Thursday, 17 December 2015

KWA YEYOTE ANAYEHUSIKA TAARIFA YA SIKU KUMI NA NNE (14) KUONDOKA NA KUACHA SHUGHULI ZOTE ZA KIBINADAMU ZINAZOFANYIKA NDANI YA MSITU WA HIFADHI WA BIHARAMULO

(Chini ya Sheria ya Misitu namba 14 ya mwaka 2002 ambayo pia inatambulika Kama Sheria ya
Misitu Sura Namba 323 (RE: 2002). Na ifahamike Kwamba;
1. MSITU WA HIFADHI WA BIHARAMULO ULIOKO KATIKA WILAYA ZA BUKOMBE, BIHARAMULO NA CHATO KATIKA MKOA WA GEITA UMEHIFADHIWA KISHERIA KWA TANGAZO LA SERIKALI (GN) NA. 292 LA MWAKA 1954 NA MAREKEBISHO YA MWAKA 1959 KWA TANGAZO LA SERIKALI (GN) NA. 311.
2. MTENDAJI MKUU WA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) ANAWATAARIFU NA KUWATANGAZIA WATU WOTE WALIOVAMIA MSITU WA
HIFADHI WA BIHARAMULO KWA KUISHI NA KUFANYA SHUGHULI ZOZOTE ZA KIBINADAMU, KUWA SHUGHULI
WANAZOZIFANYA NDANI YA MSITU HUO NI KINYUME CHA SHERIA YA MSITU NAMBA 14 YA MWAKA 2002
(FOREST ACT NO. 323 (RE: 2002).
3. KWA TAARIFA HII, MNATANGAZIWA KUWA MMEVUNJA SHERIA YA MISITU NAMBA 14 YA MWAKA 2002 KIFUNGU CHA 26 (g), (h) NA 84 (1) (b), (2), (3).
4. KWA MUJIBU WA SHERIA YA MISITU ILIYOTAJWA HAPO JUU, MNATAKIWA KUSITISHA SHUGHULI ZENU ZOTE NA KUONDOKA KATIKA MSITU WA HIFADHI WA BIHARAMULO KATIKA KIPINDI CHA SIKU KUMI NA NNE (14) KUANZIA TAREHE YA TANGAZO HILI.
5. YEYOTE ATAKAYEKAIDI MAELEKEZO YALIYOMO KWENYE TANGAZO HILI, ATAONDOLEWA KWA NGUVU NA VYOMBO VYA DOLA PAMOJA NA KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
6. PIA ATAKAYEKAIDI KUTOKA KWA HIYARI YAKE MWENYEWE, ATAWAJIBIKA KULIPA GHARAMA
ZITAKAZOTOKANA NA ZOEZI LA KUWAONDOA KWA NGUVU, KWA KULIPA FIDIA ZA UHARIBIFU WA MSITU.
7. TAFADHALI ZINGATIENI KUWA, HATUA HIZO HAPO JUU ZITACHUKULIWA MARA MOJA BAADA YA SIKU KUMI NA NNE (14) ZA TAARIFA HII KUMALIZIKA KUANZIA TAREHE 14 DESEMBA, 2015.
Juma S. Mgoo
MTENDAJI MKUU
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA-D’SALA
AM

No comments:

Post a Comment