Ray C |
Katika Misemo ya kale upo msemo usemao aisifuye mvua,imemnyea.
Usemi huu unaweza kufananishwa na kauli ya
Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rehema
Chalamila almaaruf Ray C,ambaye hivi karibuni alitoa wito kwa serikali
kuwanyonga wale wote wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Mwanamuziki huyo hivi sasa yuko kwenye kliniki
maalum akipata tiba kutokana na kuathiriwa na matumizi makubwa ya dawa
za Kulevya, baada ya kupata msaada kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete wa
Tanzania.
CHANZO; BBC Swahili
No comments:
Post a Comment