Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina akipanda mti katika Shule ya Sekondani ya Mama Salma Kikwete, Jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya upanadaji miti Jijini Dar es Salaam iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda, Kampeni hiyo ijulikanayo kama "Mti Wangu" itazinduliwa kesho Oktoba Mosi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umechangia miche ya miti 600 katika shule hiyo na miche ya miti mingine 3,000 itatolewa kesho wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa ajili ya Jijiji la Dar es Slaam, katika awamu ya pili watachangia tena miche ya miti 5,000
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Kaimu
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos 
Santos Silayo (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari 
ya Mama Salma Kikwete Jijini Dar es Salaam leo katika hafla fupi ya 
upandaji wa miti shuleni hapo kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa 
Dar es Salaam ya upandaji wa miti, Prof. Silayo amewaasa wanafunzi hao 
kuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti. 
Katika hafla hiyo TFS wamekabidhi jumla ya miche ya miti 600.
 Picha
 ya pamoja kati ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na 
Muungano, Luhaga Mpina (wa tano kushoto), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala 
wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (wa sita 
kushoto), Msanii Jackline Wolper, Watumishi na baadhi ya wanafunzi wa 
shule ya Sekondari Mama Salma Kikwete.
 





No comments:
Post a Comment