Thursday 26 May 2016

ZIWA KIUNGULULU (CRATER LAKE)

Ziwa kiungululu linapatikana katika halmashauri ya busokelo wilaya ya  Rungwe, liko umbali wa kilomita zisizozidi 48 kutoka tukuyu mjini. ziwa hili lipo eneo liitwalo lugombo katika kijiji cha kabembe kata ya itete umbali mdogo kutoka hospitali teule ya Itete.


Muonekeno wa ziwa kiungululu, lililopo lugombo na kwa nyuma ni safu za milima livingstone iliyopo lufilyo.
Hakuna mto wowote unaoingiza wala kutoa maji katika ziwa kiungululu, ziwa hili lina samaki kiasi wakubwa kwa wadogo, ukitizama kwa mbali utaona safu za milima livingstone iliyoambaa mpaka katika kingo za ziwa nyasa.
Katika masimulizi ya kihistoria juu ya utokeaji wa ziwa kiungululu inasemekana, kulikuwa na mtu mmoja alitoka sehemu za mbali sana na kufika mahali hapa, alipofika alionekana kuwa ovyo sana kwa maana ya kwamba alikuwa mchafu sana, aliingia katika nyumba ya kwanza kuomba maji ya kunywa kutokana na hali aliyokuwa nayo ya uchafu walimkatalia, basi akasogea katika nyumba ya pili vivyo hivyo wakamkatalia na kumfukuza. lakini alipofika katika nyumba ya tatu alimkuta mama mmoja msamalia mwema ambae alimuonea huruma na kumpa maji ya kuoga, akamvisha nguo zingine na kisha kumwandalia chakula, mara baada ya kumaliza kula ndipo yule mtu akamwambia mama yule uhame mahala hapa uhamie sehemu nyingine kwa maana hapa patatokea maajabu, wale watu walipomwona mama yule anahama wakamsema na kumtukana kwa kusema kichaa anamhamisha na kumuona kama mtu asiekuwa na akili, baada ya kutii agizo lile ikawa kama pigo kwa wale watu waliokuwa wamebaki. Pakadidimia na kisha yakaibuka maji.
Masimulizi hayo yalitumika ili kutoa elimu kizazi hata kizazi kuzifanya jamii kuwa na ukarimu, maana masimulizi hayo hayo yalitumika hata katika maeneo mengine mfano kisiba, ikapu, ilamba na kingili.
lakini kijiografia inasemekana ziwa kiungululu lilitokana na mlipuko wa kivolkano mfano wa mzuri ni ziwa ngozi, kisiba n.k.

No comments:

Post a Comment