Thursday 7 July 2016

TAARIFA KWA UMMA: TAARIFA YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUHUSU MALALAMIKO YA KAMPUNI YA FRIEDKIN CONSERVATION FUND JUU YA UMILIKI WA KITALU CHA UWINDAJI



1.    UTANGULIZI
Wengert Windrose Safaris Ltd (WWS) ni mojawapo ya kampuni tanzu mbili za Friedkin Conservation Fund (FCF) zinazojihusishanashughuli za uwindaji wa kitalii hapa Tanzania.  Kampuni nyingine ni Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) Ltd. Kampuni hizo ziliwasilisha maombi ya kumilikishwa vitalu kumi (10) vya uwindaji wa kitalii kwa msimu wa 2013-2018 kufuatia tangazo la Serikali lililotolewa tarehe 10 Februari 2011. Orodha ya vitalu vilivyoombwa imeoneshwa (Jedwali Na. 1). Kabla ya ugawaji wa mwaka 2011, kampuni hizo zilikuwa zinamiliki vitalu 14 (Jedwali Na. 2).
Jedwali Na. 1. Vitalu vya Uwindaji vilivyombwa na vile walivyomilikishwa makampuni ya Fredkin Conservation Fund kwa kipindi cha uwindaji cha 2013-2018.
Jina la Kampuni
Vitalu vilivyoombwa (2013-2018)
Vitalu vilivyogawiwa
(2013-2018)
WENGERT WINDROSE SAFARIS
1.    Moyowosi GR South
1.    Moyowosi GR South
2.    Lake Natron GCA (North-South)
2.    Lake Natron GCA (North-South)
3.    Lake Natron GCA (N)

4.    Moyowosi GR Njingwe 2

5.    Moyowosi GR Njingwe 3

TANZANIA GAME TRACKERS SAFARIS LTD

1.    Ugalla GR (South)
1.    Ugalla GR (South)
2.    Ugalla GR (North)
2.    Ugalla GR (North)
3.    Ugalla GR (Central)
3.    Moyowosi GR Njingwe 1
4.    Moyowosi GR Njingwe 1
4.    Maswa Kimali
5.    Maswa Kimali
5.    Maswa Mbono

Jedwali Na. 2. Vitalu vilivyokuwa vinamilikiwa na kampuni za Wengert Windrose Safaris Ltd na Tanzania Game Trackers Safaris Ltd.


Jina la Kampuni
Vitalu vilivyoombwa (2013-2018)
WENGERT WINDROSE SAFARIS
1.    Moyowosi GR Njingwe South
2.    Muhesi GR
3.    Kizigo GR East
4.    Kizigo GR Central
5.    Lake Natron GCA (North)
TANZANIA GAME TRACKERS SAFARIS LTD

1.    Monduli Juu Open Area
2.    Kizigo GR (West)
3.    Maswa GR (Kimali)
4.    Maswa GR (Mbono)
5.    Ugalla GR (East)
6.    Ugalla GR (West)
7.    Moyowosi GR Njingwe North
8.    Makere/Uvinza FR
9.    Moyowosi GR (Central)

Baada ya matokeo ya ugawaji wa vitalu Kampuni zote mbili (TGTS na WWS) ziliwasilisha rufaa kwa Waziri wa Maliasili na Utalii kupitia Kamati ya Ushauri wa Ugawaji Vitalu (iliyokaa January 2012) kutaka kufahamu sababu za kutokupewa baadhi ya vitalu walivyoomba kikiwepo cha Lake Natron Game Controlled Area (North).  Sababu za kutokupewa vitalu hivyo vilivyoombwa iliwekwa bayana kuwa ni kutokana na ushindani mkubwa. Ushindani uliongezeka zaidi kutokana na mabadiliko ya sheria ambapo kifungu cha 39(3)(b) ya Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 kinataka kampuni zitakazomilikishwa vitalu; asilimia 85 ziwe zinamilikiwa na watanzania na  asilimia 15 wageni.
Kamati ilipendekeza mgawo kwa kuzingatia matakwa ya sheria na ushindani, hali ambayo ilisababisha kampuni hizo zisigawiwe vitalu vinavyokidhi idadi iliyoombwa na maeneo yaliyokuwa wamemilikishwa.
2.    YALIYOJITOKEZA
2.1. Mgogoro wa Lake Natron Game Controlled Area (North)
·         Kutokana na WWS kutogawiwa kitalu cha Lake Natron Game Controlled Area (North) ambacho kampuni hiyo ilikuwa inakitumia hapo awali kwa shughuli za uwindaji wa kitalii, iliwasilisha rufaa kwa Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii.

·         Tarehe 21 Novemba 2011, Kamati ya Ushauri wa Ugawaji Vitalu (KUUV) ilimshauri Mhe. Waziri kuwa ili kusuluhisha mgogoro huo, kampuni ya GMS igawiwe kitalu cha Ruvu Masai GCA ambacho walikiomba na Lake Natron GCA (North) wagawiwe WWS. Hata hivyo, Mhe. Waziri hakuafiki ushauri wa Kamati.

·         Tarehe 25 Novemba 2011 KUUV ilikutana na WWS kusikiliza maelezo ya ufafanunuzi kuhusu malalamiko yao.

·         Tarehe 12 Desemba 2011, KUUV iliitisha kikao cha pamoja kati ya WWS na GMS kujadili uwezekano wa kutafuta muafaka wa suala la umiliki wa kitalu cha Lake Natron GCA (North).

·         Tarehe 13 Desemba 2011, WWS ilikutana na GMS na kujadiliana makubaliano ya kibiashara juu kitalu chake cha Lake Natron GCA (North). Hata hivyo, kwa mujibu wa WWS, ilibainika baadae kuwa makubaliano hayo yasingeweza kutekelezwa kwa sababu kulikuwa na mchakato wa kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Jamii (Wildlife Management Area).

 WWS ilidai kuwa ilikuwa imeingia mkataba wa matumizi ya ardhi na vijiji 33 katika eneo hilo hilo, hali ambayo ingesababisha mgogoro.

·         Kutokana na hali hiyo WWS ilishauri KUUV iendelee kufikiria ombi lao la kubakia na kitalu hicho kwa kuzingatia sheria, mikataba na masuala ya kiikolojia. Sababu za kiikolojia zilizobainishwa na WWS ni pamoja na kupinga eneo la Lake Natron GCA North kugawanywa kuwa vitalu viwili (Lake Natron GCA (North) na Lake Natron GCA (North-South).

·         Idara ya Wanyamapori ilihakiki ramani za vitalu vya uwindaji wa kitalii kabla ya kuzigawa kwa kampuni zilizokuwa zimepata mgawo wa vitalu kama zilivyowasilishwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kwenye KUUV. Uhakiki wa ramani hizo ulibaini kasoro za majina ya baadhi ya vitalu ambayo hayakuzingatia uhalisia wa kijiografia na asili ya eneo na hivyo kupendekeza marekebisho ya majina hayo.

Eneo
Jina la kitalu
Pendekezo la jina jipya
Lake Natron GCA
North-South
North
North
East
South-West
West
Selous GR
MHJ1
MJ1
MHJ2
MH1
MHJ3
MJ2

·         Ramani za vitalu ziligawiwa mwezi Oktoba 2012 kwa kampuni za uwindaji wa kitalii zikiwa na mabadiliko ya majina hayo. Baada ya mgawo ramani hizo, WWS ilikuja na hoja mpya kuwa kitalu chake cha Lake Natron GCA North-South kimebalishwa (swapped) na kupewa kampuni ya GMS. Ramani ya Lake Natron GCA North-South iliyofanyiwa marekebisho ya jina ilionesha ukubwa wa kitalu ulibaki vile vile na katika eneo na daraja lile lile pamoja na jira  za mpaka (GPS coordinates) zikiwa zile zile. WWS iligeuza madai hayo mapya kuwa hoja ya msingi badala ya hoja za awali.

·         Baada ya hapo suala hilo likageuka kuwa mgogoro kati ya Serikali, WWS na GMS kwamba kuna udanganyifu umefanyika wa kubadilisha vitalu.

·         Katika kikao cha tarehe 24 Mei 2013, kati ya Idara ya Wanyamapori, WWS, GMS, TAWIRI, na Kitengo cha Sheria cha Wizara; Mkuruguenzi wa GMS alitaarifu kuwa katika mojawapo ya majadiliano kati ya GMS na WWS kuwa WWS iliiomba GMS kuiuzia kitalu chake cha Lake Natron GCA North lakini GMS ilikuwa tayari kuiuzia safari na siyo kitalu.

·         Baada ya GMS kukataa ombi lao, WWS ilianza kampeni za kuichafua kampuni ya GMS ikiwa ni pamoja na tukio la Reno-Nevada, Marekani wakati kampuni hizo zikiuza safari za uwindaji wa kitalii Januari, 2015. Katika tukio hilo WWS iliifanyia fujo GMS kuwa kampuni hiyo inafanya utapeli kwa kusambaza vipeperushi vinavyopotosha kwamba inamiliki kitalu cha Lake Natron GCA North.

·         Hatua hiyo iliichafua GMS na kusababisha Mkurugenzi wake Bw. Awadhi Abdallah atoe taarifa ‘Safari Club International’ (SCI).  SCI iliingilia kati kutuliza  mgogoro huo.

·         Kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009, kampuni zote za uwindaji wa kitalii ikiwemo WWS zilitakiwa kuondoka katika vitalu tarehe 31 Machi, 2013 baada ya muhula wa umiliki wa vitalu kumalizika ili kupisha umiliki mpya ili kutekeleza mabadiliko mapya yaliyoainishwa katika sheria hiyo. Hata hivyo, WWS iligoma kuondoka na badala yake mwezi Mei 2013 iliamua kwenda Mahakamani kudai haki.

·         Mmiliki mpya wa kitalu cha Lake Natron GCA North ambacho kilibadilishwa jina na kuwa East, kampuni ya GMS aliwasilisha barua ya malalamiko kwa Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori kwamba anashindwa kuendeleza Kitalu pamoja na kujenga kambi ya uwindaji kwa kuwa bado WWS wapo ndani ya Kitalu kinyume cha sheria. Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori aliiandikia WWS barua ya tarehe 20/05/2013 ya kuiamuru kuondoka kwenye kitalu hicho katika muda wa siku tatu.

·         Amri hiyo haikutekelezwa na badala yake WWS ilirudi kwa Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii tarehe 23/5/2013 ikipinga amri ya kuondoka iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyamapori. Aidha, sambamba na hatua hiyo, WWS iliwasilisha Mahakama Kuu-Kitengo cha Biashara kuomba zuio la GMS kufanya shughuli za uwindaji katika kitalu cha Lake Natron GCA East.

·         Mhe. Waziri, alimwagiza Mkurugenzi wa Wanyamapori kuitisha kikao cha wadau wote wanaohusika na mgogoro wa kitalu cha Lake Natron (GCA) (East) ili kulijadili tena suala hili. Hata hivyo kikao hicho hakikufikia muafaka kutokana na WWS kuendelea kushikilia msimamo wa kukitaka kitalu hicho kwa gharama yoyote ile.

·         Katika kikao hicho nyaraka zote muhimu ziliwasilishwa ikiwemo Ripoti ya Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kuhusu Tathimini ya Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii Tanzania toleo la 3.1 ya Februari 2011. TAWIRI ndiyo Mamlaka ya kisayansi ya utafiti wa wanyamapori Tanzania.  Ikumbukwe kuwa, mabadiliko ya majina hayo hayakuathiri ukubwa, mipaka na jira (GPS coordinates) za vitalu.

·         Katika kikao cha tarehe 24 Mei 2013 kilichotajwa awali, WWS iliwasilisha ramani ambayo inadai kuipatia TAWIRI inayoonesha jina na mipaka kitalu cha Lake Natron GCA (North-South) ili kuthibitisha uhalali wa madai yao. Ilipohojiwa kuwa imekuwaje ipate ramani TAWIRI wakati Taasisi hiyo haina mamlaka ya kutoa ramani hizo kwa kampuni za uwindaji, kampuni ya WWS ilieleza kuwa ililazimika kufanya hivyo kwa vile haikuwahi kupewa ramani ya kitalu hicho na Idara ya Wanyamapori, jambo ambalo si kweli.
·         Kikao hakikuridhishwa na maelezo ya WWS ambapo kampuni hiyo ilitahadharishwa kutowatumia watumishi katika ofisi za umma kupata nyaraka za Serikali kinyume na utaratibu. Aidha, WWS iliambiwa kuwa kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa maadili na kinaashiria mazingira ya rushwa – jambo ambalo ni kosa la jinai kwa yule aliyetoa nyaraka hizo na aliyezipokea.
·         Kampuni ya WWS iliendelea kufungua kesi mbalimbali katika Mahakama Kuu ya Ardhi na Mahakama ya biashara bila mafanikio kama ifuatavyo;
                              i.        Miscellaneous Land Application No. 44 of 2013 Wengert Windrose Ltd Versus Green Mile Safari Ltd and Others.

                            ii.        Commercial Case No.113 of 2013 Wengert Windrose Safaris Versus Green Mile Safari Ltd.

                           iii.        Miscellaneous Commercial Case No. 88 of 2013 Wengert Windrose Safaris (T) Ltd Versus Green Mile Safari Ltd

                           iv.        Commercial Case No.115 of 2013 Green Mile Safari Ltd Versus Wengert Windrose Safaris Ltd.

                            v.        Miscellaneous Commercial application No.92 of 2013 Green Mile Safari Ltd Versus Wengert Windrose Safaris Ltd.

                           vi.        Miscellaneous Commercial Cause No.26 of 2013Wengert Windrose Safaris Ltd Versus Green Mile Safari Ltd.

                          vii.        Miscellaneous Commercial Application No.26 of 2013 Wengert Windrose Safari Ltd Versus Awadh Ally Abdallah.

                        viii.        Miscellaneous Commercial application No.68 of 2014 Awadh Abdallah Versus Wengert Windrose Safari Ltd.

·         Tarehe 05/07/2013 Mkurugenzi wa GMS aliwasilisha malalamiko kuwa kampuni ya WWS ilizuia wageni wa GMS wasifanye uwindaji katika kitalu cha Lake Natron GCA (East) ambapo wafanyakazi wa kampuni ya WWS waliandaa hila ya; kuyagonga magari ya GMS yakiwa na watalii; walichimba mashimo kwenye uwanja wa ndege ili kuzuia ndege za GMS zisitue; na walifunga barabara kwa magogo kuzuia magari ya wageni waliokuja kuwinda yasipite.
·         Sambamba na fujo hizo, kampuni ya WWS iliwachochea wanakijiji cha Armani, Longido kufanya vurugu dhidi ya wageni wa GMS. Hali hii ilisababisha Mkuu wa Wilaya ya Longido kuitisha Kikao na wawekezaji wote na kutoa onyo dhidi ya Mwekezaji yeyote ambaye angewachochea wananchi kuvuruga amani.
Kimsingi, kampuni za FCF (WWS na TGTS) zimekuwa na tabia ya ubabe na usumbufu katika Tasnia ya uwindaji wa kitalii dhidi ya kampuni nyingine na Serikali. Tabia hizi zimeendelea katika sehemu mbalimbali ambapo kampuni hizi zinafanya shughuli za utalii.

Madai kuwa kampuni za FCFzinanyanyaswa na Idara ya Wanyamapori sio ya kweli. Kimsingi, busara na uvumilivu mkubwa vimetumika kuendelea kufanya kazi na kampuni hizo. Tunapenda kubainisha mifano ifuatavyo:-

      i.        Ugawaji wa vitalu kwa uwindaji mwaka 2013-2018 umefanywa kufuata taratibu zote kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 na kanuni zake za mwaka 2010 zilizorekebishwa 2015.

    ii.        Hata pale ambapo kampuni zote mbili (TGTS na WWS) hazikuridhika na matokeo ya ugawaji wa vitalu Wizara ilikuwa tayari kuwasikiliza zaidi ya mara moja kupitia KUUV.

   iii.        Pamoja na mbinu zisizoridhisha za kampuni hizo za FCF, ikiwemo kuwachafua baadhi ya wajumbe wa Kamati na watumishi, bado Wizara iliendelea kujadiliana na WWS na walipokataa na kukaidi maelekezo, Serikali ilikubali kuburuzwa Mahakamani na WWS kwa kuamini kuwa haki itatendeka kama ilivyoainishwa hapo awali. 

   iv.        Pamoja na WWS kushindwa kesi Mahakamani, Wizara ilionyesha uvumulivu kwa kutotumia nguvu kuwaondoa kwenye kitalu ambacho hawakumilikishwa kihalali.

    v.        Pamoja na WWS kuishtaki Wizara Mahakamani, Wizara ya Maiasili na Utalii iliendelea kufungua milango ya majadiliano kila WWS ilipoomba kufanya hivyo.

   vi.        Pamoja na WWS kuzuia Kampuni iliyomilikishwa kitalu kihalali (GMS), kutishia usalama wa wageni wa GMS,  kuifanyia fujo Kampuni ya GMS katika soko la Kimataifa huko Reno, Nevada (Safari Club International) mwezi Januari, 2013, kwa kumwondoa Mkurugenzi Mtendaji wa GMS kwenye Tamasha la Utalii wa Uwindaji, kuikosesha Serikali mapato kutokana na wageni kuondoka, kuchochea wanakijiji wafanye fujo dhidi ya kampuni nyingine, bado hatua za kidiplomasia zimekuwa zinatumika kutafuta suluhu ya kudumu.  Hata hivyo, kila kitu na kila uvumilivu una mwisho.
2.2 Kuhusu Kampuni ya Green Mile Safari Ltd (GMS)
Wizara ya Maliasili na Utalii iliamua kuirejeshea leseni Kampuni ya Green Mile Safari Ltd kufanya shughuli za uwindaji wa kitalii katika vitalu vyake vya Selous GR (MK1), Lake Natron GCA (East zamani North), Gonabis/Kidunda – WMA baada ya kupitia rufaa yake dhidi ya Mkurugenzi wa Wanyamapori kupinga kunyang’anywa leseni.
Kampuni ya GMS ilifutiwa umiliki wa vitalu na leseni zake zote za uwindaji kupitia Taarifa ya Umma iliyotolewa tarehe 11 Julai, 2014.  Uamuzi huo ulifikiwa kutokana na ukiukwaji Sheria na Kanuni za Uwindaji wa Kitalii uliofanywa na wageni wa GMS wakati wakiwinda kwenye kitalu cha Gonabis/Kidunda WMA mwaka 2012. Matukio ya ukiukwaji yalibainishwa kupitia picha video (DVD) iliyowasilishwa Bungeni na Mhe. Peter Msigwa (Mb) wakati wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2014.
Kampuni ya GMS ilirejeshewa leseni kunatokana na hoja zilizoainishwa kwenye rufaa yake na tafsiri ya Sheria ya Wanyamapori Na.5 ya Mwaka 2009 katika kifungu 38(12)(c) ikisomwa kwa pamoja na – kanuni ya 17 (2) (b) ya Kanuni za Uwindaji wa Kitalii za mwaka 2010 zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2015.  Hukumu ya Mahakama iliyotolewa tarehe 31 Machi, 2015 na Jaji Songoro dhidi ya Kampuni ya WWS pamoja na tafsiri na ushauri kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa barua Kumb. Na. AGC/A.130/2J/9 ya tarehe 14 Desemba, 2015 aliyoeleza kuwa kifungu cha 38(12)(c) kinampa mamlaka Waziri wa Maliasili na Utalii kufuta umiliki wa kitalu endapo Mahakama itakuwa imemtia hatiani mmiliki wa kitalu.
Ni kwa msingi huu Wizara ilitengua maamuzi yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyamapori na kuirejeshea haki Kampuni ya GMS kufanya shughuli zake za uwindaji wa kitalii.  Aidha, Wizara ilitoa maelekezo kuwa waliohusika na uvunjifu wa sheria, kanuni na taratibu za uwindaji zilizofanywa na wageni wa kampuni ya GMS huko kwenye kitalu cha Gonabis/Kidunda WMA; wakiwamo Askari wa Wanyamapori (waliosimamia uwindaji) pamoja na Mwindaji Bingwa wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu.

Pamoja na hatua hizi, Wizara ilielekeza kampuni ya Green Mile Safari Ltd, irudi kwenye vitalu vyake na kuendelea na shughuli za uwindaji na kuwa Serikali itawapatia ulinzi kila itakapohitajika. Kufuatia uamuzi huo, kampuni ya WWS ilifungua Shauri tarehe 25 Mei 2016 katika Makahama Kuu, Kitengo cha Biashara kuomba zuio dhidi ya utekelezaji wa amri ya Wizara ya kuiamuru kuondoka katika kitalu cha Lake Natron GCA East ifikapo tarehe 31 Mei 2016. Shauri hilo lilisikilizwa na Jaji Mwambegele, J. ambapo ombi hilo halikukubaliwa.

3. HITIMISHO
Maelezo haya yanabainisha mtiririko wa chanzo cha mgogoro na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa ili kufikia suluhu yake kama ifuatavyo;

      i.        Taarifa za kukaribisha maombi kutoka kwa wadau wote wenye nia ya kufanya biashara ya uwindaji wa kitalii zilitolewa kwa uwazi kupitia vyombo vya habari.

    ii.        Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu (KUUV) ilitekeleza majukumu yake kwa kutumia taarifa halali zilizowasilishwa na kila muombaji wa vitalu. Aidha, maamuzi yaliyofanyika kwa uwazi na kuzingatia  sheria, kanuni na ushindani uliokuwepo.

   iii.        Kifungu cha 38(14) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 kinatoa fursa kwa kampuni ambazo hazikuridhika na matokeo ya ugawaji kukata rufaa kwa Mhe. Waziri na kusikilizwa kwa utaratibu wa mapitio ya kiutawala (administrative review).   Aidha, Kifungu cha 38(16) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 kinatoa fursa kwa kampuni ambazo hazikuridhishwa na uamuzi wa Mhe. Waziri kukata rufaa Mahakama Kuu.

   iv.        Baada ya kutoridhika na maamuzi mbalimbali Kampuni ya WWS ilitumia fursa hizo zote za kisheria pamoja na vikao vya usuluhishi na baada ya kubaini kwamba haikufanikiwa kufikia azima yake; ikaamua kuanzisha tuhuma mpya na kutumia mbinu mbadala zenye hila ili kuuaminisha umma, taasisi za kimataifa na vyombo vya juu vya Serikali kwamba imedhulumiwa haki yake. 

    v.        Mwenendo mbaya wa uhusiano baina ya kampuni tanzu za FCF na wananchi na wadau wengine pia umeoneshwa na Mwiba Holdings Ltd ambayo imekuwa ikituhumiwa kunyanyasa na kutesa wananchi, kuvunja mikataba halali kati yake na wananchi kwenye eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii - MAKAO(MAKAO Wildlife Management Area ). Hivi karibuni mojawapo ya magari ya uwindaji ya kampuni za FCF ilikamatwa ikisafirisha magunia kumi na moja (11) ya bangi kwenda nchi jirani ya Kenya.

4.MSIMAMO WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Vitendo vya kampuni ya Wengert Windrose Safaris Ltd sio tu vinawanyima haki wadau wengine wa tasnia ya uwindaji wa kitalii nchini bali pia vinainyima Serikali mapato; fursa ya jamii kushiriki na kufaidika na shughuli za uhifadhi; pamoja na kuiharibia jina nje ya nchi kwa kujenga hisia ya kutokuwepo kwa hali ya usalama. Hii inajitokeza hasa pale kampuni hizi zinapotishia maisha ya wageni wa kampuni ya GMS iliyojitokeza Lake Natron GCA East. Aidha, kampuni hii inachafua taswira ya Serikali yetu dhidi ya wananchi na watalii wanaoitembelea Tanzania kama wawindaji.
Kwa maslahi na heshima ya Taifa letu na tasnia ya uwindaji Wizara ya Maliasili Asili na Utalii imetoa msimamo ufuatao:
·         Kuitaka Kampuni ya WWS kuondoka mara moja katika kitalu ambacho haijamilikishwa kihalali.

·         Kwamba, FCF imewekeza nchini na kupewa hadhi ya uwekezaji mahiri (SIS) na inachangia maendeleo ya jamii.  Hata hivyo, FCF ijue kuwa hadhi hii ya SIS sio kibali cha kudharau uhuru wa nchi; kuvunja Sheria zetu; kushawishi wananchi kuvunja sheria; na kutishia uhuru na haki za raia wa kigeni wanaoishi kihalali au kutembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

·         Kwamba, Tanzania ni nchi huru (sovereign state) na kwamba Sheria ni msumeno, hivyo makampuni ya kigeni hayana kinga pale wanapovunja sheria za nchi.

·         Kampuni za FCF ziache kuwarubuni na kuwatumia wananchi kufanya fujo (to use villagers and incite violence against competitors) kwa manufaa yao kibiashara hakikubaliki na ni uvunjaji wa Sheria za nchi.

·         Wizara inashauri kuwa kampuni zinazojihusisha na shughuli za utalii zizingatie na kuheshimu Sheria na Kanuni za nchi wakati wote zipofanya shughuli zao Tanzania.

Imetolewa na;
Wizara ya Maliasili na Utalii
06 Julai, 2016

No comments:

Post a Comment