Thursday, 27 February 2014

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) atakuwa Mgeni Rasmi katika siku ya kilele cha maadhimisho ya Kumbukizi ya vita vya Maji Maji na Utalii wa Utamaduni huko Songea Ruvuma


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) atakuwa Mgeni Rasmi katika siku ya kilele cha maadhimisho ya Kumbukizi ya vita vya Maji Maji na Utalii wa Utamaduni yatakayofanyika Songea Mkoani Ruvuma Februari 27 mwaka huu.
Maadhimisho hayo ya siku tatu ambayo Kitaifa yameandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Mkoa wa Ruvuma yatafunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii tarehe 25 Februari katika ukumbi wa Maliasili, mkoa wa Ruvuma.
Madhumni ya maadhimisho haya ambayo hufanyika kila mwaka ni kuwakumbuka mashujaa 67 walionyongwa tarehe 27 Februari 1906 walipokuwa katika harakati za kupinga ukoloni wa Mjerumani. Katika maadhimisha haya, Februari 25 wananchi na wadau mbalimbali wa utalii watapata fursa ya kutembelea na kujionea utajiri wa vivutio vya utalii ulioko Kusini mwa Tanzania hususan Mkoa wa Ruvuma ili waweze kuongeza uelewa na kushiriki kutangaza vivutio hivyo.
Aidha, Februari 26 Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma itaendesha warsha ya wadau itakayofanyika katika katika ukumbi wa Hospitali ya mkoa wa Ruvuma ili kutoa nafasi kwa wadau wa malikale na utalii kujadili namna bora ya kuendeleza utalii Kusini mwa Tanzania.
Wananchi wote wa mkoa wa Ruvuma, Mikoa ya jirani na nchini kote kwa ujumla, mnakaribishwa kuhudhuria maadhimisho hayo ya Kumbukizi ya vita vya Maji Maji na Utalii wa Utamaduni.

No comments:

Post a Comment