“Tumefanya mazoezi vizuri na tupo tayari kwa mapambano, sisi ni kama
wanajeshi, tunakwenda vitani hatuhofii chochote, tutahakikisha
tunapambana vilivyo kuhakikisha tunashinda mechi hiyo na kukomesha
utawala wa wapinzani wetu,” alisisitiza.
“Sioni kitu cha kuhofia kwani hapa nyumbani wengi hawakutupa nafasi
ya kushinda, lakini tukashinda (bao 1-0) hivyo hata ugenini tunaweza
kushinda hasa kama kila mchezaji atatambua majukumu yake uwanjani.
“Tunapaswa tukacheza kwa umoja na ushirikiano na yeyote atakapoona
mwenzake mambo yamemzidi, basi mara moja achukue jukumu la kumsaidia ili
kuhakikisha malengo yetu yanatimia.”
No comments:
Post a Comment