Muonekeno wa ziwa kiungululu, lililopo lugombo na kwa nyuma ni safu za milima livingstone iliyopo lufilyo.
Hakuna mto wowote unaoingiza wala kutoa maji katika ziwa kiungululu,
ziwa hili lina samaki kiasi wakubwa kwa wadogo, ukitizama kwa mbali
utaona safu za milima livingstone iliyoambaa mpaka katika kingo za ziwa
nyasa.
Katika masimulizi ya kihistoria juu ya utokeaji wa ziwa kiungululu
inasemekana, kulikuwa na mtu mmoja alitoka sehemu za mbali sana na
kufika mahali hapa, alipofika alionekana kuwa ovyo sana kwa maana ya
kwamba alikuwa mchafu sana, aliingia katika nyumba ya kwanza kuomba maji
ya kunywa kutokana na hali aliyokuwa nayo ya uchafu walimkatalia, basi
akasogea katika nyumba ya pili vivyo hivyo wakamkatalia na kumfukuza.
lakini alipofika katika nyumba ya tatu alimkuta mama mmoja msamalia
mwema ambae alimuonea huruma na kumpa maji ya kuoga, akamvisha nguo
zingine na kisha kumwandalia chakula, mara baada ya kumaliza kula ndipo
yule mtu akamwambia mama yule uhame mahala hapa uhamie sehemu nyingine
kwa maana hapa patatokea maajabu, wale watu walipomwona mama yule
anahama wakamsema na kumtukana kwa kusema kichaa anamhamisha na kumuona
kama mtu asiekuwa na akili, baada ya kutii agizo lile ikawa kama pigo
kwa wale watu waliokuwa wamebaki. Pakadidimia na kisha yakaibuka maji.
Masimulizi hayo yalitumika ili kutoa elimu kizazi hata kizazi kuzifanya
jamii kuwa na ukarimu, maana masimulizi hayo hayo yalitumika hata katika
maeneo mengine mfano kisiba, ikapu, ilamba na kingili.
lakini kijiografia inasemekana ziwa kiungululu lilitokana na mlipuko wa kivolkano mfano wa mzuri ni ziwa ngozi, kisiba n.k.
No comments:
Post a Comment