Sunday, 3 July 2016

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YANYAKUA TUZO MBILI KATIKA MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM 2016 - SABASABA

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akikabidhi tuzo mbili za ushindi ilizoshinda Wizara yake katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwa viongozi wa Kamati ya Maonesho ya Wizara hiyo jana tarehe 01 Julai, 2016 katika viwanja vya Sabasaba. Tuzo hizo ni Mshindi wa Kwanza katika kundi la Wizara na Taasisi za Serikali na Mshindi wa pili katika kundi la Mshindi wa Jumla wa Maonesho hayo. Tuzo hizo zilikabidhiwa na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame aliyekuwa Mgeni Rasmi akiongozana na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa tano kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waoneshaji wa Wizara yake muda mfupi baada ya kupokea tuzo mbili za ushindi katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam jana tarehe 01 Julai, 2016 katika viwanja vya Sabasaba. Tuzo hizo ni Mshindi wa kwanza katika Kundi la Wizara na Taasisi za Serikali na Mshindi wa Pili katika Kundi la Mshindi wa Jumla.
 Baadhi ya Waoneshaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakifurahia ushindi wa tuzo hizo. Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ni moja ya mabanda yanayovutia zaidi katika Maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu 2016, kwa kuwa na mchanganyiko wa mambo mbali mbali yanayoelimisha kuhusu uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Utalii. Katika banda hilo zipo pia fursa za kuwaona wanyama hai kama vile Simba, Nyati, Chui, Mamba, Ndege mbalimbali n.k. Kwa upande wa Utalii wa Ndani zipo fursa za kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa gharama nafuu ya Tsh. 10,000 kwa watoto na Tsh. 20,000 kwa watu Wazima ikiwa ni nauli ya kwenda na kurudi, Aidha kwa wale watakaopenda kulala itawagharimu Tsh. 50,000.
 Baadhi ya Waoneshaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakifurahia tuzo hizo katika banda la Wizara hiyo. 
Taswira ya tuzo hizo.

No comments:

Post a Comment