Thursday, 27 February 2014

UMEIPATA HII YA ETO'O, UMRI WAKE NA ALICHOSEMA MOURINHO NA GIRLFRIEND WA ZAMANI WA ETO'O?

 
“Tatizo la Chelsea ni kukosa wafungaji, nina Eto’o ambaye ana miaka 32 au labda 35 nani anayejua?”.
Hiyo ilikua ni kauli ya kocha Jose Mourinho akimzungumzia Samuel Etoo na baadae mpenzi wa zamani wa Eto’o aliongea kuhusu umri wa mchezaji huyo kitu ambacho kimewashangaza watu wengi.
Anna Barranca alikuwa mpenzi wa zamani wa Eto’o na kupata mtoto mmoja wa kike ambaye hivi sasa ana miaka 11 amesema Eto’o ana miaka 39 kuelekea 40 na sio 35.
Mwanamke huyo amesema kwamba alijua kuhusu umri wa Eto’o wakati wapo Cameroon kutoka kwa mtu ambaye alikua pamoja na Etoo tangu utotoni.

No comments:

Post a Comment