I.
UTANGULIZI
1.
Mheshimiwa
Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu baada ya kupokea Taarifa iliyowasilishwa Bungeni na
Mwenyekiti wa
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, likubali kujadili
na kupitisha Makadirio ya Mapato
na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
2.
Mheshimiwa
Spika, awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutuwezesha
kukutana katika Bunge hili Tukufu la Bajeti. Naomba pia nitumie nafasi hii
adhimu kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa
kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, nawapongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa
Rais na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu. Tunamuomba
Mwenyezi Mungu awalinde na kuwaongoza katika kulitumikia Taifa letu kwa
uadilifu ili liendelee kuwa na amani, upendo na ustawi.
3.
Mheshimiwa
Spika, napenda pia kukupongeza wewe Mheshimiwa Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wa
Bunge kwa kuchaguliwa kuliongoza Bunge letu Tukufu. Pia, nawapongeza
walioteuliwa kuwa Mawaziri na Manaibu Waziri kuziongoza Wizara mbalimbali na
Waheshimiwa Wabunge wote kwa kupewa ridhaa na wananchi wao kuwawakilisha katika
Bunge hili Tukufu. Vilevile, nawapongeza Wenyeviti wa Kamati mbalimbali za
Kudumu za Bunge tuliowachagua kuongoza Kamati zetu za Bunge. Ni matumaini yangu
tutashirikiana vyema katika kukamilisha na kufanikisha majukumu yetu ili
kuliongoza Bunge letu kwa ufanisi.
4.
Mheshimiwa
Spika, nitumie nafasi hii pia, kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri wa Maliasili
4
na
Utalii. Jukumu hili ni kubwa, naamini kwa uwezo alionijalia Mwenyezi Mungu,
miongozo ya viongozi wa Serikali na kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali
nitaweza kutekeleza majukumu yangu ya kusimamia kwa ufanisi Sera na Sheria za
sekta zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
5.
Mheshimiwa
Spika, natoa shukurani za dhati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Utalii chini ya Mwenyekiti wake Mhandisi Atashanta Justus Nditiye (Mb.) ambayo
ilijadili, kushauri na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya
Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Naomba kuliarifu Bunge lako
Tukufu kwamba maoni, ushauri na maelekezo yaliyotolewa na Kamati yamezingatiwa
katika bajeti hii.
6.
Mheshimiwa
Spika, naomba kuungana na wenzangu kutoa salamu za pole kwa waathirika wa majanga mbalimbali yaliyolikumba
Taifa ikiwa ni pamoja mafuriko na matukio ya wananchi kuuawa na wanyamapori
wakali. Kipekee natoa pole kwa familia za watumishi wa Wizara ambao wamefikwa
na mauti wakati wakitumikia Taifa. Tuendelee kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu
awapumzishe kwa amani. Amina.
II.
TATHMINI YA HALI YA SEKTA YA
MALIASILI NA UTALII NCHINI
7.
Mheshimiwa
Spika, Sekta ya Maliasili na Utalii inasimamia sekta ndogo za Wanyamapori, Misitu, Ufugaji
Nyuki, Utalii na Malikale. Maeneo yaliyohifadhiwa kisheria yanajumuisha misitu
ya hifadhi na mbuga za wanyama ambayo ni hekta milioni 28 sawa na asilimia 33
ya ardhi ya Tanzania.
8.
Mheshimiwa
Spika, maeneo yaliyohifadhiwa kisheria yanakabiliwa na ongezeko la uvamizi hivyo kusababisha migogoro
baina ya
5
hifadhi
zetu na watu wanaovamia kulima au kufuga ndani ya hifadhi. Kutokana na hali hii
kumekuwa na mwingiliano wa maamuzi ambapo wananchi wanahamasishwa kuendelea
kutumia maeneo ya hifadhi kinyume cha sheria. Vilevile, kumekuwa na matamshi
mbalimbali yenye nia ya kubadili matumizi na hadhi ya maeneo yaliyohifadhiwa
kwa ajili ya makazi, kilimo na mifugo hali inayotishia uhifadhi kwa ujumla.
9.
Mheshimiwa
Spika, faida za uhifadhi ni dhahiri na ni kwa manufaa mapana ya kizazi cha sasa na
kijacho. Hivyo basi, ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha analinda
rasilimali hizo. Wizara itaendelea na jitihada za kuhifadhi na kutatua migogoro
inayogusa maeneo ya hifadhi kwa kushirikisha wadau wote.
a. Sekta
ndogo ya Wanyamapori
10.
Mheshimiwa
Spika, Wizara inasimamia rasilimali za wanyamapori kwenye Hifadhi za Taifa 16 zenye
ukubwa wa kilometa za mraba 57,365.05 na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro lenye
ukubwa wa kilometa za mraba 8,292. Aidha, inasimamia Mapori ya Akiba 28 yenye
kilometa za mraba 114,782.47, Mapori Tengefu 42 yenye ukubwa wa kilometa za
mraba 58,565.02,
11.
Mheshimiwa
Spika, rasilimali wanyamapori imegawanyika katika aina mbili za matumizi ambayo ni ya
uvunaji na yasiyo ya uvunaji. Matumizi ya uvunaji yanahusisha biashara ya
wanyamapori hai na uwindaji wa wanyamapori ambayo yanafanyika ndani ya mapori
ya akiba, mapori tengefu, Maeneo ya Jumuiya za Kuhifadhi Wanyamapori (WMAs) na
maeneo ya wazi. Matumizi yasiyo ya uvunaji yanahusisha utalii wa picha na kuona
na mafunzo ambayo hufanyika ndani ya Hifadhi za Taifa, Eneo la Hifadhi ya
Ngorongoro na maeneo mengine yote yenye wanyamapori. Matumizi hayo yanatoa
fursa kubwa za uwekezaji na ajira kwa Watanzania wengi.
6
12.
Mheshimiwa
Spika, Maeneo yaliyohifadhiwa yanachangia uhifadhi wa bioanuai mbalimbali zilizo hatarini kutoweka kama
faru, tembo, mbwa mwitu, simba, duma, swala-twiga (gerenuk) pamoja na jamii za
ndege mbalimbali kama bungu-nusu (shoebill stork) na kasuku mapenzi (love
bird). Pia maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na ardhioevu, ni vyanzo muhimu vya maji
kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, kilimo cha umwagiliaji, matumizi ya umeme na
uzalishaji viwandani. Vilevile, maeneo hayo huchangia katika uzalishaji wa hewa
safi na kuondoa hewa ukaa (Carbon sink) na hivyo kuwa msingi wa maisha bora kwa
viumbe hai katika sayari dunia.
13.
Mheshimiwa
Spika, baadhi ya maeneo yaliyohifadhiwa yana hadhi ya kimataifa kwa kuwekwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi
wa dunia (World Heritage Sites). Maeneo hayo ni pamoja na Pori la Akiba Selous,
Hifadhi ya Taifa Serengeti, Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro na Eneo la Hifadhi ya
Ngorongoro. Maeneo ya Hifadhi Asilia (Biosphere Reserve) ambayo ni Pori la
Akiba Selous na Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara. Aidha, Hifadhi ya Ngorongoro ni
moja ya maajabu saba ya dunia. Kutokana na kuwekwa kwenye hadhi hizo, maeneo
hayo yamekuwa kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani na nje ya nchi yetu.
14.
Mheshimiwa
Spika, Sekta ya Wanyamapori inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na:- uharibifu wa maeneo ya
hifadhi za wanyamapori kutokana na shughuli za binadamu na athari za mabadiliko
ya tabianchi; ujangili; moto; uvamizi wa mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa;
upungufu wa watumishi na vitendea kazi; na kuingia na kuzagaa kwa silaha
hususan za kivita. Aidha, baadhi ya vitalu vya uwindaji wa kitalii vimekosa
ubora unaotakiwa kwa kutokuwa na wanyama wa kutosha wenye nyara zinazoweza
kuwindwa. Hali hii inasababishwa na ujangili pamoja na baadhi ya wananchi
kuingiza mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa. Hii
imesababisha wimbi la wawekezaji kurejesha baadhi ya vitalu hivyo
7
kuikosesha
Serikali mapato ambayo ingepatikana kupitia uwindaji. Katika mwaka 2015/2016,
vitalu tisa vimerejeshwa na kufanya idadi ya vitalu vilivyorejeshwa kuwa 44
kuanzia mwaka 2013.
Wizara
itaendelea kutekeleza Mkakati wa Kupambana na na Ujangili wa mwaka 2014-2019
kwa kuimarisha doria, intelijensia na upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya
kudhibiti ujangili. Aidha, Wizara itaendeleza juhudi za ushirikiano na nchi
jirani katika maeneo ya rasilimali wanyamapori zinazovuka mipaka.
b. Sekta
ndogo ya Misitu
15.
Mheshimiwa
Spika, Tathmini ya rasilimali za misitu iliyofanyika mwaka 2010 hadi 2013 ilibainisha kuwa
Tanzania ina misitu yenye ukubwa wa hekta 48.1 milioni. Kati ya hekta hizo,
asilimia 93 ni misitu ya mataji wazi (woodland) na asilimia 7 ni misitu
iliyofunga. Mgawanyo wa mamlaka za usimamizi wa misitu hiyo ni kama ifuatavyo:-
Serikali Kuu hekta milioni 19.24 ambayo ni asilimia 34.5; Serikali za Mitaa
kupitia Halmashauri za Wilaya hekta million 3.1 ambayo ni asilimia 6.5; misitu
iliyo katika ardhi za vijiji ni hekta 21.9 ambayo ni asilimia 45.7; na watu
binafsi na vikundi wanasimamia hekta milioni 3.5 ambayo ni asilimia 7.3. Eneo
lililobaki lenye ukubwa wa hekta 2.87 sawa na asilimia 6.0 ni ardhi huria.
16.
Mheshimiwa
Spika, Tanzania ina miti yenye meta za ujazo milioni 1,046.9 inayoweza kuvunwa kibiashara
kati ya jumla ya meta za ujazo milioni 3,322 za misitu yote nchini. Hata hivyo,
maeneo ambayo uvunaji wa mazao ya misitu unaweza kufanyika kisheria ni hekta
milioni 20 ambayo ni sawa na asilimia 35 ya ujazo wote wa misitu. Zaidi ya
asilimia 70 ya kiasi cha ujazo wa miti unaopaswa kuvunwa kinapatikana katika
mikoa ya Mbeya, Lindi, Ruvuma, Tabora, Katavi na Morogoro.
8
17.
Mheshimiwa
Spika, Tanzania inakadiriwa kuwa na mita za ujazo bilioni 3.3 za miti, kati ya hizo,
mita za ujazo 3.2 bilioni sawa na asilimia 97 ipo katika misitu ya asili na
mita za ujazo 9.9 milioni sawa na asilimia 3 katika misitu ya kupandwa. Nusu ya
ujazo wa miti inapatikana katika maeneo yaliyohifadhiwa kisheria. Mahitaji
halisi ya mazao timbao kwa sasa yanakadiriwa kuwa meta za ujazo milioni 62.3
kwa mwaka. Hata hivyo, ujazo unaoweza kupatikana kutokana na uvunaji
unaofanyika kisheria na kwa njia endelevu ni meta za ujazo milioni 42.8 tu.
Zaidi ya asilimia 70 ya kiasi hiki cha ujazo wa miti unaopaswa kuvunwa
kinapatikana katika mikoa ya Mbeya, Lindi, Ruvuma, Tabora, Katavi na Morogoro.
Takwimu hizi zinaonesha kuwa kuna upungufu wa meta za ujazo milioni 19.5. kwa
mwaka.
18.
Mheshimiwa
Spika, misitu ina umuhimu mkubwa katika uhifadhi wa bioanuai, udongo na vyanzo vya maji
kwa ajili ya kuzalisha umeme na matumizi ya nyumbani, viwandani na umwagiliaji.
Aidha, misitu ni muhimu katika kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwa
kuwa inanyoya hewa ukaa. Vilevile, inatupatia mbao, kuni, mkaa, chakula,
malisho ya mifugo, dawa, kivuli na makazi ya wanyama.
19.
Mheshimiwa
Spika, misitu inachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa Taifa kwa kutoa zaidi ya
asilimia 75 ya vifaa vya kujengea na huchangia zaidi ya asilimia 90 ya nishati
inayotumika nchini. Vilevile, Misitu ni nguzo ya maendeleo ya uchumi kutokana
na mchango wake katika kuchangia fedha katika mfuko wa Serikali. Sekta ya
Misitu inachangia kwa takribani asilimia 3 ya ajira rasmi nchini; na ajira
isiyo rasmi inafikia watu milioni 3.
9
20.
Mheshimiwa
Spika, kumekuwepo na utegemezi mkubwa wa misitu kama chanzo rahisi na kikuu cha nishati, ambapo uvunaji
mkubwa wa mkaa umeathiri sana ubora wa misitu. Mahitaji ya mazao ya misitu
yamesababisha kutoweka kwa eneo la misitu linalokadiriwa kuwa na hekta 372,000
kwa mwaka. Hatua inayotakiwa kuchukuliwa kwa ushirikiano na wadau wote ni
kupanda hekta 185,000 za miti kila mwaka kwa kipindi cha miaka 16 ijayo hadi
mwaka 2030 ili kuziba pengo la upungufu uliopo wa mazao ya misitu unaokadiriwa
kuwa meta za ujazo milioni 19.5 kwa mwaka. Wizara inaendeleza ushirikiano na
wadau wa sekta mbalimbali hasa Wizara ya Nishati na Madini,Taasisi zisizo za
Serikali na jamii kwa ujumla ili kupunguza utegemezi wa misitu kama chanzo kikuu
cha nishati viwandani na kwa matumizi ya nyumbani. Vilevile, Wizara kwa
kushirikiana na wadau inahamasisha jamii kutumia nishati mbadala na matumizi ya
majiko banifu. Elimu hii inatolewa kupitia vipindi vya radio na televisheni,
mikutano ya hadhara, makongamamo na warsha.
21.
Mheshimiwa
Spika, Moto umeendelea kuwa changamoto kwa uhifadhi wa misitu. Takwimu zinaonesha kuwa, takriban asilimia
10-14 ya maeneo ya misitu Tanzania yanaathirika na moto kila mwaka. Hii ni
wastani wa hekta milioni sita za maeneo ya misitu kwa mwaka. Katika kutatua
changamoto hii, Wizara imeendelea kusafisha barabara za kuzuia moto kuingia
msituni na kutoa elimu ya jinsi ya kupambana na moto kwa jamii inayozunguka
misitu ya asili na mashamba. Vilevile, Wizara itaendelea kutunza miundombinu ya
kufuatilia na kubaini matukio ya nchini.
c. Sekta
Ndogo ya Ufugaji Nyuki
22.
Mheshimiwa
Spika, ukubwa wa misitu tuliyonayo unaweza kukidhi uzalishaji wa takribani tani 138,000 za asali na tani
9,200 za nta kwa mwaka. Hata hivyo, mpaka sasa uzalishaji umefikia tani 34,000
za asali sawa
10
na
asilimia 24.6 ya uwezo huo na tani 625 za nta peke yake. Katika kuongeza
msukumo wa uzalishaji wa mazao ya nyuki na huduma ya uchavushaji mimea, Wizara
imeainisha maeneo ya kuanzisha hifadhi 46 za nyuki zenye ukubwa wa takriban
hekta 143,936.78. Kati ya hizo, hifadhi 26 zenye ukubwa wa hekta 74,323.78
zitamilikiwa na Serikali za vijiji na 20 zenye ukubwa wa hekta 69,613 ni za
Serikali Kuu.
23.
Mheshimiwa
Spika, ufugaji nyuki una mchango mkubwa katika uhifadhi na ukuaji wa uchumi. Kwa
kuhifadhi misitu ya asili na ya kupandwa tunapata fursa ya kufanya shughuli za
ufugaji nyuki katika maeneo hayo. Shughuli hizo zinasaidia kuhifadhi misitu
yetu ambayo ni takribani hekta 48.1 milioni nchi nzima. Ufugaji nyuki umepewa
msukumo kwa kuanzishiwa mafunzo maalumu ngazi ya shahada katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam na hivyo kuongeza idadi ya wataalamu wa kuweza kusimamia sekta
ndogo ya ufugaji nyuki. Vilevile, Kitengo cha ufugaji nyuki kimeimarishwa kuwa
Idara inayojitegemea ili kutoa msukumo stahili katika shughuli za ufugaji
nyuki.
24.
Mheshimiwa
Spika, takwimu zinaonesha kuwa mahitaji katika soko la ndani yanaongezeka sanjari na
soko la dunia ukilinganisha na uzalishaji na upatikanaji wa asali. Aidha,
Tanzania ni miongoni mwa nchi 5 za Afrika zinazoruhusiwa kuuza asali yake
katika soko la Ulaya. Takwimu za usafirishaji wa mazao ya nyuki nchi nje ni
wastani wa tani 278.6 za asali na tani 347.3 za nta. Ufugaji nyuki una fursa ya
kuzalisha pia mazao mengine yanayotumika kwa urembo na tiba ambayo yanahitajika
katika soko la dunia ikiwemo gundi (propolis),
maziwa ya nyuki (royal jelly), chavua
(pollen) na sumu ya nyuki (bee venom). Naomba kutumia fursa hii
kuwahimiza Waheshimiwa Wabunge kuhamasisha wananchi katika majimbo yetu
kushiriki katika shughuli za ufugaji nyuki kwa kuwa zinatoa fursa nyingi
zikiwemo kuanzisha
11
viwanda
vya kuhudumia mahitaji ya sekta ya ufugaji nyuki, ajira, huduma ya uchavushaji
wa mimea na manufaa mengine.
25.
Mheshimiwa
Spika, Sekta ya ufugaji nyuki inakabiliwa na changamoto ya baadhi ya wafugaji nchini kuzalisha mazao ya nyuki
yasiyokidhi viwango vya ubora, hivyo kusababisha kutopata bei nzuri katika soko
la ndani na nje. Wizara yangu itaendelea kutoa elimu ya uvunaji, uchakataji na
ufungashaji wa mazao yatokanayo na nyuki ili kukidhi viwango vya ubora.
d. Sekta
ndogo ya Utalii
26.
Mheshimiwa
Spika, Sekta ndogo ya Utalii imeshika nafasi ya kwanza katika kuliingizia Taifa fedha
za kigeni kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo (2012 – 2015). Fedha hizo ni
sawa na wastani wa Dola za Kimarekani milioni 2,002 kwa mwaka ambayo ni
asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni nchini. Kwa mwaka 2015, idadi ya
watalii waliongia nchini ilikuwa 1,102,619. Sekta huchangia takriban ajira
500,000 za moja kwa moja na ajira 1,000,000 ambazo si za moja kwa moja. Aidha,
Sekta imeendelea kutoa ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi katika Sekta
mbalimbali zikiwemo kilimo, elimu, mawasiliano, miundombinu, burudani,
usafirishaji na uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa watalii. Maendeleo ya Sekta
ya utalii nchini yamechangiwa na uwepo wa amani na utulivu; ukuaji wa
teknolojia ya habari na mawasiliano; uboreshwaji wa miundombinu; na ubora wa
huduma za malazi na ukarimu. Vivutio vikuu vya Utalii wa Tanzania ni
wanyamapori, upandaji milima, utamaduni, malikale, mandhari na fukwe.
27.
Mheshimiwa
Spika, Sekta ya utalii inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa ya miundombinu bora katika
maeneo yenye vivutio ikiwemo
12
huduma
za maji, umeme na barabara. Aidha, hatuna Shirika la Ndege lenye uwezo wa kuleta
watalii moja kwa moja kutoka katika nchi ambazo ni masoko makuu ya utalii.
Hivyo, Wizara inaishukuru Serikali kwa mpango wa kununua ndege tatu katika
mwaka ujao wa fedha ili kukidhi haja hii katika kipindi cha mpito wakati
Serikali ikiimarisha Shirika la ndege la Taifa.
28.
Mheshimiwa
Spika, matumizi ya kadi za kielektroniki kuingia katika maeneo yaliyohifadhiwa kwa
ajili ya utalii yanakabiliwa na changamoto ikiwemo baadhi ya wageni kutokuwa na
uelewa wa njia hiyo ya malipo. Teknolojia hii inahitaji uwepo wa mtandao wa
intaneti katika maeneo yote ambayo ulipaji unafanyika. Ili kukabili changamoto
hizo, Wizara inaendelea kutoa elimu kwa wageni kuhusu huduma hiyo ambayo
haihitaji matumizi ya fedha taslimu. Wizara inawekeza katika kuimarisha
miundombinu za ulipaji wa mfumo wa mtandao kwa kununua satellite dishes na communication
boosters. Vilevile, inawasiliana na
watoa huduma za kibenki ili kuhakikisha kwamba
huduma za mfumo wa ulipaji kwa mtandao zinapatikana katika maeneo ya hifadhi.
29.
Mheshimiwa
Spika, upo mwamko mdogo wa wananchi katika kutembelea vivutio vya utalii pamoja na kushiriki katika biashara
za utalii pamoja na Serikali kuweka gharama ndogo za viingilio katika Hifadhi
za Taifa kwa Watanzania na raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa sasa, kiingilio
ni shilingi 10,000 kwa Hifadhi zilizopo Kaskazini; shilingi 5,000 hadi 15,000
kwa Hifadhi zilizopo Kusini; na watoto shilingi 2,000 kwa Hifadhi zote nchini.
Magari madogo hutozwa shilingi 20,000 katika hifadhi zote. Katika kukabiliana
na changamoto hii, Wizara itaendeleza kampeni mbalimbali za kuhamasisha
wananchi kushiriki katika shughuli za utalii. Aidha, Wizara imebaini kuwa,
Sekta ya Utalii haijawekwa katika vipaumbele kwenye mipango ya maendeleo ya
Mikoa na Wilaya. Katika kukabiliana na hili, Wizara itatoa elimu ya
13
uhamasishaji
kwa wadau na watoa maamuzi mbalimbali ili sekta hii ipewe kipaumbele stahili
katika mipango ya maendeleo ya Taifa, Mikoa na Wilaya.
30.
Mheshimiwa
Spika, kuna ugumu wa kupata mitaji ya uhakika kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ili kuendesha biashara za
utalii. Ugumu huo unatokana na riba kubwa zinazotozwa na Benki za Biashara. Ili
kukabiliana na changamoto hii, Wizara itaendelea kushawishi taasisi za fedha
kuona fursa ya kufanya biashara na wafanyabiashara wadogo na wa kati katika
biashara za utalii. Aidha, ipo changamoto ya miundombinu ya kuwezesha malipo
kwa kutumia credit card ambayo
watalii wengi huitumia kulipia huduma mbalimbali.
31.
Mheshimiwa
Spika, changamoto nyingine ni kutokuwa na ardhi iliyotengwa kwa ajili ya kuendeleza
utalii nchini. Wizara itaendelea kuzishawishi Mamlaka za Ardhi na Mipango Miji
katika Halmashauri zetu kutenga maeneo maalum kwa ajili ya uwekezaji wa
shughuli za utalii na kuhamasisha wananchi wanaomiliki ardhi kuingia ubia na
wawekezaji wa utalii ili kutumia ardhi yao katika maendeleo ya sekta ya utalii.
32.
Mheshimiwa
Spika, upo uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi na utaalamu katika sekta ya utalii na
hoteli. Ili kukabiliana na changamoto hii, Wizara imeanzisha Wakala wa Chuo cha
Utalii cha Taifa na kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha vyuo vyake. Aidha,
itawaendeleza watumishi kitaaluma kwa kuwapa mafunzo stahili ili kuboresha
utendaji kazi na kuongeza tija. Vilevile, Wizara itaendelea kujenga ushirikiano
wa karibu baina ya Sekta ya Utalii na sekta nyingine za uchumi na uzalishaji
kama vile kilimo, wazalishaji wa vyakula na vinywaji, vifaa vya ujenzi na
samani na miundombinu ili kuboresha huduma za utalii.
14
33.
Mheshimiwa
Spika, ili kuongeza ajira na mapato ya utalii, sekta nyingine wanashauriwa kutoa huduma na
bidhaa zenye viwango kwa uwingi na kwa wakati unaohitajika katika soko la
utalii. Aidha, wawekezaji katika sekta ya utalii waendelee kutumia bidhaa
zinazozalishwa hapa nchini katika uwekezaji na utoaji huduma kwa wageni. Wizara
itaendelea kuunga mkono jitihada za kujenga mazingira ya ustawi wa viwanda kwa
ajili ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa wingi na ubora unaohitajika katika
sekta ya utalii.
e. Sekta
ndogo ya Malikale
34.
Mheshimiwa
Spika, Malikale ni rasilimali za Urithi wa Utamaduni zinazoshikika na zisizoshikika;
zinazohamishika, na zisizohamishika, zilizo nchi kavu na ndani ya maji ambazo
zimetengenezwa, kuundwa au kuhusika na maisha ya binadamu. Majukumu ya Sekta
ndogo ya Malikale yanasimamiwa na kutekelezwa na Idara ya Mambo ya Kale pamoja
na Shirika la Makumbusho ya Taifa. Nchi yetu imebarikiwa kuwa na hazina kubwa
ya urithi wa malikale. Uhifadhi wa malikale unatekelezwa kwa kuzingatia Sera ya
Utamaduni ya mwaka 1997; Sera ya Malikale ya mwaka 2008; Sheria ya Mambo ya
Kale, Sura ya 333 ya mwaka 2002 na Sheria ya Makumbusho ya No.7 ya mwaka 1980.
Wizara ina jukumu la kutafiti, kutambua, kukusanya, kuonyesha, kuhifadhi,
kulinda na kutangaza Kumbukumbu na Urithi wa Taifa wa Kitamaduni. Kazi hizo
zinafanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
Malikale ikitumika vizuri inaweza kuleta mapato kwa sekta binafsi, sekta ya
umma na Taifa kwa ujumla.
35.
Mheshimiwa
Spika, Maeneo ya malikale nchini ni zaidi ya 500 na kati ya hayo maeneo 130 yametangazwa
katika Gazeti la Serikali kuwa Kumbukumbu ya Urithi wa Taifa letu ambapo 14
yanasimamiwa na Wizara. Maeneo yaliyobaki yanasimamiwa na wamiliki binafsi,
Taasisi na Mashirika Katika kipindi cha mwaka 2012/2013 hadi 2014/2015 wageni
waliotembelea katika maeneo ya Mambo ya Kale ni 679,116.
15
36.
Mheshimiwa
Spika, upo uharibifu wa maeneo yenye malikale na majengo ya kihistoria pamoja na
uvamizi wa maeneo hayo. Aidha, changamoto katika uhifadhi wa malikale ni
gharama za kutunza malikale kwa kuzingatia kasi ya maendeleo ya kiuchumi na
kijamii. Hali hii imechangiwa na uelewa mdogo wa jamii kuhusu thamani, umuhimu
na fursa zilizopo katika urithi wa utamaduni hivyo kutohamasika kuhifadhi na
kuendeleza rasilimalikale.
37.
Mheshimiwa
Spika, Wizara itaendelea kushirikiana na Serikali za Mitaa, Serikali za Vijiji na jamii kwa
ujumla katika uhifadhi wa malikale. Aidha, itaimarisha ushirikiano baina yake
na Taasisi za Serikali na binafsi katika usimamizi wa Sheria na kanuni ili
kuhifadhi na kuendeleza malikale. Wizara imeandaa rasimu ya Mwongozo wa
uwekezaji unaobainisha maeneo ambayo wadau mbalimbali wanaweza kuwekeza katika
shughuli za uhifadhi na ukuzaji utalii. Vilevile, Wizara itaendeleza mikutano
na wadau ili kushawishi uhifadhi wa majengo mijini.
III.
UTEKELEZAJI
WA MAJUKUMU KWA MWAKA 2015/2016 NA MALENGO YA MWAKA 2016/2017
38.
Mheshimiwa
Spika, katika utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka 2015/2016, Wizara ilizingatia
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini
Tanzania (MKUKUTA II); Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/2012
hadi 2015/2016); Mpango Mkakati wa Wizara (2013 – 2016); Mikataba ya Kimataifa
ambayo Tanzania imeridhia na Maelekezo mengine ya Kitaifa. Aidha, Wizara
imeendelea kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni mbalimbali
zinazohusu uhifadhi wa maliasili na malikale na uendelezaji utalii.
16
39. Mheshimiwa Spika Mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 umezingatia: Sera na
Mikakati ya Serikali; Malengo na kazi zilizoainishwa katika Mpango Mkakati wa
Wizara (2016-2021); Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015 – 2020; na
masuala yaliyojitokeza katika Hotuba ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wakati wa kuzindua Bunge la 11 mwezi Novemba, 2015.
40.
Mheshimiwa
Spika, utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2015/2016 hadi Aprili 2016, na Mpango
wa mwaka 2016/2017 katika Wizara yangu umeainishwa kama ifuatavyo:-
a. Sekta
Ndogo ya Wanyamapori
i.
Sheria na Kanuni
41.
Mheshimiwa
Spika, katika kutekeleza Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 (Sura 283), Kanuni za Jumuiya za
Hifadhi ya Wanyamapori (Wildlife Management Areas - WMAs) zimepitiwa. Aidha,
Rasimu za Kanuni za Uchimbaji Madini katika maeneo yaliyohifadhiwa, Kanuni za
Usajili wa Nyara, Kanuni za Shoroba, Kingo na Mapito ya Wanyamapori zimeandaliwa.
42.
Mheshimiwa
Spika, katika 2016/2017 Wizara itaendelea kupitia na kuandaa Kanuni nne za: Jeshi Usu
(Paramilitary); Usimamizi wa Mapori Tengefu; Shoroba; Kingo na Mapito ya
Wanyamapori. Aidha, Wizara itaendelea kukusanya nyara za Serikali zilizopo
kwenye vituo vya Polisi, Halmashauri za Wilaya, Hifadhi za Taifa na Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na kuhakiki nyara zilizohifadhiwa.
ii.
Uhifadhi na Usimamizi wa
Wanyamapori
17
43.
Mheshimiwa
Spika, katika kudhibiti ujangili wa wanyamapori, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa
uhifadhi ilibaini kuwa ujangili unafanyika katika ngazi (levels) tano. Ngazi
hizo ni: (i) baadhi ya wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayopakana na hifadhi
na watumishi wasio waaminifu; (ii) wawindaji haramu wanaojishusisha moja kwa
moja na kuua wanyama; (iii) wasafirishaji na madalali; (iv) wawezeshaji kwenye
ngazi ya nchi wanaonunua nyara, kusambaza vitendea kazi (silaha) ambao ni
kiungo kati ya majangili nguli na watakatishaji fedha na wahalifu walioainishwa
katika ngazi tatu za awali;na (v) ni majangili nguli wa kimataifa. Kutokana na
hali hiyo, Wizara iliimarisha Kitengo chake cha Intelijensia na kufanya doria
kwa kuzingatia mfumo wa makundi hayo.
44.
Mheshimiwa
Spika, doria zilifanyika ndani na nje ya Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu ambapo
siku-doria 109,474 zilifanyika katika mwaka 2015/2016. Doria hizi ziliwezesha
kukamatwa kwa watuhumiwa 1,176 na kesi 654 zilifunguliwa. Kesi 161 zilimalizika
kwa wahalifu 53 kuhukumiwa kifungo cha jumla ya miezi 6,360 na shilingi
363,904,800 kulipwa kama faini. Kati ya wahalifu waliohukumiwa, nane ni
majangili nguli wenye mitandao ya kimataifa. Katika doria zilizofanyika, nyara
mbalimbali za Serikali zilikamatwa. Nyara hizo ni pamoja na wanyamapori hai
(mijusi 315, kobe 202, tumbili 81 na nyani mmoja) vipande 253 vya meno ghafi ya
tembo vyenye uzito wa kilo 634 na vipande 34 vya meno ya tembo yaliyochakatwa
vyenye uzito wa kilo 2. Vilevile, kilo 10,096 za nyamapori wa aina mbalimbali
na ngozi 39 za wanyamapori zilikamatwa. Aidha, bunduki 85 na risasi 1,235 za
aina tofauti zilikamatwa.
iii.
Ushirikishwaji jamii katika
Uhifadhi wa Wanyamapori
45.
Mheshimiwa
Spika, Wizara imeendelea kuhamasisha wananchi kutenga maeneo ya Jumuiya za Hifadhi
ya Wanyamapori (WMAs). Jumuiya za Waga iliyopo Iringa Vijijini na Mufindi,
UMEMARUWA (Uhifadhi na Matumizi
18
Endelevu
ya Maliasili katika tarafa za Rujewa na Wanging’ombe) zimekamilisha vigezo na
kutangazwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali. Aidha, Wizara ipo katika hatua ya
mwisho ya kulitangaza eneo la JUHIWANGUMWA kwenye gazeti la Serikali kuwa
Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii iliyoidhinishwa. Jumuiya ya Hifadhi Wanyamapori
ILUMA (Ifakara, Lupilo na Mang’ula) - Kilombero na Ulanga imekamilisha Mpango
wa Usimamizi wa Rasilimali na kupatiwa haki ya Matumizi ya Rasilimali ya Wanyamapori.
46.
Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka 2016/2017, wananchi wanaoishi katika maeneo yanayopakana na Hifadhi
za Wanyamapori wataendelea kuhamasishwa kushiriki katika uanzishaji na
usimamizi wa maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs). Hatua za uanzishaji
wa WMAs za Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Ngorongo, Utete na Mwaseni
(JUHIWANGUMWA – Rufiji); Ziwa Natron Kaskazini - Longido; Mpimbwe - Mlele;
Matumizi Bora ya Maliasili Miguruwe, Njinjo na Kandawale (MBOMAMINJIKA -
Kilwa); na Igombe - Sagara Wildlife Management Area (ISAMIWA-Urambo)
zitakamilishwa. Wizara kwa kushirikiana na wananchi itaanzisha Mapori ya Akiba
ya Litumbandyosi–Mbinga; Geza-Mazoa – Songea; Kipindimbi – Nachingwea; Mavuji –
Kilwa; na Hifadhi ya Ardhioevu ya Mto Makangage.
iv.
Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori (TAWA)
47.
Mheshimiwa
Spika, katika kuimarisha usimamizi na ulinzi wa Wanyamapori, Serikali imeanzisha
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA). Mamlaka hii na Bodi yake
ilizinduliwa rasmi na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Awamu ya Nne wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 16 Oktoba 2015. Vilevile, Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ameteuliwa pamoja watendaji wengine. Hivi karibuni TAWA
itahamia makao yake makuu ya muda mjini Morogoro.
19
48.
Mheshimiwa
Spika, Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Ofisi ya Msajili wa Hazina
imekamilisha taratibu zote za kuwezesha Mamlaka hiyo kuanza kufanya kazi.
Napenda kulitaarifu Bunge lako tukufu kuwa, kuanzia tarehe 1 Julai, 2016,
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori itaanza kutekeleza majukumu yake rasmi.
Majukumu yote ya Usimamizi wa rasilimali ya Wanyamapori katika Mapori ya Akiba,
Mapori Tengefu na Maeneo ya Wazi yenye wanyamapori nje ya Hifadhi za Taifa na
Eneo la Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro yatasimamiwa na Mamlaka hiyo.
49.
Mheshimiwa
Spika, pamoja na kuanzishwa kwa TAWA, Idara ya Wanyamapori itaendelea kuratibu na
kurekebu Sera, Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta ndogo ya Wanyamapori.
Vilevile, Idara itaendeleza juhudi za kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika
uhifadhi wanyamapori, kuanzisha na kusimamia Jeshi Usu (Paramilitary) pamoja na kuunganisha juhudi za taasisi za utafiti na
mafunzo.
v.
Ulinzi wa Maisha na Mali za
Wananchi dhidi ya Wanyamapori
50.
Mheshimiwa
Spika, tatizo la wanyamapori wakali na waharibifu limeendelea kuwa changamoto ambapo
katika kipindi cha Julai, 2015 hadi Machi, 2016 watu 13 waliuawa na 17
kujeruhiwa. Aidha, mbuzi 39 wameuawa na wanyamapori wakali na mazao katika
mashamba yenye ukubwa wa hekta
712.31 yaliharibiwa.
Katika kukabiliana na tatizo hilo, Wizara imeendelea kufanya doria za kudhibiti
wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneo mbalimbali hususan kwenye wilaya
29 zenye matatizo sugu. Jumla ya Shilingi 10,000,000 zililipwa kama kifuta
machozi na shilingi 182,875,600 zililipwa kama kifuta jasho kwa ajili ya mazao
yaliyoharibiwa.
51.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2016/2017, Mamlaka itaendeleza ulinzi wa maisha na mali za wananchi dhidi ya
wanyamapori
20
wakali
na waharibifu. Vilevile, itafanya doria za kukabiliana na wanyamapori hao.
Aidha, utaratibu wa kulipa kifuta machozi na kifuta jasho kwa wananchi
walioathirika na wanyamapori wakali na waharibifu utaendelea.
52.
Mheshimiwa
Spika, Mamlaka itaendelea na utatuzi wa migogoro ya mipaka baina ya wananchi na maeneo
ya hifadhi za wanyamapori. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kufanya doria
ndani na nje ya Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu; kuimarisha intelijensia
katika doria ikiwemo kuwapatia watumishi mafunzo stahiki na vitendea kazi
ambavyo ni pamoja na magari, mahema, sare za watumishi, redio na vifaa vya
mawasiliano vya kisasa, silaha, boti za doria pamoja na vifaa vingine vya
kufanyia doria wakati wa usiku.
vi.
Migogoro
ya Mipaka na shughuli za kibinadamu ndani ya Hifadhi za Wanyamapori
53.
Mheshimiwa
Spika, katika kukabiliana na migogoro ya mara kwa mara baina ya wananchi na maeneo ya
Hifadhi, Wizara imefanikiwa kuainisha na kuhakiki mipaka ya maeneo
yaliyohifadhiwa yenye migogoro kwa mujibu wa Matangazo ya Serikali. Kazi hii
imefanyika kwa kushirikiana na wataalam kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais (TAMISEMI). Maeneo yaliyohusika ni Hifadhi
ya Taifa Mkomazi, Serengeti, Tarangire na Pori la Akiba Mkungunero. Aidha,
Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya za Longido, Sikonge, Kilosa,
Manyoni, Kiteto na Monduli imehakiki mipaka ya vitalu 14 vya uwindaji vyenye
migogoro. Vilevile, Wizara imeendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi na
viongozi wa vijiji vinavyozunguka maeneo yaliyohifadhiwa na umuhimu wa
kuzingatia mipango ya matumizi bora ya ardhi.
54.
Mheshimiwa
Spika, Pamoja na tatizo la mipaka, upo mgogoro mkubwa wa mifugo kuingizwa ndani ya
hifadhi. Uvamizi huu unaofanyika
21
kwenye
Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na Hifadhi za Taifa umekuwa ukiongezeka kwa
kasi na unahusu zaidi uingizaji na ulishaji wa mifugo hususan ng’ombe, mbuzi,
kondoo na punda pamoja na shughuli nyingine za kibinadamu. Maeneo
yaliyoathirika zaidi ni Serengeti, Selous, Katavi, Ruaha, Mkungunero, Uwanda,
Mkomazi, Ibanda, Rumanyika, Rungwa, Muhwesi, Muyowosi, Kigosi, Kizigo,
Ikorongo, Kijereshi na Lukwati. Kuwepo kwa wananchi pamoja na mifugo katika
maeneo hayo ni uvunjaji wa Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 (Sura ya
283). Wizara imekuwa ikishirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya na
Mikoa pamoja na wadau wengine katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo
hili. Aidha, Serikali imeagiza na kuwataka wananchi waliovamia maeneo
yaliyohifadhiwa kuondoka.
vii. Mpango
Mkakati wa kuzuia Ujangili
55.
Mheshimiwa
Spika, Wizara inaendelea kutekeleza Mkakati wa Kupambana na Ujangili na Biashara
haramu ya Nyara za Serikali ambao ulizinduliwa Novemba, 2014. Kazi
zilizotekelezwa ni kuongeza idadi ya watumishi kwa ajili ya kufanya doria
katika maeneo ya hifadhi ambapo jumla ya watumishi 558 (askari wanyamapori 447
na maafisa 111) wameajiriwa na kufanya idadi ya watumishi waliopo kwa sasa kuwa
2,064. Aidha, Wizara imeanzisha kanda nane za doria za ushirikiano katika
mifumo ya ikolojia ya Selous – Niassa – Mikumi; Ruaha – Rungwa; Katavi – Rukwa;
Moyowosi – Kigosi; Tarangire – Manyara – Simanjiro; na Ngorongoro - Serengeti.
56.
Mheshimiwa
Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi iliwezesha upatikanaji wa vitendea kazi na zana kwa ajili
ya doria. Vifaa hivyo ni magari 24, pikipiki 30, GPS 50, mahema 130, vifaa vya
mawasiliano 50, genereta 50, ndege zisizo na rubani (UAV’s) na ndege ndogo
mbili aina ya Husky. Vilevile,
mafunzo ya kujenga uwezo wa kupambana na ujangili yametolewa kwa askari 53.
Pia, chombo cha ushirikiano baina Wizara
22
na
Taasisi mbalimbali (Multi Agency Task Team – MATT) kilizinduliwa tarehe 30
Juni, 2015. Chombo hiki kimetanua wigo wa kupambana na ujangili kwa kuhusisha
vyombo vingine vya dola.
57.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2016/2017, Mamlaka itawekeza katika kuboresha miundombinu ndani ya Mapori ya Akiba na
maeneo mengine yenye vivutio. Hatua hii itawezesha maeneo mengi zaidi kufikika
hivyo kupanua wigo wa utalii wa picha kufuatia changamoto zinazokabili uwindaji
wa kitalii pamoja na usafirishaji wa nyara.
58.
Mheshimiwa
Spika, katika kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi, Mamlaka itafanya ukarabati wa nyumba 10 za watumishi na
kukamilisha ujenzi wa nyumba 12 katika vituo vitano (KDU Tabora-1,
Moyowosi/Kigosi-3, Ugalla-6, Burigi–1 na Ibanda-1). Aidha, Mamlaka itakamilisha
upatikanaji wa eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya TAWA na Kanda zake. Aidha,
Mamlaka itakarabati barabara zenye urefu wa kilometa 175 katika Mapori ya Akiba
ya Mpanga/Kipengele-25, Ugalla-25, Lukwika-25, Lwafi-25, Rungwa-50 na
Ibanda-25. Vilevile, Mamlaka itafyeka mipaka yenye urefu wa kilometa 150 katika
Mapori ya Akiba ya Rungwa-50, Mkungunero -50 na Swagaswaga-50 pamoja na kuweka
alama za kudumu ardhini (beacon) katika Pori la Akiba Swagaswaga.
viii. Shirika
la Hifadhi za Taifa
59.
Mheshimiwa
Spika, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limeendelea na jukumu lake la msingi la usimamizi wa Hifadhi za
Taifa 16, uhifadhi wa wanyamapori na kuendeleza shughuli za utalii. Katika
kudhibiti ujangili, Shirika limeendesha siku za doria 178,301 ambazo
ziliwezesha
23
kukamatwa
kwa watuhumiwa 2,529. Aidha, Shirika limeendelea kushirikiana na Bodi ya Utalii
kutangaza utalii nje na ndani ya nchi kwa kutoa maelezo na fafanuzi za
kisayansi kuhusu vivutio vya utalii ndani ya hifadhi. Ushiriki wao umechangia
kushawishi na hivyo kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi zetu.
Shirika limeanzisha utalii wa kuangalia faru katika Hifadhi ya Taifa Serengeti,
kuendesha baiskeli katika Hifadhi za Kilimanjaro na Arusha, kupanda kilele cha
Mawenzi na kuruka katika Mlima Kilimanjaro (paragliding).
60.
Mheshimiwa
Spika, ninayo furaha kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa, Shirika la Hifadhi za Taifa
katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro lilipata tuzo ya Kimataifa ya kuwa kivutio
bora cha utalii Barani Afrika (African leading Tourist Attraction). Tuzo hiyo
ilitolewa na Taasisi ya “World Travel Award” ya nchini Uingereza. Tuzo hiyo
itawezesha utalii wa Tanzania kutangazwa zaidi kupitia tovuti ya Taasisi hiyo
ambayo inatembelewa na watalii wengi duniani.
61.
Mheshimiwa
Spika, katika kuimarisha miundombinu, Shirika limefanikiwa kujenga jumla nyumba 15 kwa ajili ya watumishi 29
katika hifadhi za Arusha (1), Gombe (1), Katavi (2), Kilimanjaro (2), Kitulo
(2), Mahale (3), Mikumi (2), Rubondo (1) na Saadani (2). Ujenzi wa nyumba 10
kati ya 15 umekamilika. Vilevile, Shirika limekamilisha ujenzi wa ofisi ya
Lango la Rongai katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, jengo la mapokezi
katika uwanja wa ndege Seronera katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.
62.
Mheshimiwa
Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Shirika limeboresha mfumo wa malipo wa
ki-elektroniki kwa ajili ya wageni kulipa tozo mbalimbali wakati wa kuingia
kwenye Hifadhi za Taifa na unatumika katika hifadhi zote. Mfumo huu
umerahisisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuziba mianya ya upotevu wa
mapato na kuwarahisishia watalii kulipia huduma mbalimbali katika hifadhi.
Aidha, Shirika limeimarisha miundombinu ndani ya Hifadhi za Taifa ili kuwezesha
doria na utalii kufanyika
24
kwa
ufanisi. Katika kutimiza azma hiyo, barabara zenye urefu wa kilometa 3,500 na
viwanja vitano vya ndege vimekarabatiwa. Pia, Shirika limefunga mfumo wa kisasa
wa mawasiliano ya kidigitali katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.
63.
Mheshimiwa
Spika, katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya jamii na uwekezaji kwenye vijiji
vinavyopakana na Hifadhi, Shirika lilitumia Sh. 1,103,714,719.00. Miradi
iliyotekelezwa ambayo inahusu elimu, afya na maji ni ujenzi wa maktaba (2),
maabara (5), madarasa (12), ofisi (9), mabweni (2), nyumba za walimu (3) na
ununuzi wa madawati 425. Aidha, ujenzi nyumba tatu za wauguzi na zahanati mbili
umefanyika. Vilevile, huduma za maji zilihusu kuchimba malambo mawili, mashine
ya kusukuma maji kwa kutumia upepo (windmill) na kisima kirefu. Vikundi 20 vya
wavuvi vilipewa taa za sola 200 na mifumo ya kuchajia 40.
64.
Mheshimiwa
Spika, mwaka 2016/2017, Shirika litaendelea kudhibiti maambukizi ya magonjwa kati ya wanyama na mifugo pamoja
na magonjwa kati ya binadamu na wanyamapori. Aidha, Shirika litakamilisha
taratibu za kuunganisha eneo la Ghuba ya Speke kwenye Hifadhi ya Serengeti.
Vilevile, Shirika litajenga kituo cha kutoa habari kwa wageni, nyumba 44 za
watumishi na barabara mpya zenye urefu wa kilometa 75. Shirika litaimarisha
miundo mbinu ya barabara zenye urefu wa kilometa 5,845 na viwanja vya ndege 17
katika hifadhi za Taifa. Pia, njia za miguu zenye urefu wa kilometa 534
zitaimarishwa kwenye Hifadhi za Taifa za Arusha, Udzungwa na Kilimanjaro.
65.
Mheshimiwa
Spika, Shirika litaendesha siku za doria 196,421 katika Hifadhi za Taifa; kuimarisha
shughuli za utendaji kazi za intelijensia kwa kutoa mafunzo na vitendea kazi
kwa wahifadhi pamoja na kuimarisha uhusiano na wadau wengine wa uhifadhi na
ulinzi wa wanyamapori. Vilevile, Shirika litaendelea kutangaza utalii ndani na
nje ya nchi kwa kushiriki kwenye
25
maonesho
ya kitaifa na kimataifa; kuendelea kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii; na
kutangaza utalii mpya wa “Canopy walk” katika Hifadhi ya Manyara; utalii wa
Faru katika Hifadhi ya Serengeti; na utalii wa “paragliding” katika Hifadhi ya
Kilimanjaro. Vilevile, Shirika litaendelea kutangaza utalii wa kuendesha
baiskeli katika hifadhi za Kilimanjaro na Arusha; utalii wa kupanda kilele cha
Mawenzi na kufungua Kambi kwa utalii maalumu ndani ya kreta ya Kibo katika
Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
66.
Mheshimiwa
Spika, katika kuimarisha mfumo wa udhibiti mapato na matumizi, Shirika litanunua “software” ya ukaguzi na
kutoa mafunzo ya jinsi ya kuitumia. Aidha, Shirika litakamilisha mapendekezo ya
tozo kulingana na msimu wa utalii (low and high season) na yale ya kuwa na tozo
moja (package fees) kwa shughuli za utalii.
67.
Mheshimiwa
Spika, katika kujenga uwezo wa watumishi, Shirika litagharimia watumishi 14 kupata
mafunzo ya muda mrefu na 40 muda mfupi. Aidha, Shirika litaajiri watumishi
wapya 122 kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali. Katika
kuwezesha Shirika kuingia kwenye mfumo wa mawasiliano ya kisasa, Shirika
litaendelea kuboresha mfumo wa ki-eletroniki wa utoaji vibali (electronic
permitting system) katika Hifadhi za Taifa ambao utawezesha miamala ya fedha
kufanyika kwa njia ya mtandao (Electronic Banking). Vilevile, mfumo huu
utawezesha wageni kufanya mawasiliano ya karibu baina ya wadau na menejimenti.
Aidha, Shirika litaendelea kuimarisha mifumo ya taarifa za kijiografia katika
vituo vyote kwa lengo la kurahisha ukusanyaji, utunzaji, uchambuzi na
upatikanaji wa taarifa mbalimbali za kiikolojia.
68.
Mheshimiwa
Spika, Shirika litaendelea kutoa elimu ya uhifadhi na kupunguza migogoro baina ya
wanyamapori na binadamu kwenye maeneo yanayopakana na Hifadhi za Taifa. Katika
kuboresha mahusiano kati ya
26
Hifadhi
na wananchi wanaozunguka Hifadhi, Shirika litaendelea kuwezesha vikundi 30 vya
Benki ya vikundi vya jamii vya uhifadhi (Community Conservation Bank-COCOBA)
katika maeneo yanayozunguka Hifadhi za Taifa za Rubondo, Tarangire na Udzungwa.
Shirika litalipia vipindi 36 vya redio na 36 vya televisheni kuhusu uhifadhi na
utalii pamoja na kuandaa na kusambaza nakala 2,000 za jarida la Shirika “TANAPA
Today” linalochapishwa kila robo mwaka.
ix.
Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro
69.
Mheshimiwa
Spika, katika kuimarisha miundombinu, Mamlaka imekarabati kilometa 326 za barabara ndani ya hifadhi na nyumba
mbili za askari. Aidha, ilinunua magari saba ya doria na kutangaza zabuni za
ujenzi wa ofisi kwa ajili ya uwanja wa ndege wa Ndutu ndani ya Hifadhi hiyo.
Katika kuimarisha huduma za jamii ya wafugaji, Mamlaka imetekeleza mradi wa
kuboresha mifugo na kukamilisha mradi wa kijiji cha Jema walikohamishiwa
wafugaji waliotolewa ndani ya hifadhi na kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya
ya Ngorongoro. Aidha, Mamlaka imenunua magunia 22,000 na kupokea magunia 20,000
ya mahindi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo yalisambazwa kwa jamii inayoishi
ndani ya Hifadhi.
70.
Mheshimiwa
Spika, katika jitihada za kukabiliana na tatizo la ujangili na kuongeza ufanisi katika
ulinzi wa Wanyamapori, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuimarisha
shughuli za uhifadhi kwa kuendesha siku-doria 39,600 ndani ya eneo na katika
maeneo yanayozunguka hifadhi. Doria hizo ziliwezesha kukamatwa kwa watuhumiwa
33, kati ya hao watuhumiwa 30 walitozwa faini na watatu kesi zao zinaendelea.
71.
Mheshimiwa
Spika, Katika kuepuka utegemezi wa kipato kutokana na shughuli za utalii pekee ambazo huathirika mara nyingi
kutegemea hali ya soko la utalii duniani, Mamlaka inaendelea kujenga Kitega
27
Uchumi
jijini Arusha. Ujenzi wa jengo hilo lenye ghorofa 17, umefikia asilimia 80 na
unatarajiwa kukamilika ifikapo Novemba, 2016.
72. Mheshimiwa Spika, katika
mwaka 2016/2017, Mamlaka itaendelea
na shughuli za uhifadhi wanyamapori na malikale; kuhudumia jamii ya wafugaji na
kuendeleza shughuli za utalii. Katika kutekeleza jukumu hilo, Mamlaka itatoa
chanjo za homa ya mapafu na sotoka kwa ng’ombe 130,000 na mbuzi na kondoo
230,000 walio ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. Katika kuboresha miundombinu,
Mamlaka itajenga bwawa la maji la Olekule, Kata ya Aleilelai, kuchimba kisima
cha maji eneo la Naibarta - Endulen, kukarabati barabara yenye urefu wa
kilometa 72, kuhakiki mpaka wa eneo la hifadhi katika maeneo ya Endamagha,
Lositete, Malambo na Piyaya pamoja na kujenga vituo vitatu vya Askari.
x.
Vyuo vya Taaluma ya Wanyamapori
73.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2015/2016, Chuo cha Usimamizi na Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka (College of African
Wildlife Management Mweka – CAWM) kimedahili wanafunzi 578. Chuo kimenunua
magari mawili kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi. Aidha, Chuo
kimekarabati mabweni, bwalo la chakula, jengo la Utawala na kutengeneza
barabara ndogo za ndani. Vilevile, chuo kimekarabati sehemu ya kuegeshea magari
pamoja na kujenga nyumba moja ya wafanyakazi katika eneo la Kwakuchinja. Aidha,
Kituo cha Elimu kwa Jamii Likuyu-Sekamaganga kilitoa mafunzo ya uhifadhi
shirikishi kwa watumishi 91 kutoka Halmashauri za Wilaya za Kibondo, Kakonko,
Buhingwe, Uvinza, Kasulu na Mkuranga katika Mikoa ya Kigoma na Pwani.
74.
Mheshimiwa
Spika, Taasisi ya Mafunzo ya Wanyamapori Pasiansi imedahili wanafunzi 441, kati ya hao,
90 ni wa kozi ya Astashahada ya Uhifadhi na Ulinzi wa Wanyamapori na 351 ni
Astashahada ya Awali ya
28
Uhifadhi
na Ulinzi wa Wanyamapori; wanawake wakiwa ni 93 na wanaume 348. Aidha, Taasisi
kwa msaada wa wadau imenunua mabasi mawili, malori mawili, gari dogo moja na
kujenga kambi ya mafunzo kwa vitendo katika eneo la Fort Ikoma, Serengeti.
75.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2016/2017, Vyuo vya mafunzo ya taaluma ya wanyamapori vitadahili
jumla ya wanafunzi 1,136. Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori - Mweka kitadahili
wanafunzi 736 na Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi 400. Aidha, Kituo cha
Elimu kwa Jamii – Likuyu Sekamaganga kitaendelea kutoa elimu ya uhifadhi
wanyamapori kwa viongozi na askari wa vijiji.
76.
Mheshimiwa
Spika, Katika kuimarisha miundombinu na vitendea kazi, Chuo cha Usimamizi wa
Wanyamapori, Mweka kitanunua gari kwa ajili ya mafunzo porini; kujenga madarasa
mawili; kujenga nyumba mbili za watumishi na kuweka umeme kwenye eneo la
mafunzo la Kwakuchinja. Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi kitakarabati
nyumba tano za watumishi, bwalo la chakula na mfumo wa maji safi.
xi.
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori
(TAWIRI)
77.
Mheshimiwa
Spika, Taasisi ina jukumu la kusimamia na kufanya utafiti katika maeneo yanayohusu
wanyamapori na ikolojia wanapoishi nchini. Katika kutekeleza majukumu yake,
Taasisi imeendeleza utafiti wa magonjwa ya wanyamapori, magonjwa ya maambukizo
baina ya binadamu, wanyamapori na mifugo. Pia, inatekeleza miradi ya utafiti wa
ikolojia na uwezo wa hifadhi kuhimili idadi mbalimbali za wanyamapori kulingana
na mahitaji yao. Aidha,
29
Taasisi
imeendelea kusimamia miradi mikubwa miwili ambayo ni mradi wa kuboresha ufugaji
nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa na mradi wa uhifadhi wa mbwa mwitu katika
ikolojia ya Serengeti.
78.
Mheshimiwa
Spika, Taasisi imekamilisha utafiti kuhusu ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa (Rift Valley
Fever, RVF) ambao umekuwa ukitokea nchini kila baada ya miaka 10 hadi 15. Lengo
la mradi lilikuwa ni kutambua kirusi kinachosababisha ugonjwa huo, chanzo cha
ugonjwa na chanzo hicho hujificha wapi wakati ambapo hakuna mlipuko. Utafiti
huu umeonesha kuwa kirusi cha ugonjwa wa RVF kinatunzwa kwa kiwango cha chini
kwenye (i) mbu jamii ya Aedes na Culex- asilimia 2.7 (ii) wanyama wafugwao ng’ombe
asilimia 5.7, kondoo 5.7 na mbuzi 1.9 na (iii) wanyamapori wastani wa asilimia
14.6 (nyati, nyumbu, kongoni, swala tomi, swala granti na nyemela). Mifugo na
wanyamapori waliozaliwa mwaka mmoja hadi minne baada ya mlipuko wa mwisho wa
2006/2007 walionekana wameambukizwa na kirusi, ambayo inadhihirisha kuwa
maambukizi mapya huwa yanaendelea wakati ambao hakuna mlipuko wa ugonjwa. Mradi
umehitimisha kuwa chanzo cha mlipuko wa ugonjwa ni pale mazingira yanayowezesha
mbu kuzaliana kwa wingi yanapokuwepo, hasa wakati wa mvua nyingi na mafuriko.
79.
Mheshimiwa
Spika, katika kuboresha ufugaji nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa, Taasisi
imetengeneza na kusambaza mizinga 1,200 kwa wadau mbalimbali ikiwemo Wakala wa
Huduma za Misitu-Kanda ya Kasikazini; Muungano wa Vikundi vya Wakulima Tanzania
(MVIWATA)-Arusha; Umoja Group-Arusha; na Halmashauri ya Wilaya ya
Siha-Kilimanjaro. Matumizi ya mizinga na vifaa vya kisasa yatasaidia kuongeza
na kuboresha uzalishaji wa mazao ya nyuki.
80.
Mheshimiwa
Spika, Taasisi inasimamia mradi wa uhifadhi wa mbwa mwitu katika ikolojia ya
Serengeti ambao wapo katika hatari ya kutoweka duniani. Mradi huo una makundi
27 yenye zaidi ya mbwa mwitu
30
300
ambao mienendo na mitawanyiko yao inafuatiliwa kwa kutumia vifaa vya kisasa vya
mawasiliano ya satelaiti (GPS satellite collars). Ufuatiliaji umeonesha kuwa
mbwa mwitu hao wametawanyika katika ikolojia ya Serengeti inayojumuisha Hifadhi
ya Taifa Serengeti, Hifadhi ya Ngorongoro, Mapori ya Akiba ya Maswa, Ikorongo
Grumeti na maeneo ya wazi ya Ziwa Eyasi, Makao na Pori Tengefu Loliondo.
81.
Mheshimiwa
Spika, katika kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mbwa mwitu
katika maeneo ya mradi, TAWIRI imeendelea kusambaza vipeperushi, kalenda na
fulana zenye ujumbe mahususi unaolenga kuokoa kizazi cha mbwa mwitu ambao ni
miongoni mwa wanyamapori ambao ni kivutio kikubwa cha utalii.
82.
Mheshimiwa
Spika, mwaka 2016/2017, Taasisi itafanya sensa za wanyamapori katika sehemu mbalimbali
ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa. Maeneo hayo ni pamoja na mfumo ikolojia
wa Serengeti. Aidha, Taasisi itafanya sensa ya mamba na viboko nchi nzima.
Vilevile, itaendeleza utafiti wa mbwa mwitu katika mfumo-ikolojia wa Serengeti
na kuendelea kuhamasisha jamii kuwalinda na kuwahifadhi wanyama hao wasitoweke.
83.
Mheshimiwa
Spika, Taasisi itaendeleza tafiti za mwenendo wa magonjwa ya wanyamapori hasa homa ya
bonde la ufa, kaswende ya nyani, ugonjwa wa miguu na midomo, homa ya vipindi na
magonjwa yanayoambukiza binadamu na wanyamapori kutokana na kula nyamapori.
Aidha, Taasisi itaendelea na majaribio ya matumizi ya ndege zisizo na rubani
katika kuzuia tembo waharibifu wa mazao katika mifumo ikolojia ya Tarangire-Manyara
na Serengeti ili kupunguza mgongano kati ya tembo na Binadamu. Vilevile,
utafiti utafanyika kuhusu mfumo ikolojia wa Serengeti unavyofanya kazi na
manufaa yake kwa jamii.
31
84.
Mheshimiwa
Spika, Taasisi itaendelea kufanya utafiti kuhusu mahusiano kati ya nyuki na mimea
katika kanda zote za Tanzania Bara. Utafiti huo unatarajiwa kuwezesha uchoraji
wa ramani kulingana na aina za mimea, nyuki, asali na chavua katika maeneo
husika. Aidha, utafiti wa wadudu na vimelea wanaoshambulia nyuki katika mikoa
11 ya Tanzania Bara utafanyika.
85.
Mheshimiwa
Spika, Taasisi itaendelea kuwajengea uwezo watafiti na watumishi wengine wa Taasisi kwa
kuwaendeleza kimasomo katika ngazi mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kitaaluma
na kuleta tija katika Taasisi. Aidha, itatengeneza na kusambaza mizinga 1,500
kwa wadau wa sekta ya ufugaji nyuki. Vilevile, Taasisi itakamilisha ujenzi wa
jengo la maabara ya kisasa ya utafiti wa nyuki pamoja na mazao yake.
xii. Mfuko
wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania
86.
Mheshimiwa
Spika, Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania (Tanzania Wildlife Protection Fund,
TWPF) ulianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 21 ya mwaka 1978 baada ya kukifanyia
marekebisho kifungu cha 69 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 12 ya mwaka
1974. Marekebisho hayo yalitangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 21 la tarehe
22 Mei, 1981. Mfuko ulianzishwa kwa lengo la kuwezesha mapambano dhidi
ujangili, kugharimia tafiti za wanyamapori, kusaidia maendeleo ya wananchi
wanaopakana na hifadhi za wanyamapori na kutoa elimu ya uhifadhi kwa umma
kupitia MALIHAI clubs. Katika mwaka 2015/2016, Mfuko ulikadiria kukusanya
shilingi 16,980,000,000 Hadi kufikia Aprili 2016 shilingi 13,471,369,031.25
zilikusanywa sawa na asilimia 79.34 ya lengo. Fedha hizo zimetumika kugharamia
kazi za uhifadhi wa Wanyamapori, utafiti na mafunzo, ujenzi na ukarabati wa
miundombinu ndani ya Mapori ya Akiba na Uendeshaji wa Vyuo na Taasisi za
Wanyamapori. Aidha, Mfuko umegharamia miradi mitano ya jamii katika Wilaya za
Wanging’ombe, Kondoa, Ilembula na Singida. Miradi hiyo ni Uchimbaji wa Kisima
katika kijiji cha Mayale, kuchangia ujenzi wa ofisi
32
ya
kata ya Wanging’ombe, Zahanati katika kata ya Kwadelo na Kituo cha Afya katika
kijiji cha Pohamba. Vilevile, Mfuko umegharamia ununuzi wa vitanda 91 vya bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari ya Ilembula.
b. Sekta
Ndogo ya Misitu na Nyuki
87.
Mheshimiwa
Spika, Idara ya Misitu na Nyuki imekasimisha baadhi ya shughuli zake kwa Wakala wa Huduma za Misitu. Kwa sasa
Idara inashughulika na: kuendeleza, kufuatilia, kutathmini na kufanya marejeo
ya Sera, Sheria na Mikakati ya Misitu na Nyuki; kufuatilia maendeleo ya taasisi
za mafunzo ya misitu na ufugaji nyuki zilizo chini ya Wizara; na kuwezesha
msaada wa kitaalamu na kufuatilia utekelezaji wa shughuli za misitu na ufugaji
nyuki katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs). Kazi nyingine ni kuratibu
uanzishaji wa hifadhi za misitu na nyuki; kuwezesha Mamlaka za Serikali za
Mitaa kutoa huduma za ugani; na kuainisha maeneo na kuwezesha utafiti wa misitu
na nyuki.
i.
Sera na Sheria
88.
Mheshimiwa
Spika, katika kuimarisha uhifadhi wa misitu na kuendeleza ufugaji nyuki nchini,
Wizara yangu imeendelea kuboresha Sera za Misitu na Nyuki za mwaka 1998.
Maboresho hayo yanazingatia mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na
kimazingira yanayotokea ndani na nje ya nchi. Aidha, Wizara imeandaa rasimu ya
Programu mpya ya Misitu na Nyuki ya kipindi cha 2016-2021.
89.
Mheshimiwa
Spika, Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998, pamoja na mambo mengine, imesisitiza ushiriki wa wananchi katika
upandaji na usimamizi wa misitu ili kuongeza upatikanaji wa mazao ya misitu.
Ili kufanikisha suala hili, Wizara imeanzisha Programu ya Panda Miti Kibiashara
katika Mikoa ya Njombe, Iringa, Ruvuma na Morogoro. Mikoa hii imechaguliwa
33
kwa
sababu ya kuwa na maeneo ya kutosha kuwezesha kilimo cha miti; hali nzuri ya
hewa kwa ajili ya kilimo cha miti; utayari wa wananchi na ushiriki wao katika
shughuli za upandaji miti kibiashara. Mpaka sasa vikundi 50 vyenye wanachama
2,351 vimeundwa. Programu hii imewezesha wananchi kupanda zaidi ya hekta 3,000
zenye miche bora ya miti.
90. Mheshimiwa Spika, katika
mwaka 2016/2017, Wizara itakamilisha
na kusambaza kwa wadau nakala 5,000 za Sera Mpya ya Misitu na mkakati wake wa
utekelezaji. Vilevile, itakamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki.
Aidha, Wizara itawasilisha Bungeni muswada wa marekebisho ya Sheria ya Misitu
Namba 14 ya mwaka 2002 ili kukidhi mahitaji ya uendelezaji wa sekta ndogo ya
Misitu na Ufugaji Nyuki.
ii.
Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania
91.
Mheshimiwa
Spika, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Services Agency - TFS) ulianzishwa kwa mujibu wa
Sheria na kutangazwa katika Tangazo la Serikali Na. 269 la tarehe 30 Julai,
2010. Kiutendaji, Wakala unatekeleza majukumu yaliyokuwa ya Idara ya Misitu na
Nyuki isipokuwa utungaji wa sera, sheria na programu za misitu na nyuki.
92.
Mheshimiwa
Spika, Wakala unasimamia misitu ya hifadhi ya asili (Forest Reserves) 506 yenye hekta
15.48 milioni iliyotawanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Wakala pia unasimamia
misitu iliyotengwa kama Hifadhi za Mazingira Asilia (Forest Nature Reserves) 11
zenye jumla ya hekta 233,837. Hifadhi hizo zipo katika mikoa ya: Tanga (Amani,
Nilo na Magamba); Morogoro - (Uluguru na Mkingu); Morogoro na Iringa
(Kilombero); Mbeya (Mlima Rungwe); Kilimanjaro (Chome); Iringa (Udzungwa
Scarp); Kagera (Minziro) na Lindi (Rondo Plateau). Vilevile, Wakala unasimamia
Misitu ya Hifadhi Lindimaji (catchment forests) yenye jumla ya hekta milioni
1.4. Aidha,
34
katika
ukanda wa pwani kuna jumla ya hekta 115,000 za misitu ya mikoko iliyopo katika
mikoa ya Tanga, Pwani, Dar-es-Salaam, Lindi na Mtwara. Vilevile, Wakala
unasimamia mashamba 18 ya miti ya kupandwa yaliyoko katika mikoa 12 nchini.
Usimamizi
wa Rasilimali za Misitu
93.
Mheshimiwa
Spika, katika kudhibiti uvunaji haramu na biashara ya mazao ya misitu, jumla ya doria
siku 22,693 ziliendeshwa katika maeneo ya hifadhi za misitu, ardhi huria,
hifadhi za nyuki, maeneo ya uvunaji, usafirishaji na masoko. Kupitia doria
hizo, vipande 110,307 vya mbao, mkaa magunia 105,324 silipa 5,399 na shata za
milango 391 vilikamatwa na kuuzwa. Aidha, watuhumiwa 281 walikamatwa na kesi 22
zilifunguliwa mahakamani na zipo katika hatua mbalimbali; kambi za mkaa 29 na
matanuru 858 ya kutengeneza mkaa yaliharibiwa. Wafugaji wenye ng’ombe 3,997
walitozwa faini ambapo kiasi shilingi 1,357,115,380 zilikusanywa kutokana na
faini na mauzo ya mazao yaliyokamatwa. Aidha, Wakala iliendesha kesi za jinai
34 zilizopo mahakamani kutokana na makosa ya uvunjaji wa sheria ya Misitu. Kesi
tano zimeisha na watuhumiwa saba wamehukumiwa kifungo cha miaka saba jela.
94.
Mheshimiwa
Spika, Ukaguzi katika vizuia 72 vya Kanda saba za Wakala ulifanyika ili kubaini kama
sheria na taratibu za kusafirisha mazao ya misitu zinazingatiwa. Jumla ya
magari 5,234 yalikaguliwa katika vizuia vilivyopo Kanda ya Kati, Ziwa na
Magharibi. Magari 361 yalikiuka sheria na kanuni za kusafirisha mazao ya
misitu. Mazao yaliyotaifishwa kwenye vizuia vya Kanda ya Ziwa na Kati ni pamoja
na magunia 7,517 ya mkaa, vipande 236 vya mbao, nguzo 53, vitanda tisa, milango
tisa na kuni mita za ujazo 44.8. Aidha, vizuia sita vipya vilianzishwa katika
Kanda ya Kati na Nyanda za juu
35
95.
Mheshimiwa
Spika, Watumishi 288 wa Wakala kutoka katika kanda tatu za kaskazini, Kusini na Nyanda za juu kusini wamepatiwa
mafunzo ya kuendesha kesi, kuielewa sheria na kanuni za Misitu na ufugaji
nyuki. Vilevile, Wakala ilitoa mafunzo kuhusu taratibu za kufanya biashara ya
mazao ya misitu kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu kwa wafanya biashara
1,125 kutoka katika Kanda za Kati, Mashariki na Ziwa.
96.
Mheshimiwa
Spika, Wakala umeandaa mipango ya uvunaji katika Wilaya tano za Kilosa, Kibaha, Ulanga,
Kisarawe na Kilombero. Aidha, Kamati za Uvunaji katika Wilaya 16 ziliwezeshwa
kufanya mikutano ya kupitisha maombi ya wavunaji na kudhibiti uvunaji haramu wa
mazao ya misitu. Pia, Wakala umeandaa rasimu ya mipango ya usimamizi katika
misitu ya Korogwe na Vugiri (Tanga), North Ruvu (Pwani) na Essmingor (Arusha)
na kufanya mapitio ya mipango ya misitu ya Kindoroko (Kilimanjaro) na Rondo
(Lindi).
97.
Mheshimiwa
Spika, Wakala umeendelea kutekeleza Mpango Mkakati wa Misitu 2014-2019. Moja ya mikakati iliyomo kwenye
mpango huo ni kupanda jumla hekta 185,000 za miti kwa mwaka kwa kushirikiana na
Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na wadau wengine. Lengo ni kuongeza
uzalishaji wa miti ili kuziba pengo la mita za ujazo 19.5 milioni kwa mwaka za
timbao hadi kufikia mwaka 2030.
98.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2016/2017, Wakala utaendesha siku za doria 33,264 katika maeneo ya hifadhi za
misitu, maeneo ya uvunaji, usafirishaji na kudhibiti biashara ya mazao ya
misitu katika kanda saba. Aidha, Wakala utawezesha Kamati za Uvunaji za Wilaya
46 kufanya
36
mikutano
ya kupitisha maombi ya uvunaji. Aidha, Wakala utaandaa mipango ya uvunaji mazao
ya misitu katika Wilaya 11 kwenye maeneo ya ardhi huria.
99. Mheshimiwa Spika,
katika kutatua changamoto za uvamizi, misitu
ya hifadhi 20 yenye migogoro itashughulikiwa. Vilevile, Wakala utatekeleza
makubaliano ya pamoja ya kudhibiti biashara haramu ya mazao ya misitu kati ya
nchi jirani za Msumbiji, Zambia na Kenya kwa kufanya vikao na doria za pamoja.
Katika kutatua changamoto za uhifadhi na usimamizi wa hifadhi za misitu, Wakala
utatekeleza makubaliano yaliyoridhiwa kati yake na TAMISEMI na kutoa mafunzo
kwa wafanyabiashara 1,650 wa mazao ya misitu katika Kanda tatu za Kati, Ziwa na
Mashariki.
Kuimarisha
Mipaka na Usimamizi wa Misitu ya Hifadhi
100.
Mheshimiwa
Spika, Wakala umeondoa wananchi waliovamia misitu ya hifadhi 17 kwa ajili ya shughuli za kilimo, ufugaji na
makazi. Hali hiyo imesababisha uharibifu wa uoto wa asili, vyanzo vya maji na
bioanuwai hivyo kusababisha athari za ardhi kuwa jangwa. Hatua hiyo
imechukuliwa kwa kuzingatia Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 Kifungu cha
26 ambacho kinakataza uvamizi wa maeneo ya misitu yaliyohifadhiwa. Aidha,
Wakala umefanya mapitio ya soroveya kilometa 510.14; kusafisha mipaka ya misitu
ya hifadhi 126 yenye urefu wa kilometa 1,927.42; na kuweka maboya 972; mabango
2,075; na mashimo ya mwelekeo 228 ili kutoa tahadhari kwa jamii kuhusu maeneo
yaliyohifadhiwa. Kazi nyingine zilizofanyika ni kukuza miche 4,773,317 na
kupanda kwenye mipaka yenye urefu wa kilomita 40; kurudishia maeneo ya misitu
yenye hekta 259.8 ya misitu ya hifadhi 11 na hekta 34.8 za hifadhi ya misitu ya
mikoko iliyoharibiwa.
101.
Mheshimiwa
Spika, tathmini ya rasilimali za Misitu katika msitu wa Hifadhi Mangaliza – Mpwapwa
inaendelea na itakamilika katika mwaka wa fedha 2016/17. Rejea zilifanyika kwa
kungano (clusters) 213 katika Kanda ya
37
Magharibi
na Nyanda za Juu Kusini kwa lengo la kujua rasilimali za misitu zilizopo ili
kuandaa mipango ya usimamizi. Aidha, Wakala umehakiki, kuhuisha na kuweka
katika mfumo wa kidijitali ramani za misitu ya asili 26 na misitu ya hifadhi za
mazingira asilia mitatu.
102. Mheshimiwa Spika, katika
mwaka 2016/2017, Wakala utaendelea
kusimamia hifadhi za misitu kwa kuondoa wavamizi katika misitu ya hifadhi 27;
kufanya mapitio ya soroveya ya kilomita 227,251 za misitu; kusafisha mipaka ya
misitu ya hifadhi 98 yenye urefu wa kilomita 2,816; kupanda miche kwenye mipaka
ya misitu kilomita 167; kuweka maboya 1,290 na mabango 541 ili kutahadharisha
jamii kuhusu maeneo yaliyohifadhiwa. Vilevile, Wakala utaongoa maeneo
yaliyoharibiwa kwa kuotesha miti ya asili katika eneo lenye ukubwa wa hekta
2,041 na kupanda mikoko kwenye eneo la hekta tisa za hifadhi. Hali kadhalika,
tathmini itafanyika katika misitu ya Ijogo na Mlali; uhakiki na kuhuisha ramani
za misitu ya asili 50 na mashamba 18; na kuchora ramani ya misitu 15 na hifadhi
za nyuki tano.
Uendelezaji
wa vivutio vya Utalii ikolojia
103.
Mheshimiwa
Spika, Wakala uliboresha vivutio vya utalii ikolojia katika misitu ya hifadhi za mazingira
asilia kwa kusafisha barabara zenye urefu wa kilometa 34.5; njia vinjari
kilometa 68.9; na kambi 17 za kupumzikia wageni katika misitu mitano ya Hifadhi
za mazingira asilia za Amani, Nilo, Uluguru, Kilombero na Mkingu. Aidha, ujenzi
wa mageti 11 ya kuingia katika misitu ya hifadhi ya mazingira asilia
umefanyika. Taratibu za kupandisha hadhi msitu wa Hifadhi wa Hanang kuwa
hifadhi ya mazingira asilia zinaendelea.
104.
Mheshimiwa
Spika, Misitu ya Mifadhi za Mazingira Asilia na Misitu ya Hifadhi zimekuwa zikipata
watalii toka ndani na nje ya nchi. Mwaka
38
2015/2016,
watalii 3,800 walitembelea hifadhi za mazingira asilia. Kati ya hao, watalii
2,628 waliotoka nje ya nchi na 1,172 ni watalii wa ndani. Maeneo
yaliyotembelewa katika Misitu ya hifadhi za mazingira asilia ni Mount Rungwe,
Kilombero, Mkingu, Uluguru, Amani, Nilo, Magamba na Chome pamoja na misitu ya
hifadhi ya Duluti na Milima ya Udzungwa.
105.
Mheshimiwa
Spika, mwaka 2016/2017, Wakala kwa kushirikiana na wadau utaboresha na kuendeleza vivutio
vya utalii ikolojia kwa kutunza na kuimarisha miundombinu katika hifadhi za
misitu ya mazingira asilia. Uboreshaji huu utahusisha kutengeneza njia za
kuvinjari zenye urefu wa kilometa 110; vituo vinne vya kuangalia mandhari; na
kambi tano za kumpumzikia wageni katika hifadhi za misitu na misitu ya
mazingira asilia. Misitu itakayohusika ni pamoja na Vikindu, Pugu/Kazimzumbwi,
Kimboza, Mbeya Range, Kalambo, Pindiro, Rondo, Mkingu, Uluguru, Kilombero,
Mlima Hanang, Nilo na Chome.
106.
Mheshimiwa
Spika, Wakala utaendelea kusimamia manzuki 90 zilizopo katika Kanda na mashamba ya miti na kuzalisha asali tani
17 na tani mbili za nta. Ili kuzalisha mazao bora ya nyuki, elimu itatolewa kwa
wadau wa ufugaji nyuki 190 wakiwemo wafugaji nyuki, wafungashaji na wafanyabiashara
kutoka katika Kanda za Kati na Ziwa. Sampuli 70 za asali zitakusanywa kutoka
katika wilaya 25 kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi wa kimaabara ili kujua ubora
wa asali inayozalishwa na kutimiza masharti ya kuuza asali katika masoko ya
nje. Vilevile, Wakala utatoa mafunzo ya kutengeneza mizinga kwa wafugaji nyuki
580 na mafundi 44 kutoka katika Wilaya nane za Geita, Biharamulo, Musoma,
Bukombe, Chato, Mbogwe, Magu na Misenyi. Aidha, Wakala utawezesha Chama cha
Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania (TABEDO) kuendesha shughuli zake.
Uendelezaji
na Usimamizi wa Mashamba ya Miti
39
107.
Mheshimiwa
Spika, Wakala imeotesha miche ya miti 17,899,266, na kupanda kwenye mashamba yenye
ukubwa wa jumla ya hekta 12,277 kwa mwaka 2015/2016. Maeneo yaliyopandwa ni
pamoja na hekta 2,792 mashamba mapya, hekta 4,979 maeneo ya mashamba ya zamani
na hekta 6,060 maeneo ambayo miti haikuota. Vilevile, mashamba yenye ukubwa wa
hekta 28,882 yalipaliliwa, kuondoa matawi ya miti (kupogolea) kwenye eneo la
hekta 7,901 na kupunguza miti katika eneo la hekta 659.7. Wakala umeongeza
hekta 5,000 za Shamba la miti Wino kutoka katika eneo la kijiji cha Mkongotema
na kuandaa Mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji hicho. Wakala pia
umekarabati barabara za msituni zenye urefu wa kilomita 1,324.5 na kujenga
kilomita 100.
108.
Mheshimiwa
Spika, Wakala ulifanya doria katika eneo lenye ukubwa wa hekta 281,350.4 katika
mashamba ya miti, kusafisha kilometa 2,205; kuweka maboya 45 kwenye mipaka
katika Shamba la Miti Ruvu kaskazini na kutunza minara 17 katika Shamba la Miti
Sao Hill. Ukaguzi wa miti yenye mita za ujazo 611,355 ulifanyika katika maeneo
yaliyotengwa kwa ajili ya uvunaji. Kampeni 42 za uhamasishaji wa madhara ya
moto kwenye misitu zilitolewa kwa vijiji 40 vinavyozunguka mashamba manne ya
miti ya Kawetire, Longuza, Ruvu Kaskazini na Ukaguru.
109.
Mheshimiwa
Spika, katika kuhifadhi vyanzo vya maji vilivyoko katika mashamba ya miti, mimea ya
kigeni iling’olewa na kupanda miti ya asili. Kazi hiyo ilifanyika kwenye eneo
la hekta 147 katika Shamba la Miti Sao Hill na hekta 20 Shamba la Miti
Kawetire. Katika mashamba ya West Kilimanjaro na Kawetire Mapitio ya mipaka na
kugawanya viunga yalifanyika kwenye eneo la hekta 11,015. Vilevile, rasimu ya
mipango ya usimamizi ya mashamba mawili ya Ruvu Kaskazini na Korogwe
ilitayarishwa.
40
110. Mheshimiwa Spika, mazingira ya kazi kwa watumishi yameboreshwa ikiwa ni pamoja na
kukarabati nyumba 44 na kuendeleza ujenzi wa nyumba 13 katika mashamba ya Sao
Hill, Rubare, Mtibwa, Wino na Mbizi. Aidha, Wakala umekarabati mifumo 11 ya
usambazaji wa maji safi katika mashamba saba ya miti na ofisi nne katika Kanda
za Mashariki na Ziwa. Ujenzi wa ofisi nne katika Kanda ya Kusini, Nyanda za Juu
Kusini, Shamba la Miti Wino na Mbizi unaendelea.
111.
Mheshimiwa
Spika, Wakala umenunua na kusambaza kwenye vituo vyake vitendea kazi kwa ajili ya kuboresha na kuongeza
ufanisi wa kazi. Vifaa vilivyonunuliwa ni pamoja na magari 20, mahema 65 na GPS
25. Vilevile, Wakala ulipata msaada wa jenereta 25, telescope 15 na mtambo mmoja wa kutengenezea barabara. Aidha,
Wakala uligharimia mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 60 na mfupi kwa
watumishi 125.
112.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2016/2017, Wakala utaotesha miche ya miti 14,470,000, katika
mashamba ya miti 18, kuandaa mashamba ya kupanda miti hekta 7,822 na kupanda
miche ya miti kwenye mashamba mapya yenye ukubwa wa hekta 4,995. Pia utapanda
miche ya miti kwenye hekta 3,393 katika mashamba yaliyovunwa na hekta 2,492
katika maeneo ambayo miti haikuota. Aidha, Wakala utapalilia eneo la shamba lenye
ukubwa wa hekta 32,191, kupunguzia matawi ya miti kwenye eneo lenye ukubwa wa
hekta 8,757 na kupunguza miti kwenye eneo la shamba lenye ukubwa wa hekta
1,706. Kazi nyingine zitakazofanyika ni kusafisha/kukarabati barabara za
msituni zenye urefu wa kilomita 1,434 na kutengeneza zenye urefu wa kilomita
116. Vilevile, nyumba 63 na mifumo ya maji itakarabatiwa na nyingine mpya 13
zitajengwa. Wakala utaongeza mashamba mawili mapya ya miti katika Kanda za
Mashariki na Kusini.
41
113.
Mheshimiwa Spika, Wakala utaotesha miche ya miti 14,470,000; kutayarisha hekta 8,388 na kupanda
hekta 4,995 katika maeneo mapya, hekta 3,393 katika maeneo yaliyovunwa na hekta
2,492 katika maeneo ambayo miti haikuota. Aidha, Wakala utapalilia eneo la
shamba lenye ukubwa wa hekta 32,191; kupogoa hekta 8,757; na kupunguza miti
katika hekta 1,706. Kazi nyingine zitakazofanyika ni kusafisha na kukarabati
barabara zenye urefu wa kilometa 1,434 kwenye mashamba na kutengeneza nyingine
zenye urefu wa kilometa 116. Vilevile, nyumba 13 za watumishi zitajengwa pamoja
na kukarabati nyumba 63 na mifumo ya maji. Wakala utaongeza mashamba mawili
mapya ya miti katika Kanda za Mashariki na Kusini.
114. Mheshimiwa Spika,
katika mwaka 2016/2017, Wakala utasimamia
uvunaji wa miti yenye mita za ujazo 754,931, kuni zenye mita za ujazo 24,462 na
nguzo zenye mita za ujazo 9,800 katika mashamba ya miti. Aidha, usimamizi na
ulinzi wa mashamba ya miti utafanyika kwa kufanya doria, kusafisha njia za moto
zenye urefu wa mita 5,167 na kusafisha mipaka yenye urefu wa kilometa 1,063.
Wakala utapanda miti ya asili kwenye eneo la hekta 789 kwenye vyanzo vya maji
na mabonde baada ya kung’oa miti ya kigeni yenye athari iliyomea kwenye vyanzo
vya maeneo hayo. Pia, Wakala utatenga upya viunga kwenye mashamba ya miti yenye
ukubwa wa hekta 30,805.
Elimu
kwa Umma
115. Mheshimiwa Spika, elimu
kwa umma ilitolewa kupitia vipindi 75 vya
redio; vinne vya televisheni; maonesho ya Sabasaba na Nanenane; na siku ya
kupanda miti kitaifa. Vilevile, kampeni za kuzuia moto zilifanyika kwa viongozi
wa vijiji 93 vinavyozunguka hifadhi 23 za misitu na kamati 12 za maliasili za
vijiji. Aidha, katika vijiji hivyo, Wakala uliwezesha kuanzishwa kwa kamati 18
za Maliasili za vijiji. Ili kuhamasisha upandaji miti, Wakala
42
uliwezesha
vikundi 150, vijiji 30, taasisi 105 na watu binafsi 21 kuotesha jumla ya miche
4,548,853.
116.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2016/2017, Wakala utatoa elimu ya usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za misitu na ufugaji
nyuki kwa umma kwa kutayarisha na kurusha vipindi 48 vya redio, 14 vya
televisheni na maonesho ya video 35. Njia nyingine ni kupitia maonesho ya
Sabasaba, Nanenane, Siku ya Kupanda Miti, Kutundika Mizinga na Siku ya
Mazingira Kitaifa. Katika juhudi za kutatua changamoto ya moto wa msituni, kampeni
na elimu ya jinsi ya kupambana na moto itatolewa kwa watumishi na wananchi
katika vijiji 284 vinavyozunguka misitu ya asili na mashamba.
117.
Mheshimiwa
Spika, Wakala kwa kushirikiana na wadau mbalimbali utatoa elimu na kuhamasisha uzalishaji na matumizi bora
ya mkaa; kuhimiza matumizi ya nishati mbadala na majiko banifu ili kupunguza
matumizi ya nishati itokanayo na miti; kusaidia wachoma mkaa kuunda vikundi vya
kuchoma mkaa; na kuanzisha magulio ya kuuzia mkaa. Aidha, Wakala utahamasisha
na kuwajulisha wadau kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Usimamizi na
Uhifadhi wa Misitu na kuwashirikisha kupanda miti ili kukidhi lengo la kuziba
pengo la mita za ujazo 19.5 milioni ifikapo mwaka 2030.
Kuendeleza
Ufugaji Nyuki
118. Mheshimiwa Spika, katika
kuendeleza ufugaji nyuki Wakala umesimamia
manzuki 88 zenye jumla ya mizinga 6,214; na kuanzisha manzuki tano mpya zenye
mizinga 116. Vilevile, Wakala umetoa elimu kwa Wafugaji Nyuki 300, vikundi 11,
wafungashaji na wafanyabiashara ya asali 105. Aidha, katika kuhakiki ubora wa
asali inayozalishwa nchini, sampuli 84 za asali zilikusanywa na kufanyiwa
uchambuzi wa kimaabara. Matokeo yanaonesha kuwa asali ya Tanzania bado
inaendelea kukidhi viwango vya
43
ubora
wa soko la ndani na la kimataifa. Katika kuendeleza wafugaji nyuki nchini,
Wakala iliwezesha kuanzishwa na kusajiliwa kwa Chama cha kuendeleza Ufugaji
Nyuki Tanzania (Tanzania Beekeeping Development Organization -TABEDO).
Ushirikishwaji
wa jamii katika Usimamizi wa rasilimali za Misitu
119. Mheshimiwa Spika, katika
mwaka 2016/2017, Wakala utawezesha
wananchi katika vijiji vinavyozunguka hifadhi za misitu na mashamba ya miti,
kuotesha na kupanda miche ya miti 7,956,000 katika maeneo yao. Kazi nyingine ni
kupitia mipango nane ya usimamizi wa pamoja wa misitu katika vijiji nane vya
mikoa ya Tanga na Arusha; kuwezesha mipango ya usimamizi wa pamoja katika
hifadhi za misitu mitatu ya asili; kutoa mafunzo kwa kamati za vijiji 51; na
kutengeneza mipango ya usimamizi wa pamoja kwa vijiji viwili. Vilevile, Wakala
utakamilisha mipango ya usimamizi wa pamoja katika vijiji saba; kutoa mafunzo
kwa jamii kuhusu matumizi endelevu ya rasilimali za misitu na nyuki; na
shughuli za kuongeza kipato kwa wanavijiji 240 waishio kando ya misitu ya
hifadhi.
iii.
Vyuo vya Taaluma ya Misitu na
Ufugaji Nyuki
120. Mheshimiwa Spika, katika
mwaka 2015/2016, wanafunzi 683 wamedahiliwa
kama ifuatavyo:- Chuo cha Misitu Olmotonyi – Arusha 519 Chuo cha Mafunzo ya
Ufugaji Nyuki - Tabora 91 na Chuo cha Viwanda vya Misitu- Moshi 73. Vilevile,
Chuo cha Misitu, Olmotonyi kimekarabati bwalo la chakula, nyumba saba za
watumishi na mfumo wa mawasiliano kwa njia ya mtandao. Aidha, maandalizi ya
makisio ya gharama ya ujenzi (BOQ) kwa ajili ya ukarabati wa ukumbi wa
mihadhara, jengo la kuchakata magogo na jengo la kutengeneza samani
yanaendelea. Chuo cha Ufugaji nyuki Tabora kimekarabati madarasa mawili na
mabweni matatu. Pia, chuo kimemwezesha Mkufunzi mmoja kusomea Shahada ya
Uzamili.
44
121.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2016/2017, Vyuo vya Misitu na Ufugaji Nyuki vinatarajia kudahili
jumla ya wanafunzi 880 kama ifuatavyo: Chuo cha Misitu Olmotonyi, Arusha-600;
Chuo cha Viwanda vya Misitu, Moshi -150 na Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki,
Tabora -130.
122.
Mheshimiwa
Spika, Chuo cha Misitu Olmotonyi kinatarajia kujenga jengo moja la mihadhara na hosteli ya wasichana na
kukarabati nyumba nane za watumishi kupitia mradi wa ECOPRC (Empowering
Communities through Training on Participatory Forest Management, REDD+ and
Climate Change Initiatives). Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki, Tabora
kinatarajia kukarabati jengo la utawala, chumba cha mihadhara na kutengeneza
mfumo wa kuvuna maji ya mvua. Pia, Chuo kitanunua pikipiki mbili na mahema
matano. Chuo cha Viwanda vya Misitu kitajenga maktaba; kukarabati madarasa
mawili, mabweni mawili na bwalo la chakula. Vilevile, Chuo kitanunua vifaa vya
kisasa vya karakana na kuwawezesha watumishi watatu kupata mafunzo ya muda
mfupi.
iv.
Taasisi ya Utafiti wa Misitu
Tanzania
123. Mheshimiwa Spika,
katika mwaka 2015/2016, Taasisi iliendelea
na utafiti juu ya umri sahihi wa kuvuna miti ya misindano na ubora wa mbao
kutoka katika mashamba ya miti ya Rongai, Meru, na West Kilimanjaro. Taasisi
ilipima ubora wa miti ya misindano ya umri kati ya miaka 15 hadi 23 iliyoweza
kupatikana kwenye mashamba hayo. Miti ya umri kuanzia miaka kati ya 20 na 23
ilionekana kuwa na ubora ambao hauna tofauti aushi (significant difference) na
miti ya umri wa miaka 25. Hivyo, inashauriwa kuwa miti ya misindano inaweza
kuvunwa kuanzia miaka 20 na kuendelea na sio chini ya hapo ili kuwa na ubora
katika matumizi mbalimbali ya mbao. Utafiti huu umesaidia Wizara kuandaa
mwongozo bora wa uvunaji ambao utatumika
45
na
wadau wengine wenye mashamba ya miti ya misindano kwenye maeneo yenye ikolojia
inayofanana na sehemu utafiti ulikofanyika. Hata hivyo, Taasisi itaendelea
kufanya aina hii ya utafiti kwa mashamba yaliyobakia ya Rubya na Buhindi.
124.
Mheshimiwa
Spika, Taasisi imefanikiwa kuwashirikisha wakulima wanaolima kwenye miteremko ya safu za
milima ya Uluguru kutumia teknolojia ya Kilimo-Mseto. Teknolojia hiyo
inahusisha kilimo cha mchanganyiko wa mazao ya chakula, miti aina ya mkenge (Albizia versicolor) na utupa (Tephrosia vogelii). Katika kufanikisha
matumizi ya teknolojia hii, miche 11,175 ya mkenge ilizalishwa na kupandwa
katika vijiji vya Tandali (4,200), Ng’weme (264), Kibwege (660), Lugen (5,843)
na Mtombozi (208). Aidha, Taasisi imeshirikisha wananchi kuanzisha shamba la
Kilimo Mseto kwa kutumia teknolojia ya kontua katika vijiji vya Lugeni na
Tandali katika mkoa wa Morogoro. Teknolojia hizi zimewafikia wakulima 135
waishio katika miteremko ya safu za milima ya Uluguru na Wilaya ya Morogoro
Vijijini. Hata hivyo, kazi hii itaendelea katika mwaka 2016/2017 ili kubaini
matokeo ya uzalishaji.
125.
Mheshimiwa
Spika, Taasisi kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania na Wakala wa
Mbegu za Miti Tanzania imeendelea na utafiti wa uboreshaji wa miti ya asili ya
Mkongo (Afzelia quanzensis), Mvule (Milicia excelsa) na Mkangazi (Khaya anthotheca) kwa kutambua miti-mama
yenye ubora, kukusanya vipando na kuvipanda tayari kwa kuzalisha miche bora.
126.
Mheshimiwa
Spika, katika kuimarisha uwezo wa vituo vyake, taasisi imenunua kiwanja kwa ajili ya
ujenzi wa ofisi za kituo cha Dodoma katika wilaya ya Chamwino. Vilevile,
imeboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa kuweka mfumo wa maji safi kwenye
majengo ya Makao Makuu ya Taasisi mjini Morogoro. Taasisi imewezesha watumishi
nane kuhudhuria mafunzo ya
46
muda
mfupi na saba wamejiunga na mafunzo ya muda mrefu ya shahada za uzamili na uzamivu.
Aidha, watumishi sita wamehitimu masomo ya stashahada (2), shahada (2) na
shahada ya uzamivu (2) na kuajiri watumishi wengine 28 wa kada mbalimbali.
127.
Mheshimiwa
Spika, mwaka 2016/2017, Taasisi itaendelea na utafiti juu ya umri sahihi wa kuvuna miti ya misindano na ubora wa
mbao kutoka katika mashamba ya miti ya Rubya (Ukerewe) na Buhindi (Sengerema).
Vilevile, itaanza utafiti wa matumizi ya maji kwenye mashamba ya miti ya Ruvu
Kaskazini (Kibaha) na Sao Hill (Mufindi) yaliyopandwa mikaratusi na misindano.
Aidha, Taasisi itafanya utafiti juu ya tatizo la kukauka miti ya misindano
kwenye mashamba ya Mbizi (Sumbawanga) na Wino (Songea). Pia, Taasisi kwa
kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu na Wakala wa Mbegu za Miti
itaendelea na utafiti wa uboreshaji na uzalishaji miche bora ya Msaji/Mtiki (Tectona grandis), na Mkongo (Afzelia quanzensis) kwa kutumia
teknolojia ya tishu (Tissue Culture).
128.
Mheshimiwa
Spika, Taasisi itanunua magari mawili; vifaa vya maabara za utafiti wa uzalishaji na
matumizi ya misitu; itaimarisha mfumo wa TEHAMA kwenye ofisi za Makao Makuu na
vituo vya utafiti; na kujenga ofisi za vituo vya Tabora, Mufindi na Dodoma.
Aidha, Taasisi itaajiri watumishi 27 katika fani mbalimbali. Mapitio ya Mpango
Mkakati wa 2012-2016 yatafanyika ili kuandaa Mpango Mkakati wa miaka mitano
(2017-2021) utakaojumuisha masuala mapya yanayoikabili sekta ya misitu nchini.
v.
Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania
129. Mheshimiwa Spika, katika
mwaka 2015/16, Wakala umekusanya kilo
6,606 za mbegu za miti na kuuza kilo 3,353 zenye thamani ya shilingi
113,707,635. Aidha, aina 132 za mbegu za miti ziliuzwa, kati ya hizo aina 48 ni
miti ya asili ya Tanzania na 84 ni miti ya kigeni. Hadi mwezi April 2016,
47
kiasi
cha mbegu kilichokuwa katika maghala ya Wakala ni kilo 13,610 zenye thamani ya
shilingi 160,000,000.
130.
Mheshimiwa
Spika, ili kuhakikisha kuwa upatikanaji wa mbegu bora za miti unakuwa endelevu, Wakala
uliainisha vyanzo vitano vya mbegu bora za miti ya Mkongo (Afzelia quanzensis), Mwalambe, Mwiluti na Mpaulonia. Wakala
uliendelea kutunza vyanzo 35 vya mbegu za miti aina mbalimbali ikiwa ni pamoja
na Mfudufudu (Gmelina aborea),
Msindano (Pinus Patula), Mkangazi (Khaya anthotheca), Mtiki (Tectona grandis), Mwerezi (Cedrela odorata), Mvule (Milicia excelsa), Mninga (Pterocarpus angolencis), Mti kivuli (Acrocarpus fraxinifolius) na Mwarobaini (Azadirachta
indica).
131.
Mheshimiwa
Spika, Wakala uliuza miche 64,170 ya Mitiki (Tectona grandis),
Miembe (Mangifera indica), Mikangazi (Khaya Anthotheca)
Mgrevilea
(Grevillea robusta) na Mgolimazi (Trichilia emetica) yenye thamani ya
shilingi 67,616,000. Vilevile, Wakala uliendesha mafunzo ya muda mfupi kuhusu
kuanzisha bustani na kutunza miche ya miti kwa washiriki 12 kutoka mikoa ya
Morogoro na Iringa.
132.
Mheshimiwa
Spika, mwaka 2016/2017 Wakala utakusanya kilo 13,500, kuuza kilo 12,500 za mbegu za miti na kuuza miche ya miti
150,000. Aina ya mbegu zitakazouzwa ni pamoja na Msindano (Pinus patula), Mkangazi
(Khaya anthotheca), Mtiki (Tectona grandis), Mwerezi (Cedrela
odorata), Mkenge (Albizia versicolor), Mgunga (Acacia nilotica) na Mkongo (Afzelia quanzesis). Miche itakayouzwa ni
pamoja na Mitiki, Miembe (Mangifera
indica), Michungwa
(Citrus sinensis), Mkangazi (Khaya anthotheca), na Mwalambe
(Terminalia ivorensis).
133.
Mheshimiwa
Spika, ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa mbegu bora za miti, Wakala utaanzisha
vyanzo viwili vya mbegu bora za miti
48
ya
Mlonge na Mvule. Vilevile, Wakala utaendelea kutunza vyanzo 35 vya mbegu za
miti ya aina mbalimbali, kutambua na kusajili vyanzo vitatu vya mbegu za miti
aina ya Mkenge na Mgunga. Aidha, Wakala utaendesha mafunzo ya muda mfupi kwa
wadau mbalimbali kuhusu kuanzisha bustani na kutunza miche ya miti.
vi.
Mfuko wa Misitu Tanzania
134. Mheshimiwa Spika, Mfuko
unatoa ruzuku katika maeneo matatu ya
kipaumbele ambayo ni: Uhifadhi, Uendelezaji na Usimamizi wa Rasilimali Misitu;
Uboreshaji wa Maisha ya Jamii zinazoishi pembezoni mwa misitu kupitia shughuli
kama za ufugaji nyuki, ufugaji na samaki; na Utafiti ulengao kuboresha uhifadhi
na usimamizi wa rasilimali misitu. Kwa mwaka 2015/2016, Mfuko ulikadiria
kukusanya jumla ya Shilingi
6,486,171,000. Hadi Aprili, 2016, Mfuko umekusanya Shilingi 3,970,607,029.92 sawa na asilimia 61.2. Aidha, Mfuko ulitoa ruzuku kwa miradi 217 iliyokuwa
inaendelea na miradi mipya 83.
135. Mheshimiwa Spika, katika
mwaka 2016/2017, Mfuko unatarajia kukusanya
kiasi cha Shilingi 6,251,392,042 na
kutoa ruzuku kwa miradi 285 inayoendelea na miradi mipya 115. Vilevile, Mfuko
utawezesha uchapishwaji wa gazeti la “Misitu
ni Mali” ambapo nakala 8,000 zitasambazwa kwa wadau mbalimbali. Aidha,
Mfuko utagharamia utoaji wa elimu kwa Umma kupitia vipindi 24 vya redio na
vipindi 4 vya televisheni. Pia, utawezesha Wakala wa Mbegu za Miti (TTSA)
kuchapisha nakala 5,000 za Mwongozo wa Upandaji Miti Tanzania. Vilevile,
utaiwezesha Wakala wa Huduma za Misitu kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa
ukusanyaji wa maduhuli ya misitu.
c. Sekta Ndogo ya Utalii
i.
Sera na Sheria
49
136.
Mheshimiwa
Spika, ili kuboresha na kuongeza tija katika biashara ya utalii, Wizara kwa kutumia Sheria ya Utalii sura namba
29 imekamilisha na kuchapisha kanuni tano za kusimamia biashara hiyo nchini.
Kanuni hizo ni: Kanuni ya Tozo ya Maendeleo ya Utalii; Kanuni ya Ada za Leseni;
Kanuni ya Huduma za Malazi; Kanuni ya Wakala wa Utalii; na Kanuni za Waongoza
Watalii. Aidha, ili kukuza utalii endelevu, Wizara kwa kushirikiana na Benki ya
Dunia na wadau wengine inaandaa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kuendeleza utalii
nchini. Mpango Mkakati huo unaandaliwa sanjari na mapitio ya Sera ya Taifa ya
Utalii ya mwaka 1999.
137.
Mheshimiwa
Spika, Katika mwaka 2016/2017, Wizara itafanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Utalii ya
mwaka 1999 ili kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika
sekta ya utalii duniani. Aidha, ili kukuza utalii endelevu, Wizara kwa
kushirikiana na wadau inaandaa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kuendeleza utalii
nchini kwa ajili ya kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inaimarishwa. Mpango
Mkakati huo utaongeza mchango wa sekta ya utalii kwa maendeleo ya kiuchumi ya
nchi kupitia Pato la Taifa, mapato ya fedha za kigeni, ajira, kuvutia uwekezaji
na uwezeshaji wa maendeleo ya miundombinu. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na
wadau itaainisha maeneo ya uwekezaji wa hoteli za kitalii katika ukanda wa
pwani na maeneo mengine yenye vivutio.
ii.
Kuboresha Mazingira ya Biashara ya
Utalii Nchini
138.
Mheshimiwa
Spika, katika kuboresha mazingira ya biashara ya utalii nchini, Wizara ilianzisha Mfumo
wa kompyuta wa usajili na utoaji wa leseni za kufanya biashara ya utalii
(Tourism Online Registration and Licensing System). Mfumo huu umepunguza
usumbufu kwa wateja na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Aidha, Mfumo
umerahisisha kazi za
50
139. Mheshimiwa Spika, kupitia
mfumo huu, mapato yatokanayo na Leseni
za biashara ya utalii yameongezeka kutoka shilingi 3,575,629,297 mwaka
2013/2014 hadi kufikia shilingi 3,666,586,702 mwaka 2014/2015. Mwaka 2015/2016,
Wizara ililenga kukusanya shilingi 5,907,000,000 na hadi mwisho wa Aprili 2016 shilingi 4,647,797,932.21 sawa na
asilimia 82.7 zimekusanywa. Fedha hizo zimekusanywa kutoka katika Kampuni 890
kati ya Kampuni 1,220 zilizosajiliwa mwaka jana.
140.
Mheshimiwa
Spika, jitihada za kuboresha mazingira ya utendaji kazi ya wapagazi, wapishi na waongoza
watalii zimefanyika sambamba na kuboresha utoaji huduma kwa watalii. Wizara kwa
kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu
pamoja na sekta binafsi imekamilisha mikataba ya ajira ambayo watoa huduma
wataingia na waajiri. Mikataba hii inalenga kuondoa mgogoro kuhusu mazingira
bora ya kazi na ujira ambao umedumu kwa muda mrefu baina ya watoa huduma hao na
waajiri wao. Lengo ni kuhakikisha kwamba huduma katika sekta ya utalii
zinaboreshwa kwa maslahi mapana ya taifa.
141.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2016/2017 Wizara kwa kushirikiana na Benki Kuu, ofisi ya Taifa ya Takwimu, Idara ya
Uhamiaji na Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar itaendelea kufanya utafiti kuhusu
mwenendo wa biashara ya utalii nchini. Utafiti huo utasaidia kupata taarifa
sahihi ambazo zitasaidia katika kuaandaa mipango ya maendeleo ya sekta ya
utalii pamoja na kujua mchango wake katika Pato la Taifa. Aidha, wizara
itaendelea kukusanya na kuainisha takwimu za utalii zitakazowezesha kupima
ukuaji wa sekta ya utalii.
51
142. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza utalii Kanda ya
Kusini, Wizara kwa kushirikiana na
Benki ya Dunia inaandaa mradi wa “Resilient Natural Resource Management for
Growth” (REGROW). Mradi huu ambao maandalizi yake yameanza Novemba, 2014,
unatarajiwa kuanza rasmi Januari, 2017. Mradi unalenga kuboresha matumizi bora
ya ardhi kwenye maeneo yenye vivutio vya utalii, kuendeleza na kusimamia utalii
ikolojia, kuboresha miundombinu katika maeneo ya vivutio vya utalii na
kuainisha fursa za kiuchumi za kuendeleza utalii kusini mwa Tanzania. Maeneo
yatakayohusika katika utekelezaji wa mradi huu ni Hifadhi za Taifa Ruaha (Bonde
la ardhioevu Usangu), Mikumi, Udzungwa na Pori la Akiba Selous.
143.
Mheshimiwa
Spika, Utekelezaji wa Mradi huu unahusisha pia Ofisi ya Rais - TAMISEMI; Wizara za
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Maji na Umwagiliaji; Kilimo, Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi. Mradi utakuza kipato cha jamii inayoishi kandokando ya hifadhi
kutokana na shughuli za kiuchumi zitokanazo na utalii. Mradi huu ni fursa ya
kipekee ya kupanua wigo wa utalii nchini na kutimiza azma ya kuvutia watalii
milioni nane watakaoliingizia taifa dola za Marekani bilioni 20 ifikapo mwaka
2025. Mradi utakuwa ni mfano wa kuigwa katika kuonyesha mbinu bora za kuratibu
na kusimamia sekta zinazotegemeana lakini kiutendaji zinasigana na hivyo
kusababisha upotevu na uharibifu wa maliasili na vivutio vya utalii.
144.
Mheshimiwa
Spika, Wizara itaendelea kutoa elimu, kutangaza na kuhamasisha jamii katika maonesho ya
utalii saba ndani na nje ya nchi; kuendelea na kazi ya kupanga huduma za malazi
katika madaraja ya ubora (nyota) katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga,
Iringa, Mbeya na Rukwa. Wizara itaandaa Kanuni zinazosimamia mafunzo katika
sekta ya utalii; kuainisha maeneo kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya utalii
kwa kuzingatia vivutio vilivyopo; kufanya ukaguzi wa biashara ya utalii na
kufuatilia miradi ya utalii iliyopitishwa na Kituo cha Uwekezaji. Aidha, Wizara
itaunganisha Mfumo
52
wa
kompyuta wa usajili na utoaji wa leseni za kufanya biashara ya utalii na mifumo
ya TANAPA na Ngorongoro. Lengo ni kuimarisha udhibiti na kuhakikisha kuwa
Wakala walio na usajili na leseni ndiyo wanaofanya biashara ya utalii na
kuruhusiwa kuingia katika Hifadhi zetu.
iii.
Tozo ya Maendeleo ya Utalii (TDL)
145.
Mheshimiwa
Spika, Tozo ya Maendeleo ya Utalii ilianzishwa chini ya Sheria ya Utalii Sura Na. 29 ya
2008 kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya utalii nchini. Tozo hii ilianza
kukusanywa tarehe 1 Oktoba, 2013 kwa madhumuni ya kuendeleza vivutio vya
utalii; kudhibiti ubora wa huduma za utalii; mafunzo na utafiti katika tasnia
ya ukarimu na utalii; na utangazaji utalii. Tozo hii inatokana na michango ya
asilimia tatu ya pato ghafi la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi za
Taifa (TANAPA). Aidha, kila mtalii anapotumia huduma za malazi hutozwa tozo ya
kitanda siku (bed night levy), sawa na USD 1.5. Kwa mwaka 2013/2014, Wizara
ilikusanya shilingi 2,988,080,700 na katika mwaka 2014/2015 ilikusanya shilingi
4,263,541,672.
146.
Mheshimiwa
Spika, katika kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato yatokanayo na nyumba za kulala wageni, Wizara imekamilisha
zoezi la uhakiki wa nyumba zinazotoa huduma za malazi katika mikoa 25 ya
Tanzania bara. Jumla ya nyumba za huduma za malazi 1,424 zimebainishwa na
kuwekwa katika orodha ya kukusanya Tozo ya Maendeleo ya Utalii. Katika mwaka
2016/2017, Wizara itaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato katika
kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa tozo hizo.
iv.
Watalii wanaoingia na kuondoka
nchini
147.
Mheshimiwa
Spika, Wizara kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Idara ya Uhamiaji,
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Kamisheni ya Utalii Zanzibar ilifanya
utafiti wa watalii wanaoondoka nchini
53
kupitia
Viwanja vya Kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro (KIA) na Abeid
Amani Karume (AAKIA) Zanzibar. Vilevile, Utafiti huo ulifanyika katika vituo
vya kuingilia wageni vya Namanga, Tunduma, Mtukula, Manyovu na Horohoro ili
kujua idadi ya siku anazokaa mtalii, wastani wa matumizi ya mtalii kwa siku na
hatimaye kujua mapato yatokanayo na matumizi ya watalii waliotembelea vivutio
mbalimbali hapa nchini. Uchambuzi wa awali umebaini kwamba mtalii mmoja hukaa
nchini kwa wastani wa siku 10 na hutumia wastani wa dola za Marekani 263 kwa
siku kwa package tour na wastani wa
dola za Marekani 137 kwa non package.
Kwa mwaka 2015/2016, idadi ya watalii walioingia ni 1,102,619 na wastani wa
dola za Marekani 1,938.1 milioni zilipatikana.
Kubainisha
Vivutio vya Utalii Nchini
148.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2016/2017, Wizara itabaini vivutio vipya vya utalii katika mikoa
ya Mwanza, Geita, Mbeya, Manyara, Mara na Kigoma kwa lengo la kuvutia uwekezaji
na kuendeleza sekta ya utalii. Aidha, itafanya tathmini ya miradi ya utalii wa
kiutamaduni katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara na kuwajengea
uelewa juu ya miongozo ya kufanya biashara hiyo. Vilevile, mikutano miwili ya
Kamati ya Kufanikisha Utalii (Tourism
Facilitation Committee) na minne ya ushirikiano kati ya sekta ya umma na
binafsi (Public Private Dialogue Forum)
itafanyika.
v.
Bodi
ya Utalii Tanzania Utangazaji wa Utalii
149.
Mheshimiwa
Spika, Ili kutangaza utalii katika masoko yanayoibukia, Bodi ya Utalii Tanzania iliratibu misafara ya
mawakala wa utalii na waandishi wa habari 41 kutoka nchi za China, India na
Umoja wa Falme za Kiarabu kati ya Oktoba na Desemba, 2015. Vilevile, Bodi
ilishiriki katika kongamano la kuvutia wawekezaji na kutangaza utalii katika
nchi za Umoja wa
54
Falme
za Kiarabu lililofanyika Dubai mwezi Desemba, 2015. Aidha, Bodi ya Utalii
Tanzania iliratibu safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa waandishi wa habari
na wawakilishi kutoka kampuni za utalii za China wapatao 51. Safari hiyo
ilifanyika Novemba, 2015 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano
baina ya Tanzania na China. Safari hiyo ilitumika kutangaza utalii wa Tanzania
katika kampuni za utalii za China ili kuvutia watalii wengi kutoka soko la
utalii China.
150.
Mheshimiwa
Spika, Bodi ya Utalii Tanzania iliandaa na kusimamia Onesho la Pili la kimataifa lijulikanalo kama Swahili
International Tourism Expo (S!TE). Onesho hilo linalenga kutangaza utalii wa
Tanzania na kukutanisha wafanyabiashara ya utalii wa Tanzania na Wakala wa
Utalii wa kimataifa. Onesho hilo lilifanyika Dar es Salaam katika ukumbi wa
mikutano wa Mlimani City, kuanzia tarehe 1 hadi 3 Oktoba 2015. Jumla ya Kampuni
110 za utalii zinazojihusisha na utoaji wa huduma za malazi, kusafirisha
watalii na Mashirika ya ndege ya ndani na nje ya nchi zilishiriki. Onesho hilo
pia lilihudhuriwa na Wakala wa Utalii 39 kutoka nchi za Marekani, Israel,
Canada, Australia, Uholanzi, India, Ireland, Uingereza, Ujerumani, Afrika
Kusini, Falme za Kiarabu, Visiwa vya Ushelisheli na Kenya.
151.
Mheshimiwa
Spika, Bodi ya Utalii imeshiriki kikamilifu katika utangazaji utalii kupitia maonesho ya “Karibu
Travel and Tourism Fair”-Arusha na “Kili Fair”- Moshi, Kilimanjaro. Maonesho
haya huratibiwa kwa ushirikiano baina ya Bodi na Sekta binafsi yakishirikisha
waoneshaji kutoka ndani na nje ya nchi. Lengo la maonesho hayo ni kutangaza
utalii wa Tanzania na hufanyika mwezi Mei na Juni kila mwaka. Aidha, katika
kuvutia watalii kuja nchini, Bodi ilishiriki maonesho ya utangazaji utalii nje
ya nchi kupitia maonesho ya World Travel
Market London, Novemba 2015, ITB
Berlin-Ujerumani, Machi 2016 na Indaba
- Afrika Kusini Mei 2016.
55
152.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2016/2017, Bodi ya Utalii Tanzania, itaimarisha utangazaji kwa
njia ya TEHAMA ikiwemo tovuti, mitandao ya kijamii, ‘portal’ na ‘App’
inayopatikana kwenye simu za kisasa. Bodi kwa kushirikiana na Shirikisho la
Vyama vya Waendesha Biashara za Utalii Tanzania, itaandaa mikakati mahususi ya
utangazaji utalii katika masoko makuu ya utalii ya Uingereza, Ujerumani na
Marekani. Bodi itawawezesha wananchi kuimarisha utalii wa utamaduni kwa
kuongeza idadi ya vikundi jamii vinavyoshiriki katika programu ya utalii wa
Utamaduni kutoka 60 ya sasa hadi kufikia 75.
153.
Mheshimiwa
Spika, Katika kuhakikisha kuwa idadi ya watalii inaongezeka, Bodi imeandaa Tangazo
litakalorushwa katika vituo vya televisheni za CNN na BBC kwa kipindi cha mwaka
mmoja. Aidha, Bodi kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waendesha
Biashara za Utalii nchini (TCT) itaandaa mikakati mahsusi ya utangazaji utalii
katika masoko makuu ya Uingereza, Ujerumani na Marekani. Vile vile, Bodi
itaweka matangazo ya utalii “Travel Magazine” pamoja na kushiriki maonesho
matano ya utalii katika nchi za Uingereza, Afrika Kusini, Ujerumani na China.
Bodi itashirikiana na “diaspora”, mabalozi wa hiari wa utalii na balozi zetu
zilizo sehemu mbalimbali duniani katika kutangaza vivutio vya utalii. Katika
soko la ndani, Bodi itaendelea kushiriki maonesho mbalimbali hapa nchini kama
vile Sabasaba, Nanenane, Karibu Travel
Fair, Kili Fair pamoja na Tamasha
la Filamu la Zanzibar. Vilevile, itachapisha vipeperushi na majarida
yatakayosambazwa kwa wadau.
vi.
Wakala wa Chuo cha Taifa cha
Utalii (NCT)
154.
Mheshimiwa
Spika, Dira ya Wakala ni kuwa kituo bora Afrika kinachotoa mafunzo, utafiti na ushauri
katika fani za utalii na ukarimu. Hatua hiyo itafikiwa kwa kutoa mafunzo kwa
kutumia vifaa vya kisasa, kutoa kozi za
56
uongozi
na usimamizi, kuajiri watumishi wenye sifa na weledi, kuhakikisha udahili
unaongezeka mwaka hadi mwaka na kutoa huduma bora ya utafiti na ushauri.
Mitaala inayotumika katika Kampasi zote tatu ina Ithibati kamili ya Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi ambayo hurejewa kila baada ya miaka mitano.
155. Mheshimiwa Spika,
Wakala unaendesha mafunzo ngazi ya Astashahada
na Stashahada katika fani ya usafiri (air travel and ticketing) utalii na
ukarimu. Wakala una kampasi tatu ambazo ni Bustani yenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 360, Temeke 150 na Arusha 120. Ili kuboresha mafunzo, Wakala ulifanya
mapitio ya mitaala ngazi (levels) ya 4, 5 na 6 kwa kushirikisha wadau ambapo
mitaala mipya imeanza kutumika Septemba, 2015.
Tathmini
ya mahitaji ya mafunzo
156. Mheshimiwa Spika, Wakala
umefanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo
kwa wakufunzi wa vyuo 10 vinavyotoa elimu ya Ukarimu na Utalii nchini. Lengo ni
kubaini mahitaji ili kuwajengea uwezo wakufunzi watoao mafunzo katika vyuo
hivyo. Matokeo ya tathmini hiyo yalibaini mapungufu katika maeneo ya mbinu za
ufundishaji, ujuzi mwanana (soft skills), mbinu za uongozi na usimamizi katika
fani ya ukarimu na mbinu za mafunzo kwa vitendo. Matokeo haya yalisababisha
kuandaliwa kwa Programu ya Mafunzo ambayo utekelezaji wake umeanza mwezi
Desemba, 2015. Wakufunzi 48 wa Wakala walipata mafunzo yatakayowezesha kutoa
mafunzo kwa wakufunzi wengine katika fani za ukarimu na utalii hapa nchini.
Udahili
wa Wanafunzi
157. Mheshimiwa Spika,
Katika mwaka 2015/2016 Wakala umedahili jumla
ya wanafunzi 201. Kati ya hao, 123 ni ngazi ya Astashahada na 78 ni Stashahada.
Katika mwaka huo, wanafunzi 211 walihitimu mafunzo katika
57
ngazi
ya Astashahada na Stashahada katika kozi zitolewazo na Chuo. Aidha, Wakala kwa
kushirikiana na Sekta binafsi chini ya ufadhili wa Shirika la Kazi Duniani
(ILO) umeanzisha Programu ya Uanagenzi (Apprenticeship) ambapo wanafunzi 14
wamehitimu na wengine 21 wanaendelea na mafunzo.
158. Mheshimiwa Spika,
Katika mwaka 2016/2017, Wakala utadahili
wanafunzi 315 katika fani ya Ukarimu, Usafiri na Utalii hapa nchini. Kati
ya hao, wanafunzi wa ngazi ya Stashahada ni 96 na Astashahada 219. Jaribio la
Programu ya Uanagenzi (apprenticeship) ambalo lilifanyika kwa ushirikiano kati
ya Chama cha Wenye Hoteli, Shirika la Kazi Duniani na Wakala katika mikoa ya
Dar es Salaam na Arusha limekamilika. Hivyo, wakala utaanza mafunzo kwa
wanafunzi 200 chini ya programu hiyo. Ili kuinua kiwango cha huduma katika
sekta ya Utalii nchini, Wakala kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Vancouver na
sekta binafsi itaboresha kozi za muda mrefu na mfupi. Kozi hizo ni pamoja na
Huduma kwa Mteja, Uratibu wa Matukio (Event
Management) na Huduma za Usafiri wa
Anga.
d.
Sekta Ndogo ya Malikale
Sera
na Sheria
159.
Mheshimiwa
Spika, katika kuhifadhi na kuendeleza maeneo ya Malikale Wizara imeandaa mwongozo wa
uhifadhi wa mji wa kihistoria wa Mikindani-Mtwara. Aidha, Wizara imeandaa
rasimu ya Mwongozo wa uwekezaji unaobainisha maeneo ambayo wadau mbalimbali
wanaweza kuwekeza.
160.
Mheshimiwa
Spika, mwaka 2016/2017, Wizara itasimamia na kuratibu utekelezaji wa Sera na
mkakati wa kufanya maeneo ya malikale kuwa vivutio vya utalii na vituo vya
mafunzo. Vilevile, tathmini ya maeneo 22 ya malikale yaliyopo katika Mikoa ya
Lindi (4) na Tanga (18) yaliyotangazwa katika Gazeti la Serikali itafanyika.
Pia, wadau mbalimbali wataendelea
58
i.
Utangazaji
na Ushirikishwaji wa jamii na wadau wa Maeneo yenye Malikale
161.
Mheshimiwa
Spika, ili kutangaza na kuendelea kuijengea jamii uelewa kuhusu uwepo wa vivutio vya
rasilimalikale, Wizara imetangaza Utalii wa Urithi wa utamaduni katika maonesho
na maadhimisho mbalimbali ndani na nje ya nchi. Maonesho ya ndani ya nchi ni
pamoja na Sabasaba, Nanenane na maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita
vya Maji Maji yaliyofanyika Mjini Songea Februari, 2016. Aidha, Wizara
ilitangaza utalii wa utamaduni katika tamasha la Historia, Sanaa, na Utamaduni
kwa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki lililofanyikia Nairobi – Kenya, Agosti
2015. Vilevile, Wizara inaendelea kuhamasisha na kutoa kipaumbele kwa wananchi
wanaozunguka na wanaomiliki maeneo yaliyo na vivutio vya malikale ili watambue
fursa zilizopo katika maeneo hayo kama vile kuanzisha makumbusho, vituo vya
utalii, maduka ya vitu vya utamaduni, migahawa na kutembeza wageni.
ii.
Uhifadhi na Uendelezaji wa
Rasilimalikale
162.
Mheshimiwa
Spika, Wizara imeendelea kuhifadhi na kuendeleza urithi wa utamaduni. Mwaka 2015/2016,
Wizara imekarabati jengo lililokuwa mahabusu katika eneo la Makumbusho ya
Kumbukumbu ya Chifu Mkwawa, Kalenga mkoani Iringa, kuwa ofisi ya kituo. Aidha,
Wizara imekamilisha michoro ya ukarabati wa Jengo la Boma la Kijerumani
Pangani,Tanga. Vilevile, imekamilisha michoro ya ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu
na Taarifa cha Mapango ya Amboni; kukarabati jengo la Afya, Tabora; kuweka uzio
katika eneo la magofu ya kituo cha Kunduchi; kuboresha mandhari ya Kituo cha
59
163.
Mheshimiwa
Spika, katika kuhifadhi na kuendeleza maeneo ya Urithi wa Dunia ya Kilwa Kisiwani na
Songo Mnara, Wizara imechukua hatua za kuzuia mmomonyoko wa udongo kwa kujenga
ukuta karibu na gofu la Ngome ya Gereza, Kilwa Kisiwani ili kupunguza ama
kuzuia kabisa mawimbi ya bahari yasiiathiri ngome hiyo. Aidha, imeweza
kukamilisha Mpango wa Usimamizi wa Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Kilwa Kisiwani
na Songo Mnara wa miaka minne ( 2016-2019) na kukamilisha rasimu ya Mpango wa
Matumizi Bora ya Ardhi ya Kijiji cha Songo Mnara.
164.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2016/2017, Wizara itajenga Kituo cha Taarifa na Kumbukumbu kwenye
eneo la Mapango ya Amboni; uzio katika Magofu ya Kunduchi; na banda la kutolea
mihadhara na njia za waenda kwa miguu katika Magofu ya Kaole. Aidha, ukarabati
wa Jengo la Makumbusho ya Caravan Serai na Jengo la Afya Tabora utafanyika.
Wizara itakamilisha michoro na gharama kwa ajili ya kuboresha mandhari ya Kituo
cha Kumbukumbu cha Dkt. Livingstone Ujiji na Kituo cha Mji Mkongwe - Bagamoyo.
iii.
Utafiti wa Malikale
165.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2015/2016, jumla ya tafiti tisa za kisayansi za Mambo ya kale
zimefanyika katika maeneo ya Singida; Laetoli, Olduvai, Makuyuni na Tarangire-
Arusha; Bonde la Ufa la Rukwa; Isimila - Iringa na Kwamtoro - Kondoa. Tafiti
hizi zimefanyika kwa kushirikisha wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na
Taasisi za nje. Utafiti huu umewezesha Wizara na Taifa kwa jumla kunufaika kwa
kuongeza makusanyo ya mapato, kwa kupitia ada ya utafiti unaofanywa na
wataalamu toka nje ya
60
166.
Mheshimiwa
Spika, utafiti huo pia umewezesha kuboreshwa kwa miundo mbinu ya utafiti katika maeneo
ya malikale kama vile ujenzi wa maabara, stoo na samani za kuhifadhi mikusanyo
ya utafiti katika eneo la Bonde la Olduvai. Wizara inaendelea kushirikiana na
wadau mbalimbali wa utafiti ili kuendeleza tafiti nchini kwa lengo la kutatua
changamoto mbalimbali za uhifadhi na uendelezaji wa malikale na pia kuelimisha
jamii kuhusu malikale kupitia matokeo ya utafiti huo.
iv.
Ushiriki katika mikutano ya
kikanda na kimataifa
167.
Mheshimiwa
Spika, ili kuendelea kunufaika na fursa zilizopo katika uhifadhi wa malikale katika
ngazi ya kimataifa, mwaka 2015/2016, Wizara ilishiriki katika Mkutano Mkuu wa
Nchi Wanachama wa UNESCO uliofanyika Paris, Ufaransa mwezi Novemba, 2015.
Katika mkutano huo, Tanzania ilipata heshima ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa
Kamati ya Urithi wa Dunia (WHC). Fursa hiyo itaiwezesha Tanzania kushiriki
katika mipango na maamuzi yenye maslahi kwa nchi yetu na Afrika kwa ujumla
pamoja na kujenga uwezo wa wataalamu wetu.
v.
Mfuko wa Taifa wa Mambo ya Kale
168.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2015/2016, Mfuko ulipanga kukusanya kiasi cha Shilingi 1,000,000,000. Vyanzo vya Mfuko
vinatokana na
61
tozo
za viingilio zinazotozwa kwa watalii wanaotembelea vituo, ada za vibali kwa
watafiti, hati miliki (royality), Misaada (grants and donation), na mauzo
mbalimbali ya machapisho yakiwemo majarida, vipeperushi, vitabu, postcards
zenye taarifa za Mambo ya Kale. Hadi Aprili 2016, shilingi 533,353,883 ambazo ni sawa na asilimia 53.3 ya lengo zimekusanywa. Fedha za
Mfuko zilielekezwa katika utafiti, uhifadhi na uendelezaji wa maeneo yenye
rasilimalikale.
vi.
Shirika la Makumbusho ya Taifa
Tanzania
169.
Mheshimiwa
Spika, katika, mwaka 2015/2016, Shirika limeboresha maonesho ya muda na kudumu katika makumbusho zake
zote. Maboresho yaliyofanyika ni pamoja na kubadili vioneshwa na mpangilio wa
onesho, kuongeza idadi ya vioneshwa, kubadilisha karatasi za maelezo ya
vioneshwa (captions) na kuweka taa au kupaka rangi kumbi za maonesho. Maonesho
mapya kumi na moja (11) yamefanyika kwenye makumbusho za Shirika na moja (1) kwenye
Sabasaba. Kati ya maonesho hayo, moja lilikuwa onesho maalumu la picha za watu
wenye albinism kwa lengo la kuelimisha umma juu ya chanzo cha albinism ili
kuondoa unyanyapaa wa mila na desturi za Ki-Afrika. Vilevile, onesho maalumu
mseto la sanaa za kuchora na utafiti juu ya mitazamo ya mabadiliko ya matumizi
ya ardhi katika bonde la Kilombero limefanyika. Sanaa hizo zilichorwa na
wanavijiji wa bonde la Kilombero.
170.
Mheshimiwa
Spika, Shirika limeandaa onesho jipya la chimbuko la binadamu (The Cradle of Human
kind). Onesho hili liko Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni - Dar es Salaam na
limezinduliwa tarehe 18 Mei, 2016. Vilevile, Shirika limeandaa maonesho katika
sikukuu za Kitaifa kwa kushirikiana na Kitengo cha Maadhimisho ya Kitaifa Ofisi
ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Rais. Aidha, Shirika lilifanya programu
mbili za sanaa
62
ambazo
ni “Kivuko” (drama) na “Sauti Yetu” (contemporary dance). Programu za wanafunzi
wa Shule za Msingi zimekuwa zikifanyika kila siku ya Ijumaa hadi mwishoni mwa
2015. Kazi miradi za wanafunzi wa sekondari zimekuwa zinaendelea kufanyika kila
wiki.
171.
Mheshimiwa
Spika, Shirika linaendelea kuhamasisha jamii kutembelea Makumbusho na limechapisha na kusambaza vipeperushi
5,000 kwa wadau mbalimbali. Pia, Shirika limeandaa jarida liitwalo Museum and
House of Culture e-News Letter kuhamasisha jamii linalotolewa kila mwezi kwa
njia ya mtandao.
172.
Mheshimiwa
Spika, kumbukumbu ya Vita vya Maji Maji imefanyika mwezi Februari 2016 huko Songea. Katika maadhimisho
hayo ya kuwaenzi mashujaa wa vita ya Majimaji, familia ya Hayati Mzee Rashid
Mfaume Kawawa (Simba wa Vita) iliikabidhi rasmi Wizara, nyumba iliyoko
Bombambili Songea na vifaa 245 alivyotumia yeye na familia yake enzi za uhai
wake ili iwe sehemu ya Makumbusho ya Taifa. Nyumba hii inaelezea historia ya
Tanzania kupitia maisha ya Hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa.
173.
Mheshimiwa
Spika, napenda kutumia nafasi hii kuishukuru kwa mara nyingine familia ya Hayati Mzee
Rashid Mfaume Kawawa (Simba wa Vita) kwa kuitoa nyumba hiyo pamoja na vifaa mbalimbali
vitumike kwa ajili ya Makumbusho. Natoa wito kwa wananchi kuiga mfano huu ili
kuwa na makumbusho za aina mbalimbali ili kutunza kumbukumbu za maendeleo ya
taifa letu.
174.
Mheshimiwa
Spika, mwaka 2016/2017, Shirika litajenga upya nyumba 22 za jadi na utamaduni katika
Kijiji cha Makumbusho; kukarabati nyumba ya Hayati Mzee. Rashid Mfaume Kawawa
(Simba wa Vita) iliyopo Bombambili mjini Songea ili iwe Makumbusho. Mipango ya
kukarabati
63
nyumba
hii imeanza na inatarajiwa kuwa Februari 2017 itazinduliwa kuwa Makumbusho ya
Kumbukumbu ya Mzee Rashid. Kawawa. Vilevile, Shirika litafanya maandalizi ya
awali ya ujenzi wa jengo la kisasa la kuhifadhi na kuonesha magari ya
Kihistoria, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni. Aidha, Shirika litaboresha
maonesho na kuhakikisha usalama wa mikusanyo; kufanya Tamasha la Utamaduni wa
Mtanzania kwa kushirikisha jamii ya Wamwera; kuitangaza Makumbusho na kusogeza
huduma kwa jamii; kujenga uwezo na mazingira mazuri ya kufanyia kazi; na
kupanua makumbusho kwa kushirikisha wadau.
e. Utawala
na Maendeleo ya Rasilimali watu
175.
Mheshimiwa
Spika, mwaka 2015/2016, Wizara imeendelea kuratibu masuala ya Utawala na Maendeleo ya Rasilimaliwatu kwa
kusimamia masuala ya watumishi katika maeneo ya ajira, upandishwaji cheo,
kuthibitishwa kazini, mafunzo, nidhamu, maadili, ustawi na afya kwa watumishi.
Wizara imeajiri watumishi 1,020 na kati ya hao, watumishi 584 ni wa kada ya
Wanyamapori na 400 kada ya Misitu. Aidha, watumishi 118 wa kada mbalimbali
wamepandishwa cheo, watumishi 491 wamethibitishwa kazini na watumishi 30
wamebadilishwa cheo kwa kuzingatia miundo ya utumishi wa kada zao.
176.
Mheshimiwa
Spika, mwaka 2015/2016, Wizara imewezesha watumishi 155 kuhudhuria mafunzo mbalimbali ya muda mrefu na muda
mfupi. Kati ya hao, watumishi 89 wamehudhuria mafunzo ya muda mrefu na
watumishi 66 mafunzo ya muda mfupi.
177.
Mheshimiwa
Spika, Chama cha Akiba na Mikopo cha Wizara kimeendelea kuimarika ambapo idadi ya wanachama imeongezeka kutoka
75 hadi 176. Wanachama 21 wamenufaika kwa kupata mikopo ya dharura yenye
64
jumla
ya shilingi 10,500,000. Aidha, Wizara imeendelea kuwawezesha watumishi
wanaoishi na VVU waliojiweka wazi kwa kuwapatia fedha za kununulia lishe kwa
lengo la kuimarisha afya zao. Vilevile, elimu juu ya masuala ya UKIMWI na
magonjwa sugu yasiyoambukizwa imeendelea kutolewa kwa watumishi kupitia
mikutano mbalimbali.
178.
Mheshimiwa
Spika, katika kujenga mahusiano mazuri na watumishi wa Sekta nyingine na kutoa elimu kwa jamii, watumishi 80
walishiriki katika maonesho ya 39 ya Kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam
(Sabasaba) na watumishi wanawake 147 walishiriki maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani. Baraza la Wafanyakazi limekutana kujadili utekelezaji wa
Mpango na bajeti ya mwaka 2015/2016 na kupitia Mpango na bajeti ya mwaka
2016/2017. Aidha, Mapitio ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Wizara (2013
– 2016) yamefanyika na kuandaa
Mpango Mkakati (2016-2021).
179.
Mheshimiwa
Spika, mwaka 2016/2017, Wizara itaajiri watumishi 789, kati ya hao, 500 ni wa kada ya
Wanyamapori na 243 kada ya Misitu na Nyuki. Aidha, Wizara itapandisha cheo
watumishi 225 wa kada mbalimbali, watumishi 1,056 watathibitishwa kazini na
watumishi 289 watawezeshwa kuhudhuria mafunzo mbalimbali. Watumishi 105
watahudhuria mafunzo ya muda mrefu na 184 watahudhuria mafunzo ya muda mfupi
ikiwemo ya kuwaandaa wastaafu 48. Vilevile, Wizara itaendelea kuimarisha mifumo
ya kudhibiti watumishi hewa.
180.
Mheshimiwa
Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa afya itaandaa Mpango Mkakati wa kupambana
na UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi. Aidha, Wizara
itaendelea kuwawezesha watumishi wanaoishi na VVU waliojiweka wazi kupata fedha
ya huduma ya lishe na kuwawekea mazingira bora ya kutekeleza majukumu yao.
Vilevile,
65
181. Mheshimiwa Spika, Wizara
itaendelea kuimarisha mapambano dhidi
ya rushwa, kukuza maadili, kuboresha huduma kwa wateja na utawala bora. Aidha,
Wizara itaimarisha mahusiano na sekta nyingine na kuwawezesha watumishi kushiriki
maonesho na maadhimisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wiki ya Utumishi wa Umma,
Siku ya Wanawake Duniani na Mei Mosi. Pia, Wizara itaandaa mikutano miwili ya
Baraza la Wafanyakazi na itawawezesha watumishi kushiriki mashindano ya michezo
ya SHIMIWI na Mei Mosi. Vilevile, Wizara itaimarisha ushirikiano na sekta
binafsi na Wadau wa maendeleo kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuwashirikisha katika mapitio ya utekelezaji wa Sekta ya Maliasili na Utalii.
IV. SHUKURANI
182.
Mheshimiwa
Spika, napenda sasa kuchukua fursa hii kuwashukuru wale wote waliochangia kuiwezesha Wizara yangu
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Shukurani zangu za dhati ziende kwa
wananchi hususan wanaoishi kwenye maeneo yanayopakana na hifadhi. Ushiriki wao
katika kulinda rasilimali za maliasili na malikale umechangia uwepo wa
rasilimali hizo kwa maendeleo ya nchi. Nachukua nafasi hii kuwaomba kuendelea
kushirikiana nasi katika kuendeleza sekta hii.
183. Mheshimiwa
Spika, Napenda
kuzishukuru nchi, Mashirika na
Taasisi
mbalimbali kwa ushirikiano walioutoa katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu
ya Wizara yangu. Nachukua fursa hii kutaja baadhi yao kama ifuatavyo: Serikali
za Canada, China, Finland, Korea Kusini, Marekani, Norway, Ubelgiji, Ufaransa,
Ujerumani, Uswisi na Jumuiya ya nchi za Ulaya. Mashirika ni pamoja na AWF,
AWHF, BTC, FAO, FZS, GEF, GIZ, ILO, ICCROM, ICOM, ICOMOS, IUCN, HGBF, KfW,
NORAD, Trade Aid, UNDP, UNESCO, UNWTO, USAID, WCS, WHC, World Bank na WWF.
66
184.
Mheshimiwa
Spika, napenda kuwashukuru kwa dhati Wafanyakazi wote wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi
zilizopo chini ya Wizara kwa ushirikiano wanaonipa katika kutekeleza majukumu
yangu. Aidha, nawashukuru Mheshimiwa Mhandisi Ramo Makani (Mb.), Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii; Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi, Katibu Mkuu;
Mhandisi Angelina E. A. Madete, Naibu Katibu Mkuu; Wakurugenzi katika Idara,
Vitengo, Taasisi, Wakala na Mashirika yaliyo chini ya Wizara kwa ushauri na
utayari wao wakati wote katika kutekeleza majukumu ya Wizara kwa kuzingatia Dhana
ya HAPA KAZI TU.
V.
MAOMBI YA FEDHA
185.
Mheshimiwa
Spika, naomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya jumla ya Sh. 135,797,787,000 kwa mwaka 2016/2017. Kati ya fedha hizo, Sh.
118,051,105,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Sh. 17,746,682,000 ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Fedha za
Matumizi ya Kawaida zinajumuisha Sh. 59,592,676,000 za Mishahara ya
watumishi na Sh.58,458,429,000 za
Matumizi Mengineyo. Fedha za Miradi ya Maendeleo zinajumuisha Sh.
15,746,682,000 fedha za nje na Sh.2,000,000,000
fedha
za ndani.
186.
Mheshimiwa
Spika, Hotuba hii inapatikana pia katika tovuti ya Wizara ya Maliasili na Utalii:
www.mnrt.go.tz
No comments:
Post a Comment