Safari hizi zitafanyika kwa hifadhi za Mikumi na Saadani wakati wa
maonesho ya kimataifa ya biashara "Saba saba" kuanzia tarehe 1 hadi 7
July 2015.
UTARATIBU UTAKUWA KAMA IFUATAVYO
- Safari zitaanza ijumaa tarehe 3 hadi jumanne tarehe 7 Julai 2015
- Kutakuwa na safari za aina mbili- za kutwa (go and return) na za kulala (over night) katika hifadhi zote za Mikumi na Saadani.
- Kwa safari za kutwa (day trips -go and return) wakubwa watalipa Tsh 20,000 na watoto Tsh 10,000. Hii itahusisha gharama ya kwenda, kiingilio, mwongoza wageni, kutalii na kurudi
- Safari za kulala gharama yake ni Tsh 35,000 (watoto), Tsh 60,000 (watu wazima) kwa Saadani. Tsh50,000 single au Tsh 60,000 double kwa Mikumi. Hii ni pamoja na usafiri kwenda na kurudi, malazi, chakula cha usiku na chai asubuhi.
- Saadani kutakuwa na Safari za boti ambazo gharama yake ni Tsh 25,000 (watoto) na Tsh 45,000 (watu wazima) ikijumuisha usafiri kwenda na kurudi pamoja na utalii wa boti.
- Safari zote hizi zitaanzia Dar es Salaam na kuishia Dar es Salaam: Kwa wanaokwenda Saadani Kituo ni Mwenge (kituo cha mafuta), kwa wanaokwenda Saadani kituo ni Kimara (Bahama mama) na Sabasabai.
- Muda wa kuondoka kwa wale wa safari za kutwa ni saa 12.00 alfajiri na kurudi jioni siku hiyo hiyo. Kwa wale wanaokwenda kulala wataondoka saa 9.00 alasiri na kurudi siku inayofuata.
- Tafadhali zingatia muda, ukichelewa fedha haitarejeshwa.
- Karibu ufurahie mandhari nzuri, ndege wazuri na wanyama wa kuvutia ambao nchi yetu imejaliwa na mwenyezi Mungu
MPANGILIO WA SAFARI
TAREHE | HIFADHI |
IDADI YA MAGARI/TRIP
|
IDADI YA WATALII WA NDANI KILA SIKU |
3.7.2015 | MIKUMI |
1
|
20 for over night (kulala) |
SAADANI |
1
|
10 for over night (kulala) | |
4.7.2015 |
MIKUMI |
1
|
28 |
SAADANI |
1
|
28 | |
5.7.2015 |
MIKUMI |
1
|
28 |
SAADANI |
2
|
56 | |
6.7.2015 |
MIKUMI |
2
|
56 |
SAADANI |
3
|
84 | |
7.7.2015 |
MIKUMI |
4
|
110 |
SAADANI |
4
|
112 | |
JUMLA |
20
|
532 |
JINSI YA KUJIANDIKISHA
Tembelea banda la TANAPA lililopo ndani ya jengo la
Wizara ya Mali Asili na Utalii katika viwanja vya Saba Saba kuanzia
tarehe 28 Juni hadi 6 Julai 2015.
Zingatia: WAHI MAPEMA, NAFASI NI CHACHE.
UKICHELEWA SAFARI PESA HAIRUDISHWI
IMETOLEWA NA IDARA YA MASOKO
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
S.L.P 3134
ARUSHA, TANZANIA
UKICHELEWA SAFARI PESA HAIRUDISHWI
IMETOLEWA NA IDARA YA MASOKO
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
S.L.P 3134
ARUSHA, TANZANIA
No comments:
Post a Comment