Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi
akizungumza kwenye mkutano kabla ya kukabidhi rasmi hati mbili kwa
pamoja ya kuitambua Jumuiya ya JUHIWANGUMWA kama chombo halali
kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za
wanyamapori zilizopo ndani ya eneo laJumuiya hiyo kwa tangazo la
serikali Na. 204 na hati ya matumizi endelevu ya rasilimali za
Maliasili. Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika kijiji cha Utete
Wilayani Rufiji
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi (
katikati) akiwa kwenye kikao cha Kamati Endeshi ( Steering Committee)
inayosimamia Mradi wa KILOWEMP cha kujadili miradi inayotekelezwa
katika maeneo ya Wilaya ya Rufiji. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa
Ubelgiji ( BTC), Bw. Ton Snis na kushoto na upande wa kulia ni Mhifadhi
Mkuu wa Idara ya Wanyamapori. Bw. Herman Keryaro.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi
akioneshwa ramani na Mratibu wa mradi Kitaifa wa KILORWEMP Bw. Pellage
Kauzeni unaotenganisha kati ya eneo la hifadhi ya Jumuiya ya
JUHIWANGUMWA na kijiji cha Utete Wilayani Rufiji kabla ya kukabidhi
rasmi hati ya kuitambua Jumuiya hiyo kama chombo halali
kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za
wanyamapori zilizopo ndani ya eneo laJumuiya hiyo kwa tangazo la
serikali Na. 204 na hati ya matumizi endelevu ya rasilimali za
Maliasili. Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika kijiji cha Utete
Wilayani Rufiji
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa
pili kushoto) alipotembelea Kambi ya Watalii jana iitwayo Trackers
inayopatikana katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUHIWANGUMWA
mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kukabidhi rasmi hati mbili
kwa pamoja ya kuitambua Jumuiya ya JUHIWANGUMWA kama chombo halali
kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za
wanyamapori zilizopo ndani ya eneo laJumuiya hiyo kwa tangazo la
serikali Na 204 na hati ya matumizi endelevu ya rasilimali za Maliasili
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa
pilia kulia aliyekaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na na Kamati
Endeshi ( Steering Committee) inayosimamia Mradi wa KILOWEMP katika
kikao kilichofanyika jana Wilayani Rufiji . Kamati hiyo ndiyo
iliyosaidia kuratibu mpaka kufikia hatua Serikali kuamua kukabidhi hati
mbili kwa pamoja katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya
JUHIWANGUMWA.
Serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.
Gen Gaudence Milanzi, imekabidhi rasmi hati ya ya kuitambua Jumuiya
ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUHIWANGUMWA kama chombo halali
kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za
wanyamapori zilizopo ndani ya eneo la Jumuiya hiyo, Rufiji mkoani
Pwani.
Pia, imekabidhi hati ya matumizi endelevu ya rasilimali za
Maliasili hususani wanyamapori kwa kuwapa wananchi mamlaka ya
kusimamia na kutumia rasilimali hizo kwa kuwa na uhifadhi na maendeleo
endelevu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho katika maeneo yao,
Taifa na Dunia kwa ujumla.
Akizungumza jana katika kijiji cha
Utete wilayani Rufiji wakati akikabidhi hati hizo mbili kwa pamoja
kwa Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya JUHIWANGUMWA , Milanzi
amewatahadhalisha Viongozi wa Jumuiya hiyo kuwa na waadilifu wawazi
hususani katika masuala ya pesa na mikataba watakayoingia na
wawekezaji ili kuweza kuepuka migogoro isiyo ya lazima kutoka kwa
Wananchi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika jumuiya
nyingine.
‘’Tunataka fedha zitakazopatikana kupitia utalii wa
Picha na utalii wa uwindaji ( photographic and tourist hunting)
zitumike katika huduma za kijamii kwa kuboresha miundombinu, shule,
hospitali na huduma nyinginezo za kijamii na sio pesa hizo zitumike
kuwaneemesha watu wachache’’ alisema Milanzi
Aliongeza kuwa,
Serikali kuu ( Wizara) itaendelea kuwasaidia pale inapohitajika kufanya
hivyo katika masuala ya Uhifadhi, ‘’hatutaki kuwaingilia katika
masuala yenu mfano katika masuala ya mapato na matumizi hivyo
nawataka mshirikiane na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili msiweze kutumbukia
kwenye migogoro ya namna hiyo’’ alisisitiza Milanzi
Aidha ,
Maj.Gen. Milanzi amewataka Wakuu wa Wilaya ya Rufiji, Malinyi,
Kilombero na Ulanga ambazo ni Wilaya zinazounda jumuiya hiyo ya
JUHIWANGUMWA yenye ukubwa wa kilomita za mraba 496.5 Kuhakikisha kuwa
wanashirikiana na wananchi kuzuia mifugo isiingie ndani ya hifadhi
kwa kuwa ni kinyume cha sheria ya uhifadhi kulisha mifugo hifadhini.
Milanzi alisema ‘’ Suala la kuingiza mifugo kwenye hifadhi lisiwe la
kisiasa ni lazima kila mwananchi atambue kuingiza mifugo ndani ya
hifadhi ya wanyamapori ni kuvunja sheria ya Uhifadhi hivyo
atakayebainika lazima sheria ifuate mkondo wake’’
Pia, Milanzi
alishukuru Serikali ya Ubelgiji kwa kusaidia kuanzishwa kwa hifadhi hiyo
tangu mchakato ulipoanza mwaka 006 chini ya mradi wa ‘’ Eastern Selous
Conservation Project’’ kwa juhudi wanazofanya kusaidia uhifadhi na hasa
kwa kushirikisha wananchi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya
Rufiji,Bw.Juma Njwaya alisema atahakikisha Hifadhi ya JUHIWANGUMWA
inakuwa mfano katika masuala ya uwazi na uwajibakaji ili kuwawezesha
wananchi kunufaika na rasilimali zao hususani wanyamapori.
Naye ,
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Shabani Dihongo alisema wanajisikia
fahari kwa hatua ambayo Serikali imefikia ya kuweza kupewa mamlaka
kamili katika kuisimamia hifadhi yao
‘’Tutahakikisha tunafanya
doria za kutosha na pia kila mwananchi atashirikishwa ili aweze kuona
faida ya hifadhi hii ambayo tumeipigania kwa muda mrefu hatimaye leo
tumeweza kupewa mamlaka kamili ya kuweza kuisimamia’’ alisema
No comments:
Post a Comment