Monday, 25 July 2016

UTALII WA NDANI: JUX & VANESSA SERENGETI, MRISHO MPOTO YEYE APANDA MLIMA KILIMANJARO

Vanessa Mdee na mpenzi wake Jux wameamua kwenda kupumzika kwa muda kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti. Wawili hao wamelazimika kusimamisha ratiba zao ndefu za muziki na biashara kujionea maajabu kwenye mbuga hiyo maarufu duniani iliyopo wilayani Serengeti, mkoani Mara.

aaaa

Wamefikia kwenye moja ya hoteli za mbugani bora zaidi duniani, Singita Serengeti Grumeti. Hoteli hizo zinazomilikiwa na wawekezaji wa Afrika Kusini, ni miongoni mwa hoteli zinazotoza gharama kubwa zaidi kwenye mbuga za wanyama barani Afrika.
Wawili hao wamefikia kwenye hoteli ya Faru Faru Lodge ambayo ni miongoni wa himaya za Singita zilizo katikati kabisa mwa mbuga hiyo kiasi ambacho wakati mwingine wageni huwezi kuwaona wanyama wakiwa wamejipumzisha kwenye vyumba vyao.

Msanii Jux akiangalia wanyama

Madiko diko kwa sana......

Akipost picha ya Vanessa akiwa kwenye Jacuzzi, mbele kukiwa na glasi mbili za champagne, akifurahia mandhari ya mbuga hiyo, Jux ameandika: Day 1 at Sasakwa Lodge was nice but the queen arrived on day 2 so we had to upgrade for that better view Farufaru is almost as dreamy as her #Tanzania #Serengeti #Vacation.”
Naye Vee kwenye picha hiyo hiyo aliyoiweka Instagram, aliandika: Reboot in session #SheKing #OurSingita. Kwenye picha nyingine aliandika #Day 1 at Faru Faru. Much needed vacay. #Safari #Tanzania #Serengeti #Africa #UtaliiwaNdani #OurSingita.”
Tazama picha zaidi:


Kwa upande wa Msanii Mrisho Mpoto, alipanda Mlima Mrefu kuliko wote Afrika, Kilimanjaro
222

Juxr
Mpoto Kileleni
rrr
rrx4

Pole pole ndio mwendo....

Habari hii kwa hisani ya Bongo5.com