Tanzania imebarikiwa kwa kila kitu!
milima, mabonde, mito, wanyama, maziwa, bahari, visiwa, madini ya kila
aina na watu wake wakarimu; yote haya yanaifanya Tanzania kusifika kwa
uzuri wake huku kitovu cha amani kikiwa ndio tunu pekee ya taifa hilo.
Katika vipengele tisa vya Tuzo za Dunia
za Mashindano ya Utalii (WTA) kwa mwaka 2016 zinazotarajiwa kutolewa
Disemba 2 mwaka huu huko nchini Maldives, nchi ya Tanzania tayari
imesajili vivutio vyake 10 ili kuchuana na nchi nyingine katika tuzo
hizo.
Msemaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB),
Geofrey Tengeneza amesema “Pazia limefunguliwa tangu Septemba 23 na
litafungwa Oktoba 24. Kila Mtanzania anaweza kupiga kura kwa kuitembelea
tovuti ya WTA na kupiga kura kwenye vipengele vya dunia na Afrika ili
kuuleta ushindi nyumbani”.Kwa uchache vipengele ambavyo Tanzania imeviorodhesha ni pamoja na nchi bora ya kuitembelea, ufukwe na kisiwa bora zaidi (Zanzibar), hoteli ya kifahari na kampuni ya utunzaji wa mazingira.
Chema chajiuza kwani uzuri wa Tanzania
haufichiki, ni wakati wako sasa mtanzania mzalendo kupiga kura kupitia
tovuti ya WTA ili Tanzania itwae tuzo hizi.
No comments:
Post a Comment