Monday 16 February 2015

‘’VIONGOZI WA DINI KEMEENI UJANGILI’’

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amewataka viongozi wa dini nchini kuingilia kati mapambano dhidi ya ujangili unaofanyika nchini kwa kuwa tatizo lililopo ni kubwa kuliko uwezo wa Serikali.
Amesema kwamba viongozi wa kiroho wana nafasi kubwa ya kuzungumza na roho za watu ikiwa ni pamoja na kubadlisha fikra za waumini wao kuachana na ujangili kwani majangili si watu wanaotoka sayari nyingine bali ni miongoni kati ya waislamu na wakristo
‘’Ninawaomba viongozi wa kiroho kwa pamoja mtafakari kwa kina namna ya kuwafunza watanzania jinsi ya kulinda, kutunza na kuendeleza Maliasili tulizonazo, ili kizazi kijacho waweze kunufaika nazo’’ alisema Nyalandu.
Wito huo aliutoa Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa viongozi wa dini kuhusu mchango wao katika kuokoa maisha ya Wanyamapori na maliasili nyingine. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya kimataifa wanyamapori ya ‘’WILD AID’’
‘’Viongozi wa dini mna nguvu kubwa ambayo watu wengine wanatamani kuwa nayo kemeeni uovu huu rasilimali zetu zinakwisha kwa faida ya wachache wenye uchu wa kupata utajiri wa haraka’’Mhe.Nyalandu alisisitiza
Aidha, Mhe. Nyalandu amesema kuwa serikali inatajia kutumia ndege sizizo na rubani kwa ajili ya kupata taarifa za kiinteligensia zitakazotumika katika pori la Selous ili kutokomeza ujangili ‘’ Ninyi viongozi wa kiroho ni muhimu zaidi ya hizo drones kuishinda vita hii’’ Nyalandu alisisitiza..
‘’Ninawaombeni viongozi wa dini msiwe watu wa kwanza kuwafanya majangili wajisikie wao ni watu muhimu kwa kuwa ndio wanaoongoza kutoa sadaka kubwa msiwape viti mbele wakeemeni waachane na tabia hiyo’’ Nyalandu alisema
Awali akizungumza katika mkutano huo, Askofu mstaafu wa Anglikani Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentino Mokiwa alisema serikali iangalie adhabu kali kwa majangili kwani ujangili ni chukizo mbele za Mwenyezi Mungu
‘’Majangili wapewe dhabu ya kifo mara watakapobainika kwani kila kiumbe kiliumbwa na Mwenyezi Mungu kwa makusudi yake, adhabu hii itakuwa ni fundisho kwa wengine ’’
Kwa upande wake, Sheikh wa Dar e s Salaam Alhad Musa amesema katika Mafundisho Mungu anataka binadamu wawatendee wanyama hisani.’’

No comments:

Post a Comment