689-062 369 (airtel)
0767 – 536 140 (vodacom)
Simu ya Mkononi;
0689 – 062 369 (Airtel)
0767 – 536 140 (Vodacom).
0689 – 062 369 (Airtel)
0767 – 536 140 (Vodacom).
MAWASILIANO HIFADHINI SERENGETI
(MOJA KWA MOJA)
0689 - 062 243 (Airtel)
0767 – 536 125 (Vodacom)
0689 - 062 243 (Airtel)
0767 – 536 125 (Vodacom)
MAMBO YA KUZINGATIA HIFADHINI,
Kanuni na taratibu za hifadhi.
Kanuni na taratibu za hifadhi.
No comments:
Post a Comment