Baadhi ya askari wanyamapori waliohitimu mafunzo wakiwa kwenye paredi jana katika Pori la Akiba la Rungwa mkoani Singida, Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika kupambana na kukabiliana na majangili.
Askari wanyamapori wakionesha kwa vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu yaliyofanyika katika Pori la Akiba la Rungwa Mkoani Singida yaliyohitimishwa jana wakionesha namna ya kupambana na majangili wakati wakiwakamata majangili
7. Askari wanyamapori wakionesha kwa vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu yaliyofanyika katika Pori la Akiba la Rungwa Mkoani Singida yaliyohitimishwa jana wakionesha namna ya kupambana na majangili wakati wakimkama ta jangili akiwa amejisalimisha yeye mwenyewe.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress akizungumza wakati wa kufunga mafunzo maalumu ya ya kupambana na ujangili kwa Askari wanyamapori katika Pori la Akiba la Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika kupambana na kukabiliana na majangili.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania ( TAWA) Bw. Martin Loibook akizungumza wakati wa kufunga mafunzo maalumu ya ya kupambana na ujangili kwa Askari wanyamapori katika Pori la Akiba la Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori kupata taarifa za kiitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika kupambana na kukabiliana na majangili.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ametoa wito kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ujangili waache kazi hiyo baadala yake watafute kazi nyingine
zitakazoweza kuwaingizia vipato halali kwa kufanya hivyo wataweza kujiepusha kutiwa nguvuni na askari wanyamapori waliobobea kwa kazi hiyo.
Milanzi alitoa wito huo jana wakati wa akifunga mafunzo maalumu
ya kupambana na Ujangili kwa askari wanyamapori katika pori la akiba la
Rungwa mkoani Singida yaliyofadhiliwa na Marekani na yaliyotolewa na
Kikosi maalum cha wanajeshi kutoka Marekani.
Amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa askari wanyamapori ili kuendelea na kukabiliana na wimbi kubwa la ujangili kwa kuwa majangili wasasa wanatumia silaha za kisasa tofauti na majangili wa zamani ambao walikuwa wakitumia upinde na mishale.
Aliongeza kuwa majangili wa sasa ambao askari wanyamapori wamekuwa wakikabiliana nao maporini ni wale ambao wanatumia silaha za kivita hiyo ni lazima askari wetu wapewe mafunzo ya hali ya juu ili waweze kukabiliana nao.
Aidha Katibu Mkuu, Milanzi alisema Wizara imejipanga kuhakikisha suala la ujangili linakwisha ambapo kituo kingine cha mafunzo ya kijeshi kwa askari wanyamapori cha Mlele kilichopo Mkoani Katavi kimeanzishwa mbali na vyuo vya Pasiansi na Mweka, Likuyu Sekamaganga ambavyo pekee ndivyo vilivyokuwa vikitoa mafunzo kwa askari wanyamapori.
Aliongeza kuwa, kwa sasa Serikali imejipanga kwa kushirikiana na Interpol kuhakikisha kuwa hatakamatwa jangili tu aliyehusika kuua mnyama porini bali mtandao wote utakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria mahali popote.
Akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo, Milanzi alisema mafunzo hayo yamejikita kuwasaidia kupambana na majangili, magaidi pamoja na majambazi ambapo wao ndo watu wa kwanza kukumbana nao wakiwa porini kwani ndiko wanakotumia kujificha kwahiyo ujuzi walioupata umewaongezea ufanisi katika kulinda maliasili zilizopo kwenye maeneo yao.
Aliwataka pia wahitimu hao kufanya kazi kwa kujituma wasiishie tu kusherekea kumaliza mafunzo bali waonyeshe kwa vitendo hii itasaidia na kuipa ari Marekani pamoja na Asasi za kimataifa zenye lengo la kusaidia nchi katika vita dhidi ya Ujangili.
Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress amewataka wahitimu wazingatie mafunzo waliyopata kwa kuyafanyia kazi ili Pori la Akiba la Rungwa liwe sehemu salama kwa wanyamapori wanaopatikana katika pori hilo.
Ameahidi kuwa nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania kwa kuwa suala la ujangili bado ni kubwa linalohitaji ushirikiano wa pande zote ili liweze kutokomezwa.

No comments:
Post a Comment