Friday 10 July 2015

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

1.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III –(NAFASI 100)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
• Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
• Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
• Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
• Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
• Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
• Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
• Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
• Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kukusanya takwimu zao
• Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi
• Kudhibiti wanyamapori waharibifu
• Kudhibiti moto kwenye hifadhi
• Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya Uhifadhi Wanyamapori
(Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka
Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au  chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B2 kwa mwezi.

2.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III –(NAFASI 327)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

2.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
• Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
• Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
• Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
• Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
• Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
• Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
• Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
• Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kukusanya takwimu zao
• Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi
• Kudhibiti wanyamapori waharibifu
• Kudhibiti moto kwenye hifadhi
• Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake

2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya Awali ya Uhifadhi wa  Wanyamapori (Basic Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya  Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B1 kwa mwezi.

3.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II –(NAFASI 10)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

3.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
• Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
• Kusimamia uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
• Kulinda Nyara za Serikali
• Kusimamia usafirishaji wa wanyamapori na nyara nje na ndani ya Nchi
• Kusimamia matumizi ya magari ya doria
• Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kutunza takwimu zao
• Kuratibu uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba
• Kudhibiti moto katika hifadhi
• Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
• Kukusanya takwimu za wanyama na mimea kwenye hifadhi
• Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake

3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Stashahada ya Uhifadhi Wanyamapori  (Diploma in Wildlife Management) kutoka Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Mweka au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi

AFISA UTALII DARAJA LA II - 15 POST
Employer: Ministry of Natural Resources and Tourism
Date Published: 2015-07-09
Application Deadline: 2015-07-24

JOB SUMMARY:
N/A
DUTIES AND RESPONSIBILITIES:
• Kukusanya taarifa za maeneo mapya yenye vivutio vya utalii kwa kushirikiana na wadau wote
• Kutoa leseni za utalii kwa mahoteli na wakala wa utalii
• Kukusanya na kuweka takwimu za watalii na safari za kitalii
• Kutafuta na kupanga nafasi za masomo ya utalii ndani na nje ya nchi
• Kujibu malalamiko kutoka kwa watalii
• Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau katika uendeshaji wa biashara ya utalii
•  Kuandaa kaguzi mbalimbali za wakala wa utalii
• Kuchambua miradi ya wakala wa utalii na hoteli
• Kukagua hoteli, loji na migahawa
• Kujibu na kufuatilia malalamiko yanayotolewa  na watalii
• Kutoa ushauri wa kitaalaam kwa  wakala wa utalii
• Kukusanya takwimu za watalii kwenye sehemu/  vituo  nchini vya kuingilia/ kutoka kwa wageni
• Kutunza kumbukumbu za vitabu/ majalada ya maktaba ya utalii
• Kutayarisha taarifa za kila mwezi ya takwimu ya watalii walioingia nchini na mapato yaliyopatikana
• Kufanya tafiti ndogo “survey” kwenye hifadhi za Taifa na maeneo
• Kufuatilia kwa karibu  na kushirikiana na VETA  juu ya maendeleo ya vyuo vinavyotoa mafunzo ya utalii nchini
• Kuratibu miradi yote inayohusiana na utoaji wa mafunzo ya utalii
• Kutayarisha ripoti ya robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima
• Kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya sekta kwa kufanya savey
• Kutayarisha ripoti na kusambaza kwa wajumbe na kufuatilia utekelezaji wa maazimio
• Kupitia miongozo inayohusu ‘ Tourism Facilitation Committee’
• Kuratibu shughuri za kubuni vivutio utalii na mienendo mipya ya kuendeleza utalii utalii
• Kutayarisha na kuhakiki vivutio vya utalii nchini
• Kuitisha mikutano/ semina za uhamasishaji kuhusu uendeshaji utalii
• Kushiriki katika kupitia ripoti za EIA kuhusu miradi ya utalii
• Kushirikiana na Mashirika? Taasisi mbalimbali za mazingira katika shughuri zihusuzo utalii na mazingira
• Kukusanya rasilimali za uendeshaji katika vyanzo vya ndani na nje

QUALIFICATION AND EXPERIENCE:
• Kuajiriwa wenye Shahada/ Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Utalii, Hoteli, Uhusiano wa kimataifa, Biashara (masoko) au Sheria (Commercial law) kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali
REMUNERATION: Salary Scale TGS D

MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi
ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha,  kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelez
o binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za
simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita
kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
-Shahada ya juu/Shahada/Stashahada ya juu/Stashahada/Astashahada
.-Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
-Cheti cha Kompyuta
-Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. “Transcripts”, “Testmonials”, “
Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato
cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi ku
omba isipokuwa kama
wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma
wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa
tar
ehe 30 Novemba, 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 15 Aprili, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti
ya Ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani Ifuatayo;-

Katibu, AU Secretary,
Sekretarieti ya Ajira katika Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma, Secretariat,
SLP.63100, P.O.Box 63100
Dar es Salaam. Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment