Saturday 4 June 2016

HOTUBA YA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MHESHIMIWA PROF. JUMANNE ABDALLAH MAGHEMBE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KWA MWAKA 2016/2017



I.             UTANGULIZI


1.           Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu baada ya kupokea Taarifa iliyowasilishwa Bungeni na Mwenyekiti wa

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, likubali kujadili

na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.

2.           Mheshimiwa Spika, awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kukutana katika Bunge hili Tukufu la Bajeti. Naomba pia nitumie nafasi hii adhimu kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, nawapongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awalinde na kuwaongoza katika kulitumikia Taifa letu kwa uadilifu ili liendelee kuwa na amani, upendo na ustawi.

3.           Mheshimiwa Spika, napenda pia kukupongeza wewe Mheshimiwa Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuchaguliwa kuliongoza Bunge letu Tukufu. Pia, nawapongeza walioteuliwa kuwa Mawaziri na Manaibu Waziri kuziongoza Wizara mbalimbali na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kupewa ridhaa na wananchi wao kuwawakilisha katika Bunge hili Tukufu. Vilevile, nawapongeza Wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Kudumu za Bunge tuliowachagua kuongoza Kamati zetu za Bunge. Ni matumaini yangu tutashirikiana vyema katika kukamilisha na kufanikisha majukumu yetu ili kuliongoza Bunge letu kwa ufanisi.

4.           Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii pia, kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri wa Maliasili

4


na Utalii. Jukumu hili ni kubwa, naamini kwa uwezo alionijalia Mwenyezi Mungu, miongozo ya viongozi wa Serikali na kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali nitaweza kutekeleza majukumu yangu ya kusimamia kwa ufanisi Sera na Sheria za sekta zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

5.           Mheshimiwa Spika, natoa shukurani za dhati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii chini ya Mwenyekiti wake Mhandisi Atashanta Justus Nditiye (Mb.) ambayo ilijadili, kushauri na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba maoni, ushauri na maelekezo yaliyotolewa na Kamati yamezingatiwa katika bajeti hii.


6.           Mheshimiwa Spika, naomba kuungana na wenzangu kutoa salamu za pole kwa waathirika wa majanga mbalimbali yaliyolikumba Taifa ikiwa ni pamoja mafuriko na matukio ya wananchi kuuawa na wanyamapori wakali. Kipekee natoa pole kwa familia za watumishi wa Wizara ambao wamefikwa na mauti wakati wakitumikia Taifa. Tuendelee kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani. Amina.

II.           TATHMINI YA HALI YA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII NCHINI


7.           Mheshimiwa Spika, Sekta ya Maliasili na Utalii inasimamia sekta ndogo za Wanyamapori, Misitu, Ufugaji Nyuki, Utalii na Malikale. Maeneo yaliyohifadhiwa kisheria yanajumuisha misitu ya hifadhi na mbuga za wanyama ambayo ni hekta milioni 28 sawa na asilimia 33 ya ardhi ya Tanzania.

8.           Mheshimiwa Spika, maeneo yaliyohifadhiwa kisheria yanakabiliwa na ongezeko la uvamizi hivyo kusababisha migogoro baina ya

5


hifadhi zetu na watu wanaovamia kulima au kufuga ndani ya hifadhi. Kutokana na hali hii kumekuwa na mwingiliano wa maamuzi ambapo wananchi wanahamasishwa kuendelea kutumia maeneo ya hifadhi kinyume cha sheria. Vilevile, kumekuwa na matamshi mbalimbali yenye nia ya kubadili matumizi na hadhi ya maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya makazi, kilimo na mifugo hali inayotishia uhifadhi kwa ujumla.


9.           Mheshimiwa Spika, faida za uhifadhi ni dhahiri na ni kwa manufaa mapana ya kizazi cha sasa na kijacho. Hivyo basi, ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha analinda rasilimali hizo. Wizara itaendelea na jitihada za kuhifadhi na kutatua migogoro inayogusa maeneo ya hifadhi kwa kushirikisha wadau wote.

a.    Sekta ndogo ya Wanyamapori



10.       Mheshimiwa Spika, Wizara inasimamia rasilimali za wanyamapori kwenye Hifadhi za Taifa 16 zenye ukubwa wa kilometa za mraba 57,365.05 na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro lenye ukubwa wa kilometa za mraba 8,292. Aidha, inasimamia Mapori ya Akiba 28 yenye kilometa za mraba 114,782.47, Mapori Tengefu 42 yenye ukubwa wa kilometa za mraba 58,565.02,

11.       Mheshimiwa Spika, rasilimali wanyamapori imegawanyika katika aina mbili za matumizi ambayo ni ya uvunaji na yasiyo ya uvunaji. Matumizi ya uvunaji yanahusisha biashara ya wanyamapori hai na uwindaji wa wanyamapori ambayo yanafanyika ndani ya mapori ya akiba, mapori tengefu, Maeneo ya Jumuiya za Kuhifadhi Wanyamapori (WMAs) na maeneo ya wazi. Matumizi yasiyo ya uvunaji yanahusisha utalii wa picha na kuona na mafunzo ambayo hufanyika ndani ya Hifadhi za Taifa, Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na maeneo mengine yote yenye wanyamapori. Matumizi hayo yanatoa fursa kubwa za uwekezaji na ajira kwa Watanzania wengi.


6



12.       Mheshimiwa Spika, Maeneo yaliyohifadhiwa yanachangia uhifadhi wa bioanuai mbalimbali zilizo hatarini kutoweka kama faru, tembo, mbwa mwitu, simba, duma, swala-twiga (gerenuk) pamoja na jamii za ndege mbalimbali kama bungu-nusu (shoebill stork) na kasuku mapenzi (love bird). Pia maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na ardhioevu, ni vyanzo muhimu vya maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, kilimo cha umwagiliaji, matumizi ya umeme na uzalishaji viwandani. Vilevile, maeneo hayo huchangia katika uzalishaji wa hewa safi na kuondoa hewa ukaa (Carbon sink) na hivyo kuwa msingi wa maisha bora kwa viumbe hai katika sayari dunia.

13.       Mheshimiwa Spika, baadhi ya maeneo yaliyohifadhiwa yana hadhi ya kimataifa kwa kuwekwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia (World Heritage Sites). Maeneo hayo ni pamoja na Pori la Akiba Selous, Hifadhi ya Taifa Serengeti, Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Maeneo ya Hifadhi Asilia (Biosphere Reserve) ambayo ni Pori la Akiba Selous na Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara. Aidha, Hifadhi ya Ngorongoro ni moja ya maajabu saba ya dunia. Kutokana na kuwekwa kwenye hadhi hizo, maeneo hayo yamekuwa kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani na nje ya nchi yetu.


14.       Mheshimiwa Spika, Sekta ya Wanyamapori inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na:- uharibifu wa maeneo ya hifadhi za wanyamapori kutokana na shughuli za binadamu na athari za mabadiliko ya tabianchi; ujangili; moto; uvamizi wa mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa; upungufu wa watumishi na vitendea kazi; na kuingia na kuzagaa kwa silaha hususan za kivita. Aidha, baadhi ya vitalu vya uwindaji wa kitalii vimekosa ubora unaotakiwa kwa kutokuwa na wanyama wa kutosha wenye nyara zinazoweza kuwindwa. Hali hii inasababishwa na ujangili pamoja na baadhi ya wananchi kuingiza mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa. Hii

imesababisha     wimbi     la     wawekezaji     kurejesha      baadhi      ya     vitalu      hivyo

7


kuikosesha Serikali mapato ambayo ingepatikana kupitia uwindaji. Katika mwaka 2015/2016, vitalu tisa vimerejeshwa na kufanya idadi ya vitalu vilivyorejeshwa kuwa 44 kuanzia mwaka 2013.


Wizara itaendelea kutekeleza Mkakati wa Kupambana na na Ujangili wa mwaka 2014-2019 kwa kuimarisha doria, intelijensia na upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kudhibiti ujangili. Aidha, Wizara itaendeleza juhudi za ushirikiano na nchi jirani katika maeneo ya rasilimali wanyamapori zinazovuka mipaka.

b.   Sekta ndogo ya Misitu


15.         Mheshimiwa Spika, Tathmini ya rasilimali za misitu iliyofanyika mwaka 2010 hadi 2013 ilibainisha kuwa Tanzania ina misitu yenye ukubwa wa hekta 48.1 milioni. Kati ya hekta hizo, asilimia 93 ni misitu ya mataji wazi (woodland) na asilimia 7 ni misitu iliyofunga. Mgawanyo wa mamlaka za usimamizi wa misitu hiyo ni kama ifuatavyo:- Serikali Kuu hekta milioni 19.24 ambayo ni asilimia 34.5; Serikali za Mitaa kupitia Halmashauri za Wilaya hekta million 3.1 ambayo ni asilimia 6.5; misitu iliyo katika ardhi za vijiji ni hekta 21.9 ambayo ni asilimia 45.7; na watu binafsi na vikundi wanasimamia hekta milioni 3.5 ambayo ni asilimia 7.3. Eneo lililobaki lenye ukubwa wa hekta 2.87 sawa na asilimia 6.0 ni ardhi huria.

16.       Mheshimiwa Spika, Tanzania ina miti yenye meta za ujazo milioni 1,046.9 inayoweza kuvunwa kibiashara kati ya jumla ya meta za ujazo milioni 3,322 za misitu yote nchini. Hata hivyo, maeneo ambayo uvunaji wa mazao ya misitu unaweza kufanyika kisheria ni hekta milioni 20 ambayo ni sawa na asilimia 35 ya ujazo wote wa misitu. Zaidi ya asilimia 70 ya kiasi cha ujazo wa miti unaopaswa kuvunwa kinapatikana katika mikoa ya Mbeya, Lindi, Ruvuma, Tabora, Katavi na Morogoro.

8



17.       Mheshimiwa Spika, Tanzania inakadiriwa kuwa na mita za ujazo bilioni 3.3 za miti, kati ya hizo, mita za ujazo 3.2 bilioni sawa na asilimia 97 ipo katika misitu ya asili na mita za ujazo 9.9 milioni sawa na asilimia 3 katika misitu ya kupandwa. Nusu ya ujazo wa miti inapatikana katika maeneo yaliyohifadhiwa kisheria. Mahitaji halisi ya mazao timbao kwa sasa yanakadiriwa kuwa meta za ujazo milioni 62.3 kwa mwaka. Hata hivyo, ujazo unaoweza kupatikana kutokana na uvunaji unaofanyika kisheria na kwa njia endelevu ni meta za ujazo milioni 42.8 tu. Zaidi ya asilimia 70 ya kiasi hiki cha ujazo wa miti unaopaswa kuvunwa kinapatikana katika mikoa ya Mbeya, Lindi, Ruvuma, Tabora, Katavi na Morogoro. Takwimu hizi zinaonesha kuwa kuna upungufu wa meta za ujazo milioni 19.5. kwa mwaka.


18.       Mheshimiwa Spika, misitu ina umuhimu mkubwa katika uhifadhi wa bioanuai, udongo na vyanzo vya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme na matumizi ya nyumbani, viwandani na umwagiliaji. Aidha, misitu ni muhimu katika kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa inanyoya hewa ukaa. Vilevile, inatupatia mbao, kuni, mkaa, chakula, malisho ya mifugo, dawa, kivuli na makazi ya wanyama.



19.       Mheshimiwa Spika, misitu inachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa Taifa kwa kutoa zaidi ya asilimia 75 ya vifaa vya kujengea na huchangia zaidi ya asilimia 90 ya nishati inayotumika nchini. Vilevile, Misitu ni nguzo ya maendeleo ya uchumi kutokana na mchango wake katika kuchangia fedha katika mfuko wa Serikali. Sekta ya Misitu inachangia kwa takribani asilimia 3 ya ajira rasmi nchini; na ajira isiyo rasmi inafikia watu milioni 3.






9


20.       Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na utegemezi mkubwa wa misitu kama chanzo rahisi na kikuu cha nishati, ambapo uvunaji mkubwa wa mkaa umeathiri sana ubora wa misitu. Mahitaji ya mazao ya misitu yamesababisha kutoweka kwa eneo la misitu linalokadiriwa kuwa na hekta 372,000 kwa mwaka. Hatua inayotakiwa kuchukuliwa kwa ushirikiano na wadau wote ni kupanda hekta 185,000 za miti kila mwaka kwa kipindi cha miaka 16 ijayo hadi mwaka 2030 ili kuziba pengo la upungufu uliopo wa mazao ya misitu unaokadiriwa kuwa meta za ujazo milioni 19.5 kwa mwaka. Wizara inaendeleza ushirikiano na wadau wa sekta mbalimbali hasa Wizara ya Nishati na Madini,Taasisi zisizo za Serikali na jamii kwa ujumla ili kupunguza utegemezi wa misitu kama chanzo kikuu cha nishati viwandani na kwa matumizi ya nyumbani. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na wadau inahamasisha jamii kutumia nishati mbadala na matumizi ya majiko banifu. Elimu hii inatolewa kupitia vipindi vya radio na televisheni, mikutano ya hadhara, makongamamo na warsha.

21.       Mheshimiwa Spika, Moto umeendelea kuwa changamoto kwa uhifadhi wa misitu. Takwimu zinaonesha kuwa, takriban asilimia 10-14 ya maeneo ya misitu Tanzania yanaathirika na moto kila mwaka. Hii ni wastani wa hekta milioni sita za maeneo ya misitu kwa mwaka. Katika kutatua changamoto hii, Wizara imeendelea kusafisha barabara za kuzuia moto kuingia msituni na kutoa elimu ya jinsi ya kupambana na moto kwa jamii inayozunguka misitu ya asili na mashamba. Vilevile, Wizara itaendelea kutunza miundombinu ya kufuatilia na kubaini matukio ya nchini.



c.    Sekta Ndogo ya Ufugaji Nyuki


22.       Mheshimiwa Spika, ukubwa wa misitu tuliyonayo unaweza kukidhi uzalishaji wa takribani tani 138,000 za asali na tani 9,200 za nta kwa mwaka. Hata hivyo, mpaka sasa uzalishaji umefikia tani 34,000 za asali sawa

10


na asilimia 24.6 ya uwezo huo na tani 625 za nta peke yake. Katika kuongeza msukumo wa uzalishaji wa mazao ya nyuki na huduma ya uchavushaji mimea, Wizara imeainisha maeneo ya kuanzisha hifadhi 46 za nyuki zenye ukubwa wa takriban hekta 143,936.78. Kati ya hizo, hifadhi 26 zenye ukubwa wa hekta 74,323.78 zitamilikiwa na Serikali za vijiji na 20 zenye ukubwa wa hekta 69,613 ni za Serikali Kuu.

23.       Mheshimiwa Spika, ufugaji nyuki una mchango mkubwa katika uhifadhi na ukuaji wa uchumi. Kwa kuhifadhi misitu ya asili na ya kupandwa tunapata fursa ya kufanya shughuli za ufugaji nyuki katika maeneo hayo. Shughuli hizo zinasaidia kuhifadhi misitu yetu ambayo ni takribani hekta 48.1 milioni nchi nzima. Ufugaji nyuki umepewa msukumo kwa kuanzishiwa mafunzo maalumu ngazi ya shahada katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na hivyo kuongeza idadi ya wataalamu wa kuweza kusimamia sekta ndogo ya ufugaji nyuki. Vilevile, Kitengo cha ufugaji nyuki kimeimarishwa kuwa Idara inayojitegemea ili kutoa msukumo stahili katika shughuli za ufugaji nyuki.




24.       Mheshimiwa Spika, takwimu zinaonesha kuwa mahitaji katika soko la ndani yanaongezeka sanjari na soko la dunia ukilinganisha na uzalishaji na upatikanaji wa asali. Aidha, Tanzania ni miongoni mwa nchi 5 za Afrika zinazoruhusiwa kuuza asali yake katika soko la Ulaya. Takwimu za usafirishaji wa mazao ya nyuki nchi nje ni wastani wa tani 278.6 za asali na tani 347.3 za nta. Ufugaji nyuki una fursa ya kuzalisha pia mazao mengine yanayotumika kwa urembo na tiba ambayo yanahitajika katika soko la dunia ikiwemo gundi (propolis), maziwa ya nyuki (royal jelly), chavua (pollen) na sumu ya nyuki (bee venom). Naomba kutumia fursa hii kuwahimiza Waheshimiwa Wabunge kuhamasisha wananchi katika majimbo yetu kushiriki katika shughuli za ufugaji nyuki kwa kuwa zinatoa fursa nyingi zikiwemo kuanzisha



11


viwanda vya kuhudumia mahitaji ya sekta ya ufugaji nyuki, ajira, huduma ya uchavushaji wa mimea na manufaa mengine.


25.       Mheshimiwa Spika, Sekta ya ufugaji nyuki inakabiliwa na changamoto ya baadhi ya wafugaji nchini kuzalisha mazao ya nyuki yasiyokidhi viwango vya ubora, hivyo kusababisha kutopata bei nzuri katika soko la ndani na nje. Wizara yangu itaendelea kutoa elimu ya uvunaji, uchakataji na ufungashaji wa mazao yatokanayo na nyuki ili kukidhi viwango vya ubora.




d.   Sekta ndogo ya Utalii


26.       Mheshimiwa Spika, Sekta ndogo ya Utalii imeshika nafasi ya kwanza katika kuliingizia Taifa fedha za kigeni kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo (2012 – 2015). Fedha hizo ni sawa na wastani wa Dola za Kimarekani milioni 2,002 kwa mwaka ambayo ni asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni nchini. Kwa mwaka 2015, idadi ya watalii waliongia nchini ilikuwa 1,102,619. Sekta huchangia takriban ajira 500,000 za moja kwa moja na ajira 1,000,000 ambazo si za moja kwa moja. Aidha, Sekta imeendelea kutoa ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi katika Sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, elimu, mawasiliano, miundombinu, burudani, usafirishaji na uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa watalii. Maendeleo ya Sekta ya utalii nchini yamechangiwa na uwepo wa amani na utulivu; ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano; uboreshwaji wa miundombinu; na ubora wa huduma za malazi na ukarimu. Vivutio vikuu vya Utalii wa Tanzania ni wanyamapori, upandaji milima, utamaduni, malikale, mandhari na fukwe.

27.       Mheshimiwa Spika, Sekta ya utalii inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa ya miundombinu bora katika maeneo yenye vivutio ikiwemo

12


huduma za maji, umeme na barabara. Aidha, hatuna Shirika la Ndege lenye uwezo wa kuleta watalii moja kwa moja kutoka katika nchi ambazo ni masoko makuu ya utalii. Hivyo, Wizara inaishukuru Serikali kwa mpango wa kununua ndege tatu katika mwaka ujao wa fedha ili kukidhi haja hii katika kipindi cha mpito wakati Serikali ikiimarisha Shirika la ndege la Taifa.

28.       Mheshimiwa Spika, matumizi ya kadi za kielektroniki kuingia katika maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya utalii yanakabiliwa na changamoto ikiwemo baadhi ya wageni kutokuwa na uelewa wa njia hiyo ya malipo. Teknolojia hii inahitaji uwepo wa mtandao wa intaneti katika maeneo yote ambayo ulipaji unafanyika. Ili kukabili changamoto hizo, Wizara inaendelea kutoa elimu kwa wageni kuhusu huduma hiyo ambayo haihitaji matumizi ya fedha taslimu. Wizara inawekeza katika kuimarisha miundombinu za ulipaji wa mfumo wa mtandao kwa kununua satellite dishes na communication boosters. Vilevile, inawasiliana na watoa huduma za kibenki ili kuhakikisha kwamba huduma za mfumo wa ulipaji kwa mtandao zinapatikana katika maeneo ya hifadhi.


29.       Mheshimiwa Spika, upo mwamko mdogo wa wananchi katika kutembelea vivutio vya utalii pamoja na kushiriki katika biashara za utalii pamoja na Serikali kuweka gharama ndogo za viingilio katika Hifadhi za Taifa kwa Watanzania na raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa sasa, kiingilio ni shilingi 10,000 kwa Hifadhi zilizopo Kaskazini; shilingi 5,000 hadi 15,000 kwa Hifadhi zilizopo Kusini; na watoto shilingi 2,000 kwa Hifadhi zote nchini. Magari madogo hutozwa shilingi 20,000 katika hifadhi zote. Katika kukabiliana na changamoto hii, Wizara itaendeleza kampeni mbalimbali za kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za utalii. Aidha, Wizara imebaini kuwa, Sekta ya Utalii haijawekwa katika vipaumbele kwenye mipango ya maendeleo ya Mikoa na Wilaya. Katika kukabiliana na hili, Wizara itatoa elimu ya



13


uhamasishaji kwa wadau na watoa maamuzi mbalimbali ili sekta hii ipewe kipaumbele stahili katika mipango ya maendeleo ya Taifa, Mikoa na Wilaya.

30.       Mheshimiwa Spika, kuna ugumu wa kupata mitaji ya uhakika kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ili kuendesha biashara za utalii. Ugumu huo unatokana na riba kubwa zinazotozwa na Benki za Biashara. Ili kukabiliana na changamoto hii, Wizara itaendelea kushawishi taasisi za fedha kuona fursa ya kufanya biashara na wafanyabiashara wadogo na wa kati katika biashara za utalii. Aidha, ipo changamoto ya miundombinu ya kuwezesha malipo kwa kutumia credit card ambayo watalii wengi huitumia kulipia huduma mbalimbali.




31.       Mheshimiwa Spika, changamoto nyingine ni kutokuwa na ardhi iliyotengwa kwa ajili ya kuendeleza utalii nchini. Wizara itaendelea kuzishawishi Mamlaka za Ardhi na Mipango Miji katika Halmashauri zetu kutenga maeneo maalum kwa ajili ya uwekezaji wa shughuli za utalii na kuhamasisha wananchi wanaomiliki ardhi kuingia ubia na wawekezaji wa utalii ili kutumia ardhi yao katika maendeleo ya sekta ya utalii.

32.       Mheshimiwa Spika, upo uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi na utaalamu katika sekta ya utalii na hoteli. Ili kukabiliana na changamoto hii, Wizara imeanzisha Wakala wa Chuo cha Utalii cha Taifa na kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha vyuo vyake. Aidha, itawaendeleza watumishi kitaaluma kwa kuwapa mafunzo stahili ili kuboresha utendaji kazi na kuongeza tija. Vilevile, Wizara itaendelea kujenga ushirikiano wa karibu baina ya Sekta ya Utalii na sekta nyingine za uchumi na uzalishaji kama vile kilimo, wazalishaji wa vyakula na vinywaji, vifaa vya ujenzi na samani na miundombinu ili kuboresha huduma za utalii.



14


33.       Mheshimiwa Spika, ili kuongeza ajira na mapato ya utalii, sekta nyingine wanashauriwa kutoa huduma na bidhaa zenye viwango kwa uwingi na kwa wakati unaohitajika katika soko la utalii. Aidha, wawekezaji katika sekta ya utalii waendelee kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini katika uwekezaji na utoaji huduma kwa wageni. Wizara itaendelea kuunga mkono jitihada za kujenga mazingira ya ustawi wa viwanda kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa wingi na ubora unaohitajika katika sekta ya utalii.

e.    Sekta ndogo ya Malikale


34.       Mheshimiwa Spika, Malikale ni rasilimali za Urithi wa Utamaduni zinazoshikika na zisizoshikika; zinazohamishika, na zisizohamishika, zilizo nchi kavu na ndani ya maji ambazo zimetengenezwa, kuundwa au kuhusika na maisha ya binadamu. Majukumu ya Sekta ndogo ya Malikale yanasimamiwa na kutekelezwa na Idara ya Mambo ya Kale pamoja na Shirika la Makumbusho ya Taifa. Nchi yetu imebarikiwa kuwa na hazina kubwa ya urithi wa malikale. Uhifadhi wa malikale unatekelezwa kwa kuzingatia Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997; Sera ya Malikale ya mwaka 2008; Sheria ya Mambo ya Kale, Sura ya 333 ya mwaka 2002 na Sheria ya Makumbusho ya No.7 ya mwaka 1980. Wizara ina jukumu la kutafiti, kutambua, kukusanya, kuonyesha, kuhifadhi, kulinda na kutangaza Kumbukumbu na Urithi wa Taifa wa Kitamaduni. Kazi hizo zinafanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Malikale ikitumika vizuri inaweza kuleta mapato kwa sekta binafsi, sekta ya umma na Taifa kwa ujumla.

35.       Mheshimiwa Spika, Maeneo ya malikale nchini ni zaidi ya 500 na kati ya hayo maeneo 130 yametangazwa katika Gazeti la Serikali kuwa Kumbukumbu ya Urithi wa Taifa letu ambapo 14 yanasimamiwa na Wizara. Maeneo yaliyobaki yanasimamiwa na wamiliki binafsi, Taasisi na Mashirika Katika kipindi cha mwaka 2012/2013 hadi 2014/2015 wageni waliotembelea katika maeneo ya Mambo ya Kale ni 679,116.

15




36.       Mheshimiwa Spika, upo uharibifu wa maeneo yenye malikale na majengo ya kihistoria pamoja na uvamizi wa maeneo hayo. Aidha, changamoto katika uhifadhi wa malikale ni gharama za kutunza malikale kwa kuzingatia kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hali hii imechangiwa na uelewa mdogo wa jamii kuhusu thamani, umuhimu na fursa zilizopo katika urithi wa utamaduni hivyo kutohamasika kuhifadhi na kuendeleza rasilimalikale.


37.       Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kushirikiana na Serikali za Mitaa, Serikali za Vijiji na jamii kwa ujumla katika uhifadhi wa malikale. Aidha, itaimarisha ushirikiano baina yake na Taasisi za Serikali na binafsi katika usimamizi wa Sheria na kanuni ili kuhifadhi na kuendeleza malikale. Wizara imeandaa rasimu ya Mwongozo wa uwekezaji unaobainisha maeneo ambayo wadau mbalimbali wanaweza kuwekeza katika shughuli za uhifadhi na ukuzaji utalii. Vilevile, Wizara itaendeleza mikutano na wadau ili kushawishi uhifadhi wa majengo mijini.




III.         UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KWA MWAKA 2015/2016 NA MALENGO YA MWAKA 2016/2017

38.       Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka 2015/2016, Wizara ilizingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA II); Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/2012 hadi 2015/2016); Mpango Mkakati wa Wizara (2013 – 2016); Mikataba ya Kimataifa ambayo Tanzania imeridhia na Maelekezo mengine ya Kitaifa. Aidha, Wizara imeendelea kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni mbalimbali zinazohusu uhifadhi wa maliasili na malikale na uendelezaji utalii.


16


39.       Mheshimiwa Spika Mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 umezingatia: Sera na Mikakati ya Serikali; Malengo na kazi zilizoainishwa katika Mpango Mkakati wa Wizara (2016-2021); Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015 – 2020; na masuala yaliyojitokeza katika Hotuba ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kuzindua Bunge la 11 mwezi Novemba, 2015.

40.       Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2015/2016 hadi Aprili 2016, na Mpango wa mwaka 2016/2017 katika Wizara yangu umeainishwa kama ifuatavyo:-

a.    Sekta Ndogo ya Wanyamapori

i.             Sheria na Kanuni


41.         Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 (Sura 283), Kanuni za Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (Wildlife Management Areas - WMAs) zimepitiwa. Aidha, Rasimu za Kanuni za Uchimbaji Madini katika maeneo yaliyohifadhiwa, Kanuni za Usajili wa Nyara, Kanuni za Shoroba, Kingo na Mapito ya Wanyamapori zimeandaliwa.

42.         Mheshimiwa Spika, katika 2016/2017 Wizara itaendelea kupitia na kuandaa Kanuni nne za: Jeshi Usu (Paramilitary); Usimamizi wa Mapori Tengefu; Shoroba; Kingo na Mapito ya Wanyamapori. Aidha, Wizara itaendelea kukusanya nyara za Serikali zilizopo kwenye vituo vya Polisi, Halmashauri za Wilaya, Hifadhi za Taifa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na kuhakiki nyara zilizohifadhiwa.

ii.           Uhifadhi na Usimamizi wa Wanyamapori




17


43.         Mheshimiwa Spika, katika kudhibiti ujangili wa wanyamapori, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi ilibaini kuwa ujangili unafanyika katika ngazi (levels) tano. Ngazi hizo ni: (i) baadhi ya wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayopakana na hifadhi na watumishi wasio waaminifu; (ii) wawindaji haramu wanaojishusisha moja kwa moja na kuua wanyama; (iii) wasafirishaji na madalali; (iv) wawezeshaji kwenye ngazi ya nchi wanaonunua nyara, kusambaza vitendea kazi (silaha) ambao ni kiungo kati ya majangili nguli na watakatishaji fedha na wahalifu walioainishwa katika ngazi tatu za awali;na (v) ni majangili nguli wa kimataifa. Kutokana na hali hiyo, Wizara iliimarisha Kitengo chake cha Intelijensia na kufanya doria kwa kuzingatia mfumo wa makundi hayo.

44.         Mheshimiwa Spika, doria zilifanyika ndani na nje ya Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu ambapo siku-doria 109,474 zilifanyika katika mwaka 2015/2016. Doria hizi ziliwezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 1,176 na kesi 654 zilifunguliwa. Kesi 161 zilimalizika kwa wahalifu 53 kuhukumiwa kifungo cha jumla ya miezi 6,360 na shilingi 363,904,800 kulipwa kama faini. Kati ya wahalifu waliohukumiwa, nane ni majangili nguli wenye mitandao ya kimataifa. Katika doria zilizofanyika, nyara mbalimbali za Serikali zilikamatwa. Nyara hizo ni pamoja na wanyamapori hai (mijusi 315, kobe 202, tumbili 81 na nyani mmoja) vipande 253 vya meno ghafi ya tembo vyenye uzito wa kilo 634 na vipande 34 vya meno ya tembo yaliyochakatwa vyenye uzito wa kilo 2. Vilevile, kilo 10,096 za nyamapori wa aina mbalimbali na ngozi 39 za wanyamapori zilikamatwa. Aidha, bunduki 85 na risasi 1,235 za aina tofauti zilikamatwa.

iii.         Ushirikishwaji jamii katika Uhifadhi wa Wanyamapori


45.         Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuhamasisha wananchi kutenga maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs). Jumuiya za Waga iliyopo Iringa Vijijini na Mufindi, UMEMARUWA (Uhifadhi na Matumizi

18


Endelevu ya Maliasili katika tarafa za Rujewa na Wanging’ombe) zimekamilisha vigezo na kutangazwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali. Aidha, Wizara ipo katika hatua ya mwisho ya kulitangaza eneo la JUHIWANGUMWA kwenye gazeti la Serikali kuwa Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii iliyoidhinishwa. Jumuiya ya Hifadhi Wanyamapori ILUMA (Ifakara, Lupilo na Mang’ula) - Kilombero na Ulanga imekamilisha Mpango wa Usimamizi wa Rasilimali na kupatiwa haki ya Matumizi ya Rasilimali ya Wanyamapori.

46.         Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2016/2017, wananchi wanaoishi katika maeneo yanayopakana na Hifadhi za Wanyamapori wataendelea kuhamasishwa kushiriki katika uanzishaji na usimamizi wa maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs). Hatua za uanzishaji wa WMAs za Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Ngorongo, Utete na Mwaseni (JUHIWANGUMWA – Rufiji); Ziwa Natron Kaskazini - Longido; Mpimbwe - Mlele; Matumizi Bora ya Maliasili Miguruwe, Njinjo na Kandawale (MBOMAMINJIKA - Kilwa); na Igombe - Sagara Wildlife Management Area (ISAMIWA-Urambo) zitakamilishwa. Wizara kwa kushirikiana na wananchi itaanzisha Mapori ya Akiba ya Litumbandyosi–Mbinga; Geza-Mazoa – Songea; Kipindimbi – Nachingwea; Mavuji – Kilwa; na Hifadhi ya Ardhioevu ya Mto Makangage.




iv.         Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA)


47.         Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi na ulinzi wa Wanyamapori, Serikali imeanzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA). Mamlaka hii na Bodi yake ilizinduliwa rasmi na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 16 Oktoba 2015. Vilevile, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ameteuliwa pamoja watendaji wengine. Hivi karibuni TAWA itahamia makao yake makuu ya muda mjini Morogoro.

19



48.         Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Ofisi ya Msajili wa Hazina imekamilisha taratibu zote za kuwezesha Mamlaka hiyo kuanza kufanya kazi. Napenda kulitaarifu Bunge lako tukufu kuwa, kuanzia tarehe 1 Julai, 2016, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori itaanza kutekeleza majukumu yake rasmi. Majukumu yote ya Usimamizi wa rasilimali ya Wanyamapori katika Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na Maeneo ya Wazi yenye wanyamapori nje ya Hifadhi za Taifa na Eneo la Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro yatasimamiwa na Mamlaka hiyo.

49.         Mheshimiwa Spika, pamoja na kuanzishwa kwa TAWA, Idara ya Wanyamapori itaendelea kuratibu na kurekebu Sera, Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta ndogo ya Wanyamapori. Vilevile, Idara itaendeleza juhudi za kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika uhifadhi wanyamapori, kuanzisha na kusimamia Jeshi Usu (Paramilitary) pamoja na kuunganisha juhudi za taasisi za utafiti na mafunzo.

v.           Ulinzi wa Maisha na Mali za Wananchi dhidi ya Wanyamapori


50.         Mheshimiwa Spika, tatizo la wanyamapori wakali na waharibifu limeendelea kuwa changamoto ambapo katika kipindi cha Julai, 2015 hadi Machi, 2016 watu 13 waliuawa na 17 kujeruhiwa. Aidha, mbuzi 39 wameuawa na wanyamapori wakali na mazao katika mashamba yenye ukubwa wa hekta

712.31    yaliharibiwa. Katika kukabiliana na tatizo hilo, Wizara imeendelea kufanya doria za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneo mbalimbali hususan kwenye wilaya 29 zenye matatizo sugu. Jumla ya Shilingi 10,000,000 zililipwa kama kifuta machozi na shilingi 182,875,600 zililipwa kama kifuta jasho kwa ajili ya mazao yaliyoharibiwa.

51.         Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Mamlaka itaendeleza ulinzi wa maisha na mali za wananchi dhidi ya wanyamapori

20


wakali na waharibifu. Vilevile, itafanya doria za kukabiliana na wanyamapori hao. Aidha, utaratibu wa kulipa kifuta machozi na kifuta jasho kwa wananchi walioathirika na wanyamapori wakali na waharibifu utaendelea.

52.           Mheshimiwa Spika, Mamlaka itaendelea na utatuzi wa migogoro ya mipaka baina ya wananchi na maeneo ya hifadhi za wanyamapori. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kufanya doria ndani na nje ya Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu; kuimarisha intelijensia katika doria ikiwemo kuwapatia watumishi mafunzo stahiki na vitendea kazi ambavyo ni pamoja na magari, mahema, sare za watumishi, redio na vifaa vya mawasiliano vya kisasa, silaha, boti za doria pamoja na vifaa vingine vya kufanyia doria wakati wa usiku.

vi.         Migogoro ya Mipaka na shughuli za kibinadamu ndani ya Hifadhi za Wanyamapori

53.         Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na migogoro ya mara kwa mara baina ya wananchi na maeneo ya Hifadhi, Wizara imefanikiwa kuainisha na kuhakiki mipaka ya maeneo yaliyohifadhiwa yenye migogoro kwa mujibu wa Matangazo ya Serikali. Kazi hii imefanyika kwa kushirikiana na wataalam kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais (TAMISEMI). Maeneo yaliyohusika ni Hifadhi ya Taifa Mkomazi, Serengeti, Tarangire na Pori la Akiba Mkungunero. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya za Longido, Sikonge, Kilosa, Manyoni, Kiteto na Monduli imehakiki mipaka ya vitalu 14 vya uwindaji vyenye migogoro. Vilevile, Wizara imeendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi na viongozi wa vijiji vinavyozunguka maeneo yaliyohifadhiwa na umuhimu wa kuzingatia mipango ya matumizi bora ya ardhi.




54.         Mheshimiwa Spika, Pamoja na tatizo la mipaka, upo mgogoro mkubwa wa mifugo kuingizwa ndani ya hifadhi. Uvamizi huu unaofanyika

21


kwenye Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na Hifadhi za Taifa umekuwa ukiongezeka kwa kasi na unahusu zaidi uingizaji na ulishaji wa mifugo hususan ng’ombe, mbuzi, kondoo na punda pamoja na shughuli nyingine za kibinadamu. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Serengeti, Selous, Katavi, Ruaha, Mkungunero, Uwanda, Mkomazi, Ibanda, Rumanyika, Rungwa, Muhwesi, Muyowosi, Kigosi, Kizigo, Ikorongo, Kijereshi na Lukwati. Kuwepo kwa wananchi pamoja na mifugo katika maeneo hayo ni uvunjaji wa Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 (Sura ya 283). Wizara imekuwa ikishirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya na Mikoa pamoja na wadau wengine katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili. Aidha, Serikali imeagiza na kuwataka wananchi waliovamia maeneo yaliyohifadhiwa kuondoka.

vii.       Mpango Mkakati wa kuzuia Ujangili


55.         Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kutekeleza Mkakati wa Kupambana na Ujangili na Biashara haramu ya Nyara za Serikali ambao ulizinduliwa Novemba, 2014. Kazi zilizotekelezwa ni kuongeza idadi ya watumishi kwa ajili ya kufanya doria katika maeneo ya hifadhi ambapo jumla ya watumishi 558 (askari wanyamapori 447 na maafisa 111) wameajiriwa na kufanya idadi ya watumishi waliopo kwa sasa kuwa 2,064. Aidha, Wizara imeanzisha kanda nane za doria za ushirikiano katika mifumo ya ikolojia ya Selous – Niassa – Mikumi; Ruaha – Rungwa; Katavi – Rukwa; Moyowosi – Kigosi; Tarangire – Manyara – Simanjiro; na Ngorongoro - Serengeti.

56.           Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi iliwezesha upatikanaji wa vitendea kazi na zana kwa ajili ya doria. Vifaa hivyo ni magari 24, pikipiki 30, GPS 50, mahema 130, vifaa vya mawasiliano 50, genereta 50, ndege zisizo na rubani (UAV’s) na ndege ndogo mbili aina ya Husky. Vilevile, mafunzo ya kujenga uwezo wa kupambana na ujangili yametolewa kwa askari 53. Pia, chombo cha ushirikiano baina Wizara

22


na Taasisi mbalimbali (Multi Agency Task Team – MATT) kilizinduliwa tarehe 30 Juni, 2015. Chombo hiki kimetanua wigo wa kupambana na ujangili kwa kuhusisha vyombo vingine vya dola.

57.         Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Mamlaka itawekeza katika kuboresha miundombinu ndani ya Mapori ya Akiba na maeneo mengine yenye vivutio. Hatua hii itawezesha maeneo mengi zaidi kufikika hivyo kupanua wigo wa utalii wa picha kufuatia changamoto zinazokabili uwindaji wa kitalii pamoja na usafirishaji wa nyara.

58.         Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi, Mamlaka itafanya ukarabati wa nyumba 10 za watumishi na kukamilisha ujenzi wa nyumba 12 katika vituo vitano (KDU Tabora-1, Moyowosi/Kigosi-3, Ugalla-6, Burigi–1 na Ibanda-1). Aidha, Mamlaka itakamilisha upatikanaji wa eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya TAWA na Kanda zake. Aidha, Mamlaka itakarabati barabara zenye urefu wa kilometa 175 katika Mapori ya Akiba ya Mpanga/Kipengele-25, Ugalla-25, Lukwika-25, Lwafi-25, Rungwa-50 na Ibanda-25. Vilevile, Mamlaka itafyeka mipaka yenye urefu wa kilometa 150 katika Mapori ya Akiba ya Rungwa-50, Mkungunero -50 na Swagaswaga-50 pamoja na kuweka alama za kudumu ardhini (beacon) katika Pori la Akiba Swagaswaga.








viii.     Shirika la Hifadhi za Taifa


59.         Mheshimiwa Spika, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limeendelea na jukumu lake la msingi la usimamizi wa Hifadhi za Taifa 16, uhifadhi wa wanyamapori na kuendeleza shughuli za utalii. Katika kudhibiti ujangili, Shirika limeendesha siku za doria 178,301 ambazo ziliwezesha

23


kukamatwa kwa watuhumiwa 2,529. Aidha, Shirika limeendelea kushirikiana na Bodi ya Utalii kutangaza utalii nje na ndani ya nchi kwa kutoa maelezo na fafanuzi za kisayansi kuhusu vivutio vya utalii ndani ya hifadhi. Ushiriki wao umechangia kushawishi na hivyo kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi zetu. Shirika limeanzisha utalii wa kuangalia faru katika Hifadhi ya Taifa Serengeti, kuendesha baiskeli katika Hifadhi za Kilimanjaro na Arusha, kupanda kilele cha Mawenzi na kuruka katika Mlima Kilimanjaro (paragliding).

60.         Mheshimiwa Spika, ninayo furaha kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa, Shirika la Hifadhi za Taifa katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro lilipata tuzo ya Kimataifa ya kuwa kivutio bora cha utalii Barani Afrika (African leading Tourist Attraction). Tuzo hiyo ilitolewa na Taasisi ya “World Travel Award” ya nchini Uingereza. Tuzo hiyo itawezesha utalii wa Tanzania kutangazwa zaidi kupitia tovuti ya Taasisi hiyo ambayo inatembelewa na watalii wengi duniani.



61.         Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha miundombinu, Shirika limefanikiwa kujenga jumla nyumba 15 kwa ajili ya watumishi 29 katika hifadhi za Arusha (1), Gombe (1), Katavi (2), Kilimanjaro (2), Kitulo (2), Mahale (3), Mikumi (2), Rubondo (1) na Saadani (2). Ujenzi wa nyumba 10 kati ya 15 umekamilika. Vilevile, Shirika limekamilisha ujenzi wa ofisi ya Lango la Rongai katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, jengo la mapokezi katika uwanja wa ndege Seronera katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.

62.            Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Shirika limeboresha mfumo wa malipo wa ki-elektroniki kwa ajili ya wageni kulipa tozo mbalimbali wakati wa kuingia kwenye Hifadhi za Taifa na unatumika katika hifadhi zote. Mfumo huu umerahisisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuwarahisishia watalii kulipia huduma mbalimbali katika hifadhi. Aidha, Shirika limeimarisha miundombinu ndani ya Hifadhi za Taifa ili kuwezesha doria na utalii kufanyika
24


kwa ufanisi. Katika kutimiza azma hiyo, barabara zenye urefu wa kilometa 3,500 na viwanja vitano vya ndege vimekarabatiwa. Pia, Shirika limefunga mfumo wa kisasa wa mawasiliano ya kidigitali katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.

63.         Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya jamii na uwekezaji kwenye vijiji vinavyopakana na Hifadhi, Shirika lilitumia Sh. 1,103,714,719.00. Miradi iliyotekelezwa ambayo inahusu elimu, afya na maji ni ujenzi wa maktaba (2), maabara (5), madarasa (12), ofisi (9), mabweni (2), nyumba za walimu (3) na ununuzi wa madawati 425. Aidha, ujenzi nyumba tatu za wauguzi na zahanati mbili umefanyika. Vilevile, huduma za maji zilihusu kuchimba malambo mawili, mashine ya kusukuma maji kwa kutumia upepo (windmill) na kisima kirefu. Vikundi 20 vya wavuvi vilipewa taa za sola 200 na mifumo ya kuchajia 40.

64.         Mheshimiwa Spika, mwaka 2016/2017, Shirika litaendelea kudhibiti maambukizi ya magonjwa kati ya wanyama na mifugo pamoja na magonjwa kati ya binadamu na wanyamapori. Aidha, Shirika litakamilisha taratibu za kuunganisha eneo la Ghuba ya Speke kwenye Hifadhi ya Serengeti. Vilevile, Shirika litajenga kituo cha kutoa habari kwa wageni, nyumba 44 za watumishi na barabara mpya zenye urefu wa kilometa 75. Shirika litaimarisha miundo mbinu ya barabara zenye urefu wa kilometa 5,845 na viwanja vya ndege 17 katika hifadhi za Taifa. Pia, njia za miguu zenye urefu wa kilometa 534 zitaimarishwa kwenye Hifadhi za Taifa za Arusha, Udzungwa na Kilimanjaro.

65.         Mheshimiwa Spika, Shirika litaendesha siku za doria 196,421 katika Hifadhi za Taifa; kuimarisha shughuli za utendaji kazi za intelijensia kwa kutoa mafunzo na vitendea kazi kwa wahifadhi pamoja na kuimarisha uhusiano na wadau wengine wa uhifadhi na ulinzi wa wanyamapori. Vilevile, Shirika litaendelea kutangaza utalii ndani na nje ya nchi kwa kushiriki kwenye

25


maonesho ya kitaifa na kimataifa; kuendelea kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii; na kutangaza utalii mpya wa “Canopy walk” katika Hifadhi ya Manyara; utalii wa Faru katika Hifadhi ya Serengeti; na utalii wa “paragliding” katika Hifadhi ya Kilimanjaro. Vilevile, Shirika litaendelea kutangaza utalii wa kuendesha baiskeli katika hifadhi za Kilimanjaro na Arusha; utalii wa kupanda kilele cha Mawenzi na kufungua Kambi kwa utalii maalumu ndani ya kreta ya Kibo katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.


66.         Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha mfumo wa udhibiti mapato na matumizi, Shirika litanunua “software” ya ukaguzi na kutoa mafunzo ya jinsi ya kuitumia. Aidha, Shirika litakamilisha mapendekezo ya tozo kulingana na msimu wa utalii (low and high season) na yale ya kuwa na tozo moja (package fees) kwa shughuli za utalii.

67.         Mheshimiwa Spika, katika kujenga uwezo wa watumishi, Shirika litagharimia watumishi 14 kupata mafunzo ya muda mrefu na 40 muda mfupi. Aidha, Shirika litaajiri watumishi wapya 122 kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali. Katika kuwezesha Shirika kuingia kwenye mfumo wa mawasiliano ya kisasa, Shirika litaendelea kuboresha mfumo wa ki-eletroniki wa utoaji vibali (electronic permitting system) katika Hifadhi za Taifa ambao utawezesha miamala ya fedha kufanyika kwa njia ya mtandao (Electronic Banking). Vilevile, mfumo huu utawezesha wageni kufanya mawasiliano ya karibu baina ya wadau na menejimenti. Aidha, Shirika litaendelea kuimarisha mifumo ya taarifa za kijiografia katika vituo vyote kwa lengo la kurahisha ukusanyaji, utunzaji, uchambuzi na upatikanaji wa taarifa mbalimbali za kiikolojia.

68.         Mheshimiwa Spika, Shirika litaendelea kutoa elimu ya uhifadhi na kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na binadamu kwenye maeneo yanayopakana na Hifadhi za Taifa. Katika kuboresha mahusiano kati ya

26


Hifadhi na wananchi wanaozunguka Hifadhi, Shirika litaendelea kuwezesha vikundi 30 vya Benki ya vikundi vya jamii vya uhifadhi (Community Conservation Bank-COCOBA) katika maeneo yanayozunguka Hifadhi za Taifa za Rubondo, Tarangire na Udzungwa. Shirika litalipia vipindi 36 vya redio na 36 vya televisheni kuhusu uhifadhi na utalii pamoja na kuandaa na kusambaza nakala 2,000 za jarida la Shirika “TANAPA Today” linalochapishwa kila robo mwaka.

ix.         Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro


69.         Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha miundombinu, Mamlaka imekarabati kilometa 326 za barabara ndani ya hifadhi na nyumba mbili za askari. Aidha, ilinunua magari saba ya doria na kutangaza zabuni za ujenzi wa ofisi kwa ajili ya uwanja wa ndege wa Ndutu ndani ya Hifadhi hiyo. Katika kuimarisha huduma za jamii ya wafugaji, Mamlaka imetekeleza mradi wa kuboresha mifugo na kukamilisha mradi wa kijiji cha Jema walikohamishiwa wafugaji waliotolewa ndani ya hifadhi na kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro. Aidha, Mamlaka imenunua magunia 22,000 na kupokea magunia 20,000 ya mahindi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo yalisambazwa kwa jamii inayoishi ndani ya Hifadhi.

70.         Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kukabiliana na tatizo la ujangili na kuongeza ufanisi katika ulinzi wa Wanyamapori, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuimarisha shughuli za uhifadhi kwa kuendesha siku-doria 39,600 ndani ya eneo na katika maeneo yanayozunguka hifadhi. Doria hizo ziliwezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 33, kati ya hao watuhumiwa 30 walitozwa faini na watatu kesi zao zinaendelea.

71.         Mheshimiwa Spika, Katika kuepuka utegemezi wa kipato kutokana na shughuli za utalii pekee ambazo huathirika mara nyingi kutegemea hali ya soko la utalii duniani, Mamlaka inaendelea kujenga Kitega
27


Uchumi jijini Arusha. Ujenzi wa jengo hilo lenye ghorofa 17, umefikia asilimia 80 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Novemba, 2016.

72. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Mamlaka itaendelea na shughuli za uhifadhi wanyamapori na malikale; kuhudumia jamii ya wafugaji na kuendeleza shughuli za utalii. Katika kutekeleza jukumu hilo, Mamlaka itatoa chanjo za homa ya mapafu na sotoka kwa ng’ombe 130,000 na mbuzi na kondoo 230,000 walio ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. Katika kuboresha miundombinu, Mamlaka itajenga bwawa la maji la Olekule, Kata ya Aleilelai, kuchimba kisima cha maji eneo la Naibarta - Endulen, kukarabati barabara yenye urefu wa kilometa 72, kuhakiki mpaka wa eneo la hifadhi katika maeneo ya Endamagha, Lositete, Malambo na Piyaya pamoja na kujenga vituo vitatu vya Askari.

x.           Vyuo vya Taaluma ya Wanyamapori


73.         Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/2016, Chuo cha Usimamizi na Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka (College of African Wildlife Management Mweka – CAWM) kimedahili wanafunzi 578. Chuo kimenunua magari mawili kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi. Aidha, Chuo kimekarabati mabweni, bwalo la chakula, jengo la Utawala na kutengeneza barabara ndogo za ndani. Vilevile, chuo kimekarabati sehemu ya kuegeshea magari pamoja na kujenga nyumba moja ya wafanyakazi katika eneo la Kwakuchinja. Aidha, Kituo cha Elimu kwa Jamii Likuyu-Sekamaganga kilitoa mafunzo ya uhifadhi shirikishi kwa watumishi 91 kutoka Halmashauri za Wilaya za Kibondo, Kakonko, Buhingwe, Uvinza, Kasulu na Mkuranga katika Mikoa ya Kigoma na Pwani.

74.         Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Mafunzo ya Wanyamapori Pasiansi imedahili wanafunzi 441, kati ya hao, 90 ni wa kozi ya Astashahada ya Uhifadhi na Ulinzi wa Wanyamapori na 351 ni Astashahada ya Awali ya

28


Uhifadhi na Ulinzi wa Wanyamapori; wanawake wakiwa ni 93 na wanaume 348. Aidha, Taasisi kwa msaada wa wadau imenunua mabasi mawili, malori mawili, gari dogo moja na kujenga kambi ya mafunzo kwa vitendo katika eneo la Fort Ikoma, Serengeti.


75.         Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Vyuo vya mafunzo ya taaluma ya wanyamapori vitadahili jumla ya wanafunzi 1,136. Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori - Mweka kitadahili wanafunzi 736 na Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi 400. Aidha, Kituo cha Elimu kwa Jamii – Likuyu Sekamaganga kitaendelea kutoa elimu ya uhifadhi wanyamapori kwa viongozi na askari wa vijiji.

76.         Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha miundombinu na vitendea kazi, Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kitanunua gari kwa ajili ya mafunzo porini; kujenga madarasa mawili; kujenga nyumba mbili za watumishi na kuweka umeme kwenye eneo la mafunzo la Kwakuchinja. Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi kitakarabati nyumba tano za watumishi, bwalo la chakula na mfumo wa maji safi.








xi.         Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)


77.         Mheshimiwa Spika, Taasisi ina jukumu la kusimamia na kufanya utafiti katika maeneo yanayohusu wanyamapori na ikolojia wanapoishi nchini. Katika kutekeleza majukumu yake, Taasisi imeendeleza utafiti wa magonjwa ya wanyamapori, magonjwa ya maambukizo baina ya binadamu, wanyamapori na mifugo. Pia, inatekeleza miradi ya utafiti wa ikolojia na uwezo wa hifadhi kuhimili idadi mbalimbali za wanyamapori kulingana na mahitaji yao. Aidha,
29


Taasisi imeendelea kusimamia miradi mikubwa miwili ambayo ni mradi wa kuboresha ufugaji nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa na mradi wa uhifadhi wa mbwa mwitu katika ikolojia ya Serengeti.

78.         Mheshimiwa Spika, Taasisi imekamilisha utafiti kuhusu ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa (Rift Valley Fever, RVF) ambao umekuwa ukitokea nchini kila baada ya miaka 10 hadi 15. Lengo la mradi lilikuwa ni kutambua kirusi kinachosababisha ugonjwa huo, chanzo cha ugonjwa na chanzo hicho hujificha wapi wakati ambapo hakuna mlipuko. Utafiti huu umeonesha kuwa kirusi cha ugonjwa wa RVF kinatunzwa kwa kiwango cha chini kwenye (i) mbu jamii ya Aedes na Culex- asilimia 2.7 (ii) wanyama wafugwao ng’ombe asilimia 5.7, kondoo 5.7 na mbuzi 1.9 na (iii) wanyamapori wastani wa asilimia 14.6 (nyati, nyumbu, kongoni, swala tomi, swala granti na nyemela). Mifugo na wanyamapori waliozaliwa mwaka mmoja hadi minne baada ya mlipuko wa mwisho wa 2006/2007 walionekana wameambukizwa na kirusi, ambayo inadhihirisha kuwa maambukizi mapya huwa yanaendelea wakati ambao hakuna mlipuko wa ugonjwa. Mradi umehitimisha kuwa chanzo cha mlipuko wa ugonjwa ni pale mazingira yanayowezesha mbu kuzaliana kwa wingi yanapokuwepo, hasa wakati wa mvua nyingi na mafuriko.

79.         Mheshimiwa Spika, katika kuboresha ufugaji nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa, Taasisi imetengeneza na kusambaza mizinga 1,200 kwa wadau mbalimbali ikiwemo Wakala wa Huduma za Misitu-Kanda ya Kasikazini; Muungano wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA)-Arusha; Umoja Group-Arusha; na Halmashauri ya Wilaya ya Siha-Kilimanjaro. Matumizi ya mizinga na vifaa vya kisasa yatasaidia kuongeza na kuboresha uzalishaji wa mazao ya nyuki.

80.         Mheshimiwa Spika, Taasisi inasimamia mradi wa uhifadhi wa mbwa mwitu katika ikolojia ya Serengeti ambao wapo katika hatari ya kutoweka duniani. Mradi huo una makundi 27 yenye zaidi ya mbwa mwitu

30


300 ambao mienendo na mitawanyiko yao inafuatiliwa kwa kutumia vifaa vya kisasa vya mawasiliano ya satelaiti (GPS satellite collars). Ufuatiliaji umeonesha kuwa mbwa mwitu hao wametawanyika katika ikolojia ya Serengeti inayojumuisha Hifadhi ya Taifa Serengeti, Hifadhi ya Ngorongoro, Mapori ya Akiba ya Maswa, Ikorongo Grumeti na maeneo ya wazi ya Ziwa Eyasi, Makao na Pori Tengefu Loliondo.

81.         Mheshimiwa Spika, katika kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mbwa mwitu katika maeneo ya mradi, TAWIRI imeendelea kusambaza vipeperushi, kalenda na fulana zenye ujumbe mahususi unaolenga kuokoa kizazi cha mbwa mwitu ambao ni miongoni mwa wanyamapori ambao ni kivutio kikubwa cha utalii.


82.         Mheshimiwa Spika, mwaka 2016/2017, Taasisi itafanya sensa za wanyamapori katika sehemu mbalimbali ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa. Maeneo hayo ni pamoja na mfumo ikolojia wa Serengeti. Aidha, Taasisi itafanya sensa ya mamba na viboko nchi nzima. Vilevile, itaendeleza utafiti wa mbwa mwitu katika mfumo-ikolojia wa Serengeti na kuendelea kuhamasisha jamii kuwalinda na kuwahifadhi wanyama hao wasitoweke.

83.         Mheshimiwa Spika, Taasisi itaendeleza tafiti za mwenendo wa magonjwa ya wanyamapori hasa homa ya bonde la ufa, kaswende ya nyani, ugonjwa wa miguu na midomo, homa ya vipindi na magonjwa yanayoambukiza binadamu na wanyamapori kutokana na kula nyamapori. Aidha, Taasisi itaendelea na majaribio ya matumizi ya ndege zisizo na rubani katika kuzuia tembo waharibifu wa mazao katika mifumo ikolojia ya Tarangire-Manyara na Serengeti ili kupunguza mgongano kati ya tembo na Binadamu. Vilevile, utafiti utafanyika kuhusu mfumo ikolojia wa Serengeti unavyofanya kazi na manufaa yake kwa jamii.


31


84.         Mheshimiwa Spika, Taasisi itaendelea kufanya utafiti kuhusu mahusiano kati ya nyuki na mimea katika kanda zote za Tanzania Bara. Utafiti huo unatarajiwa kuwezesha uchoraji wa ramani kulingana na aina za mimea, nyuki, asali na chavua katika maeneo husika. Aidha, utafiti wa wadudu na vimelea wanaoshambulia nyuki katika mikoa 11 ya Tanzania Bara utafanyika.

85.         Mheshimiwa Spika, Taasisi itaendelea kuwajengea uwezo watafiti na watumishi wengine wa Taasisi kwa kuwaendeleza kimasomo katika ngazi mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kitaaluma na kuleta tija katika Taasisi. Aidha, itatengeneza na kusambaza mizinga 1,500 kwa wadau wa sekta ya ufugaji nyuki. Vilevile, Taasisi itakamilisha ujenzi wa jengo la maabara ya kisasa ya utafiti wa nyuki pamoja na mazao yake.

xii.       Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania


86.         Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania (Tanzania Wildlife Protection Fund, TWPF) ulianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 21 ya mwaka 1978 baada ya kukifanyia marekebisho kifungu cha 69 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 12 ya mwaka 1974. Marekebisho hayo yalitangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 21 la tarehe 22 Mei, 1981. Mfuko ulianzishwa kwa lengo la kuwezesha mapambano dhidi ujangili, kugharimia tafiti za wanyamapori, kusaidia maendeleo ya wananchi wanaopakana na hifadhi za wanyamapori na kutoa elimu ya uhifadhi kwa umma kupitia MALIHAI clubs. Katika mwaka 2015/2016, Mfuko ulikadiria kukusanya shilingi 16,980,000,000 Hadi kufikia Aprili 2016 shilingi 13,471,369,031.25 zilikusanywa sawa na asilimia 79.34 ya lengo. Fedha hizo zimetumika kugharamia kazi za uhifadhi wa Wanyamapori, utafiti na mafunzo, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ndani ya Mapori ya Akiba na Uendeshaji wa Vyuo na Taasisi za Wanyamapori. Aidha, Mfuko umegharamia miradi mitano ya jamii katika Wilaya za Wanging’ombe, Kondoa, Ilembula na Singida. Miradi hiyo ni Uchimbaji wa Kisima katika kijiji cha Mayale, kuchangia ujenzi wa ofisi

32


ya kata ya Wanging’ombe, Zahanati katika kata ya Kwadelo na Kituo cha Afya katika kijiji cha Pohamba. Vilevile, Mfuko umegharamia ununuzi wa vitanda 91 vya bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari ya Ilembula.

b.   Sekta Ndogo ya Misitu na Nyuki

87.         Mheshimiwa Spika, Idara ya Misitu na Nyuki imekasimisha baadhi ya shughuli zake kwa Wakala wa Huduma za Misitu. Kwa sasa Idara inashughulika na: kuendeleza, kufuatilia, kutathmini na kufanya marejeo ya Sera, Sheria na Mikakati ya Misitu na Nyuki; kufuatilia maendeleo ya taasisi za mafunzo ya misitu na ufugaji nyuki zilizo chini ya Wizara; na kuwezesha msaada wa kitaalamu na kufuatilia utekelezaji wa shughuli za misitu na ufugaji nyuki katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs). Kazi nyingine ni kuratibu uanzishaji wa hifadhi za misitu na nyuki; kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa huduma za ugani; na kuainisha maeneo na kuwezesha utafiti wa misitu na nyuki.

i.             Sera na Sheria


88.         Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha uhifadhi wa misitu na kuendeleza ufugaji nyuki nchini, Wizara yangu imeendelea kuboresha Sera za Misitu na Nyuki za mwaka 1998. Maboresho hayo yanazingatia mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kimazingira yanayotokea ndani na nje ya nchi. Aidha, Wizara imeandaa rasimu ya Programu mpya ya Misitu na Nyuki ya kipindi cha 2016-2021.

89.         Mheshimiwa Spika, Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998, pamoja na mambo mengine, imesisitiza ushiriki wa wananchi katika upandaji na usimamizi wa misitu ili kuongeza upatikanaji wa mazao ya misitu. Ili kufanikisha suala hili, Wizara imeanzisha Programu ya Panda Miti Kibiashara katika Mikoa ya Njombe, Iringa, Ruvuma na Morogoro. Mikoa hii imechaguliwa

33


kwa sababu ya kuwa na maeneo ya kutosha kuwezesha kilimo cha miti; hali nzuri ya hewa kwa ajili ya kilimo cha miti; utayari wa wananchi na ushiriki wao katika shughuli za upandaji miti kibiashara. Mpaka sasa vikundi 50 vyenye wanachama 2,351 vimeundwa. Programu hii imewezesha wananchi kupanda zaidi ya hekta 3,000 zenye miche bora ya miti.


90. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Wizara itakamilisha na kusambaza kwa wadau nakala 5,000 za Sera Mpya ya Misitu na mkakati wake wa utekelezaji. Vilevile, itakamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki. Aidha, Wizara itawasilisha Bungeni muswada wa marekebisho ya Sheria ya Misitu Namba 14 ya mwaka 2002 ili kukidhi mahitaji ya uendelezaji wa sekta ndogo ya Misitu na Ufugaji Nyuki.

ii.           Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania



91.         Mheshimiwa Spika, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Services Agency - TFS) ulianzishwa kwa mujibu wa Sheria na kutangazwa katika Tangazo la Serikali Na. 269 la tarehe 30 Julai, 2010. Kiutendaji, Wakala unatekeleza majukumu yaliyokuwa ya Idara ya Misitu na Nyuki isipokuwa utungaji wa sera, sheria na programu za misitu na nyuki.

92.         Mheshimiwa Spika, Wakala unasimamia misitu ya hifadhi ya asili (Forest Reserves) 506 yenye hekta 15.48 milioni iliyotawanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Wakala pia unasimamia misitu iliyotengwa kama Hifadhi za Mazingira Asilia (Forest Nature Reserves) 11 zenye jumla ya hekta 233,837. Hifadhi hizo zipo katika mikoa ya: Tanga (Amani, Nilo na Magamba); Morogoro - (Uluguru na Mkingu); Morogoro na Iringa (Kilombero); Mbeya (Mlima Rungwe); Kilimanjaro (Chome); Iringa (Udzungwa Scarp); Kagera (Minziro) na Lindi (Rondo Plateau). Vilevile, Wakala unasimamia Misitu ya Hifadhi Lindimaji (catchment forests) yenye jumla ya hekta milioni 1.4. Aidha,

34


katika ukanda wa pwani kuna jumla ya hekta 115,000 za misitu ya mikoko iliyopo katika mikoa ya Tanga, Pwani, Dar-es-Salaam, Lindi na Mtwara. Vilevile, Wakala unasimamia mashamba 18 ya miti ya kupandwa yaliyoko katika mikoa 12 nchini.

Usimamizi wa Rasilimali za Misitu


93.         Mheshimiwa Spika, katika kudhibiti uvunaji haramu na biashara ya mazao ya misitu, jumla ya doria siku 22,693 ziliendeshwa katika maeneo ya hifadhi za misitu, ardhi huria, hifadhi za nyuki, maeneo ya uvunaji, usafirishaji na masoko. Kupitia doria hizo, vipande 110,307 vya mbao, mkaa magunia 105,324 silipa 5,399 na shata za milango 391 vilikamatwa na kuuzwa. Aidha, watuhumiwa 281 walikamatwa na kesi 22 zilifunguliwa mahakamani na zipo katika hatua mbalimbali; kambi za mkaa 29 na matanuru 858 ya kutengeneza mkaa yaliharibiwa. Wafugaji wenye ng’ombe 3,997 walitozwa faini ambapo kiasi shilingi 1,357,115,380 zilikusanywa kutokana na faini na mauzo ya mazao yaliyokamatwa. Aidha, Wakala iliendesha kesi za jinai 34 zilizopo mahakamani kutokana na makosa ya uvunjaji wa sheria ya Misitu. Kesi tano zimeisha na watuhumiwa saba wamehukumiwa kifungo cha miaka saba jela.

94.         Mheshimiwa Spika, Ukaguzi katika vizuia 72 vya Kanda saba za Wakala ulifanyika ili kubaini kama sheria na taratibu za kusafirisha mazao ya misitu zinazingatiwa. Jumla ya magari 5,234 yalikaguliwa katika vizuia vilivyopo Kanda ya Kati, Ziwa na Magharibi. Magari 361 yalikiuka sheria na kanuni za kusafirisha mazao ya misitu. Mazao yaliyotaifishwa kwenye vizuia vya Kanda ya Ziwa na Kati ni pamoja na magunia 7,517 ya mkaa, vipande 236 vya mbao, nguzo 53, vitanda tisa, milango tisa na kuni mita za ujazo 44.8. Aidha, vizuia sita vipya vilianzishwa katika Kanda ya Kati na Nyanda za juu




35


Kusini ili kuimarisha utekelezaji wa Sheria ya Misitu namba 14 ya mwaka 2002.


95.         Mheshimiwa Spika, Watumishi 288 wa Wakala kutoka katika kanda tatu za kaskazini, Kusini na Nyanda za juu kusini wamepatiwa mafunzo ya kuendesha kesi, kuielewa sheria na kanuni za Misitu na ufugaji nyuki. Vilevile, Wakala ilitoa mafunzo kuhusu taratibu za kufanya biashara ya mazao ya misitu kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu kwa wafanya biashara 1,125 kutoka katika Kanda za Kati, Mashariki na Ziwa.


96.         Mheshimiwa Spika, Wakala umeandaa mipango ya uvunaji katika Wilaya tano za Kilosa, Kibaha, Ulanga, Kisarawe na Kilombero. Aidha, Kamati za Uvunaji katika Wilaya 16 ziliwezeshwa kufanya mikutano ya kupitisha maombi ya wavunaji na kudhibiti uvunaji haramu wa mazao ya misitu. Pia, Wakala umeandaa rasimu ya mipango ya usimamizi katika misitu ya Korogwe na Vugiri (Tanga), North Ruvu (Pwani) na Essmingor (Arusha) na kufanya mapitio ya mipango ya misitu ya Kindoroko (Kilimanjaro) na Rondo (Lindi).


97.         Mheshimiwa Spika, Wakala umeendelea kutekeleza Mpango Mkakati wa Misitu 2014-2019. Moja ya mikakati iliyomo kwenye mpango huo ni kupanda jumla hekta 185,000 za miti kwa mwaka kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na wadau wengine. Lengo ni kuongeza uzalishaji wa miti ili kuziba pengo la mita za ujazo 19.5 milioni kwa mwaka za timbao hadi kufikia mwaka 2030.

98.         Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Wakala utaendesha siku za doria 33,264 katika maeneo ya hifadhi za misitu, maeneo ya uvunaji, usafirishaji na kudhibiti biashara ya mazao ya misitu katika kanda saba. Aidha, Wakala utawezesha Kamati za Uvunaji za Wilaya 46 kufanya


36


mikutano ya kupitisha maombi ya uvunaji. Aidha, Wakala utaandaa mipango ya uvunaji mazao ya misitu katika Wilaya 11 kwenye maeneo ya ardhi huria.

99. Mheshimiwa Spika, katika kutatua changamoto za uvamizi, misitu ya hifadhi 20 yenye migogoro itashughulikiwa. Vilevile, Wakala utatekeleza makubaliano ya pamoja ya kudhibiti biashara haramu ya mazao ya misitu kati ya nchi jirani za Msumbiji, Zambia na Kenya kwa kufanya vikao na doria za pamoja. Katika kutatua changamoto za uhifadhi na usimamizi wa hifadhi za misitu, Wakala utatekeleza makubaliano yaliyoridhiwa kati yake na TAMISEMI na kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara 1,650 wa mazao ya misitu katika Kanda tatu za Kati, Ziwa na Mashariki.

Kuimarisha Mipaka na Usimamizi wa Misitu ya Hifadhi


100.      Mheshimiwa Spika, Wakala umeondoa wananchi waliovamia misitu ya hifadhi 17 kwa ajili ya shughuli za kilimo, ufugaji na makazi. Hali hiyo imesababisha uharibifu wa uoto wa asili, vyanzo vya maji na bioanuwai hivyo kusababisha athari za ardhi kuwa jangwa. Hatua hiyo imechukuliwa kwa kuzingatia Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 Kifungu cha 26 ambacho kinakataza uvamizi wa maeneo ya misitu yaliyohifadhiwa. Aidha, Wakala umefanya mapitio ya soroveya kilometa 510.14; kusafisha mipaka ya misitu ya hifadhi 126 yenye urefu wa kilometa 1,927.42; na kuweka maboya 972; mabango 2,075; na mashimo ya mwelekeo 228 ili kutoa tahadhari kwa jamii kuhusu maeneo yaliyohifadhiwa. Kazi nyingine zilizofanyika ni kukuza miche 4,773,317 na kupanda kwenye mipaka yenye urefu wa kilomita 40; kurudishia maeneo ya misitu yenye hekta 259.8 ya misitu ya hifadhi 11 na hekta 34.8 za hifadhi ya misitu ya mikoko iliyoharibiwa.

101.      Mheshimiwa Spika, tathmini ya rasilimali za Misitu katika msitu wa Hifadhi Mangaliza – Mpwapwa inaendelea na itakamilika katika mwaka wa fedha 2016/17. Rejea zilifanyika kwa kungano (clusters) 213 katika Kanda ya

37


Magharibi na Nyanda za Juu Kusini kwa lengo la kujua rasilimali za misitu zilizopo ili kuandaa mipango ya usimamizi. Aidha, Wakala umehakiki, kuhuisha na kuweka katika mfumo wa kidijitali ramani za misitu ya asili 26 na misitu ya hifadhi za mazingira asilia mitatu.

102. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Wakala utaendelea kusimamia hifadhi za misitu kwa kuondoa wavamizi katika misitu ya hifadhi 27; kufanya mapitio ya soroveya ya kilomita 227,251 za misitu; kusafisha mipaka ya misitu ya hifadhi 98 yenye urefu wa kilomita 2,816; kupanda miche kwenye mipaka ya misitu kilomita 167; kuweka maboya 1,290 na mabango 541 ili kutahadharisha jamii kuhusu maeneo yaliyohifadhiwa. Vilevile, Wakala utaongoa maeneo yaliyoharibiwa kwa kuotesha miti ya asili katika eneo lenye ukubwa wa hekta 2,041 na kupanda mikoko kwenye eneo la hekta tisa za hifadhi. Hali kadhalika, tathmini itafanyika katika misitu ya Ijogo na Mlali; uhakiki na kuhuisha ramani za misitu ya asili 50 na mashamba 18; na kuchora ramani ya misitu 15 na hifadhi za nyuki tano.


Uendelezaji wa vivutio vya Utalii ikolojia



103.      Mheshimiwa Spika, Wakala uliboresha vivutio vya utalii ikolojia katika misitu ya hifadhi za mazingira asilia kwa kusafisha barabara zenye urefu wa kilometa 34.5; njia vinjari kilometa 68.9; na kambi 17 za kupumzikia wageni katika misitu mitano ya Hifadhi za mazingira asilia za Amani, Nilo, Uluguru, Kilombero na Mkingu. Aidha, ujenzi wa mageti 11 ya kuingia katika misitu ya hifadhi ya mazingira asilia umefanyika. Taratibu za kupandisha hadhi msitu wa Hifadhi wa Hanang kuwa hifadhi ya mazingira asilia zinaendelea.

104.      Mheshimiwa Spika, Misitu ya Mifadhi za Mazingira Asilia na Misitu ya Hifadhi zimekuwa zikipata watalii toka ndani na nje ya nchi. Mwaka

38


2015/2016, watalii 3,800 walitembelea hifadhi za mazingira asilia. Kati ya hao, watalii 2,628 waliotoka nje ya nchi na 1,172 ni watalii wa ndani. Maeneo yaliyotembelewa katika Misitu ya hifadhi za mazingira asilia ni Mount Rungwe, Kilombero, Mkingu, Uluguru, Amani, Nilo, Magamba na Chome pamoja na misitu ya hifadhi ya Duluti na Milima ya Udzungwa.

105.      Mheshimiwa Spika, mwaka 2016/2017, Wakala kwa kushirikiana na wadau utaboresha na kuendeleza vivutio vya utalii ikolojia kwa kutunza na kuimarisha miundombinu katika hifadhi za misitu ya mazingira asilia. Uboreshaji huu utahusisha kutengeneza njia za kuvinjari zenye urefu wa kilometa 110; vituo vinne vya kuangalia mandhari; na kambi tano za kumpumzikia wageni katika hifadhi za misitu na misitu ya mazingira asilia. Misitu itakayohusika ni pamoja na Vikindu, Pugu/Kazimzumbwi, Kimboza, Mbeya Range, Kalambo, Pindiro, Rondo, Mkingu, Uluguru, Kilombero, Mlima Hanang, Nilo na Chome.

106.      Mheshimiwa Spika, Wakala utaendelea kusimamia manzuki 90 zilizopo katika Kanda na mashamba ya miti na kuzalisha asali tani 17 na tani mbili za nta. Ili kuzalisha mazao bora ya nyuki, elimu itatolewa kwa wadau wa ufugaji nyuki 190 wakiwemo wafugaji nyuki, wafungashaji na wafanyabiashara kutoka katika Kanda za Kati na Ziwa. Sampuli 70 za asali zitakusanywa kutoka katika wilaya 25 kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi wa kimaabara ili kujua ubora wa asali inayozalishwa na kutimiza masharti ya kuuza asali katika masoko ya nje. Vilevile, Wakala utatoa mafunzo ya kutengeneza mizinga kwa wafugaji nyuki 580 na mafundi 44 kutoka katika Wilaya nane za Geita, Biharamulo, Musoma, Bukombe, Chato, Mbogwe, Magu na Misenyi. Aidha, Wakala utawezesha Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania (TABEDO) kuendesha shughuli zake.


Uendelezaji na Usimamizi wa Mashamba ya Miti


39




107.      Mheshimiwa Spika, Wakala imeotesha miche ya miti 17,899,266, na kupanda kwenye mashamba yenye ukubwa wa jumla ya hekta 12,277 kwa mwaka 2015/2016. Maeneo yaliyopandwa ni pamoja na hekta 2,792 mashamba mapya, hekta 4,979 maeneo ya mashamba ya zamani na hekta 6,060 maeneo ambayo miti haikuota. Vilevile, mashamba yenye ukubwa wa hekta 28,882 yalipaliliwa, kuondoa matawi ya miti (kupogolea) kwenye eneo la hekta 7,901 na kupunguza miti katika eneo la hekta 659.7. Wakala umeongeza hekta 5,000 za Shamba la miti Wino kutoka katika eneo la kijiji cha Mkongotema na kuandaa Mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji hicho. Wakala pia umekarabati barabara za msituni zenye urefu wa kilomita 1,324.5 na kujenga kilomita 100.

108.      Mheshimiwa Spika, Wakala ulifanya doria katika eneo lenye ukubwa wa hekta 281,350.4 katika mashamba ya miti, kusafisha kilometa 2,205; kuweka maboya 45 kwenye mipaka katika Shamba la Miti Ruvu kaskazini na kutunza minara 17 katika Shamba la Miti Sao Hill. Ukaguzi wa miti yenye mita za ujazo 611,355 ulifanyika katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uvunaji. Kampeni 42 za uhamasishaji wa madhara ya moto kwenye misitu zilitolewa kwa vijiji 40 vinavyozunguka mashamba manne ya miti ya Kawetire, Longuza, Ruvu Kaskazini na Ukaguru.

109.      Mheshimiwa Spika, katika kuhifadhi vyanzo vya maji vilivyoko katika mashamba ya miti, mimea ya kigeni iling’olewa na kupanda miti ya asili. Kazi hiyo ilifanyika kwenye eneo la hekta 147 katika Shamba la Miti Sao Hill na hekta 20 Shamba la Miti Kawetire. Katika mashamba ya West Kilimanjaro na Kawetire Mapitio ya mipaka na kugawanya viunga yalifanyika kwenye eneo la hekta 11,015. Vilevile, rasimu ya mipango ya usimamizi ya mashamba mawili ya Ruvu Kaskazini na Korogwe ilitayarishwa.



40


110.      Mheshimiwa Spika, mazingira ya kazi kwa watumishi yameboreshwa ikiwa ni pamoja na kukarabati nyumba 44 na kuendeleza ujenzi wa nyumba 13 katika mashamba ya Sao Hill, Rubare, Mtibwa, Wino na Mbizi. Aidha, Wakala umekarabati mifumo 11 ya usambazaji wa maji safi katika mashamba saba ya miti na ofisi nne katika Kanda za Mashariki na Ziwa. Ujenzi wa ofisi nne katika Kanda ya Kusini, Nyanda za Juu Kusini, Shamba la Miti Wino na Mbizi unaendelea.

111.      Mheshimiwa Spika, Wakala umenunua na kusambaza kwenye vituo vyake vitendea kazi kwa ajili ya kuboresha na kuongeza ufanisi wa kazi. Vifaa vilivyonunuliwa ni pamoja na magari 20, mahema 65 na GPS 25. Vilevile, Wakala ulipata msaada wa jenereta 25, telescope 15 na mtambo mmoja wa kutengenezea barabara. Aidha, Wakala uligharimia mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 60 na mfupi kwa watumishi 125.


112.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Wakala utaotesha miche ya miti 14,470,000, katika mashamba ya miti 18, kuandaa mashamba ya kupanda miti hekta 7,822 na kupanda miche ya miti kwenye mashamba mapya yenye ukubwa wa hekta 4,995. Pia utapanda miche ya miti kwenye hekta 3,393 katika mashamba yaliyovunwa na hekta 2,492 katika maeneo ambayo miti haikuota. Aidha, Wakala utapalilia eneo la shamba lenye ukubwa wa hekta 32,191, kupunguzia matawi ya miti kwenye eneo lenye ukubwa wa hekta 8,757 na kupunguza miti kwenye eneo la shamba lenye ukubwa wa hekta 1,706. Kazi nyingine zitakazofanyika ni kusafisha/kukarabati barabara za msituni zenye urefu wa kilomita 1,434 na kutengeneza zenye urefu wa kilomita 116. Vilevile, nyumba 63 na mifumo ya maji itakarabatiwa na nyingine mpya 13 zitajengwa. Wakala utaongeza mashamba mawili mapya ya miti katika Kanda za Mashariki na Kusini.





41


113. Mheshimiwa Spika, Wakala utaotesha miche ya miti 14,470,000; kutayarisha hekta 8,388 na kupanda hekta 4,995 katika maeneo mapya, hekta 3,393 katika maeneo yaliyovunwa na hekta 2,492 katika maeneo ambayo miti haikuota. Aidha, Wakala utapalilia eneo la shamba lenye ukubwa wa hekta 32,191; kupogoa hekta 8,757; na kupunguza miti katika hekta 1,706. Kazi nyingine zitakazofanyika ni kusafisha na kukarabati barabara zenye urefu wa kilometa 1,434 kwenye mashamba na kutengeneza nyingine zenye urefu wa kilometa 116. Vilevile, nyumba 13 za watumishi zitajengwa pamoja na kukarabati nyumba 63 na mifumo ya maji. Wakala utaongeza mashamba mawili mapya ya miti katika Kanda za Mashariki na Kusini.

114. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Wakala utasimamia uvunaji wa miti yenye mita za ujazo 754,931, kuni zenye mita za ujazo 24,462 na nguzo zenye mita za ujazo 9,800 katika mashamba ya miti. Aidha, usimamizi na ulinzi wa mashamba ya miti utafanyika kwa kufanya doria, kusafisha njia za moto zenye urefu wa mita 5,167 na kusafisha mipaka yenye urefu wa kilometa 1,063. Wakala utapanda miti ya asili kwenye eneo la hekta 789 kwenye vyanzo vya maji na mabonde baada ya kung’oa miti ya kigeni yenye athari iliyomea kwenye vyanzo vya maeneo hayo. Pia, Wakala utatenga upya viunga kwenye mashamba ya miti yenye ukubwa wa hekta 30,805.




Elimu kwa Umma


115. Mheshimiwa Spika, elimu kwa umma ilitolewa kupitia vipindi 75 vya redio; vinne vya televisheni; maonesho ya Sabasaba na Nanenane; na siku ya kupanda miti kitaifa. Vilevile, kampeni za kuzuia moto zilifanyika kwa viongozi wa vijiji 93 vinavyozunguka hifadhi 23 za misitu na kamati 12 za maliasili za vijiji. Aidha, katika vijiji hivyo, Wakala uliwezesha kuanzishwa kwa kamati 18 za Maliasili za vijiji. Ili kuhamasisha upandaji miti, Wakala


42


uliwezesha vikundi 150, vijiji 30, taasisi 105 na watu binafsi 21 kuotesha jumla ya miche 4,548,853.

116.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Wakala utatoa elimu ya usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za misitu na ufugaji nyuki kwa umma kwa kutayarisha na kurusha vipindi 48 vya redio, 14 vya televisheni na maonesho ya video 35. Njia nyingine ni kupitia maonesho ya Sabasaba, Nanenane, Siku ya Kupanda Miti, Kutundika Mizinga na Siku ya Mazingira Kitaifa. Katika juhudi za kutatua changamoto ya moto wa msituni, kampeni na elimu ya jinsi ya kupambana na moto itatolewa kwa watumishi na wananchi katika vijiji 284 vinavyozunguka misitu ya asili na mashamba.

117.      Mheshimiwa Spika, Wakala kwa kushirikiana na wadau mbalimbali utatoa elimu na kuhamasisha uzalishaji na matumizi bora ya mkaa; kuhimiza matumizi ya nishati mbadala na majiko banifu ili kupunguza matumizi ya nishati itokanayo na miti; kusaidia wachoma mkaa kuunda vikundi vya kuchoma mkaa; na kuanzisha magulio ya kuuzia mkaa. Aidha, Wakala utahamasisha na kuwajulisha wadau kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Usimamizi na Uhifadhi wa Misitu na kuwashirikisha kupanda miti ili kukidhi lengo la kuziba pengo la mita za ujazo 19.5 milioni ifikapo mwaka 2030.

Kuendeleza Ufugaji Nyuki


118. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza ufugaji nyuki Wakala umesimamia manzuki 88 zenye jumla ya mizinga 6,214; na kuanzisha manzuki tano mpya zenye mizinga 116. Vilevile, Wakala umetoa elimu kwa Wafugaji Nyuki 300, vikundi 11, wafungashaji na wafanyabiashara ya asali 105. Aidha, katika kuhakiki ubora wa asali inayozalishwa nchini, sampuli 84 za asali zilikusanywa na kufanyiwa uchambuzi wa kimaabara. Matokeo yanaonesha kuwa asali ya Tanzania bado inaendelea kukidhi viwango vya

43


ubora wa soko la ndani na la kimataifa. Katika kuendeleza wafugaji nyuki nchini, Wakala iliwezesha kuanzishwa na kusajiliwa kwa Chama cha kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania (Tanzania Beekeeping Development Organization -TABEDO).

Ushirikishwaji wa jamii katika Usimamizi wa rasilimali za Misitu

119. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Wakala utawezesha wananchi katika vijiji vinavyozunguka hifadhi za misitu na mashamba ya miti, kuotesha na kupanda miche ya miti 7,956,000 katika maeneo yao. Kazi nyingine ni kupitia mipango nane ya usimamizi wa pamoja wa misitu katika vijiji nane vya mikoa ya Tanga na Arusha; kuwezesha mipango ya usimamizi wa pamoja katika hifadhi za misitu mitatu ya asili; kutoa mafunzo kwa kamati za vijiji 51; na kutengeneza mipango ya usimamizi wa pamoja kwa vijiji viwili. Vilevile, Wakala utakamilisha mipango ya usimamizi wa pamoja katika vijiji saba; kutoa mafunzo kwa jamii kuhusu matumizi endelevu ya rasilimali za misitu na nyuki; na shughuli za kuongeza kipato kwa wanavijiji 240 waishio kando ya misitu ya hifadhi.

iii.         Vyuo vya Taaluma ya Misitu na Ufugaji Nyuki


120. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/2016, wanafunzi 683 wamedahiliwa kama ifuatavyo:- Chuo cha Misitu Olmotonyi – Arusha 519 Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki - Tabora 91 na Chuo cha Viwanda vya Misitu- Moshi 73. Vilevile, Chuo cha Misitu, Olmotonyi kimekarabati bwalo la chakula, nyumba saba za watumishi na mfumo wa mawasiliano kwa njia ya mtandao. Aidha, maandalizi ya makisio ya gharama ya ujenzi (BOQ) kwa ajili ya ukarabati wa ukumbi wa mihadhara, jengo la kuchakata magogo na jengo la kutengeneza samani yanaendelea. Chuo cha Ufugaji nyuki Tabora kimekarabati madarasa mawili na mabweni matatu. Pia, chuo kimemwezesha Mkufunzi mmoja kusomea Shahada ya Uzamili.

44



121.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Vyuo vya Misitu na Ufugaji Nyuki vinatarajia kudahili jumla ya wanafunzi 880 kama ifuatavyo: Chuo cha Misitu Olmotonyi, Arusha-600; Chuo cha Viwanda vya Misitu, Moshi -150 na Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki, Tabora -130.

122.      Mheshimiwa Spika, Chuo cha Misitu Olmotonyi kinatarajia kujenga jengo moja la mihadhara na hosteli ya wasichana na kukarabati nyumba nane za watumishi kupitia mradi wa ECOPRC (Empowering Communities through Training on Participatory Forest Management, REDD+ and Climate Change Initiatives). Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki, Tabora kinatarajia kukarabati jengo la utawala, chumba cha mihadhara na kutengeneza mfumo wa kuvuna maji ya mvua. Pia, Chuo kitanunua pikipiki mbili na mahema matano. Chuo cha Viwanda vya Misitu kitajenga maktaba; kukarabati madarasa mawili, mabweni mawili na bwalo la chakula. Vilevile, Chuo kitanunua vifaa vya kisasa vya karakana na kuwawezesha watumishi watatu kupata mafunzo ya muda mfupi.



iv.         Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania


123. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/2016, Taasisi iliendelea na utafiti juu ya umri sahihi wa kuvuna miti ya misindano na ubora wa mbao kutoka katika mashamba ya miti ya Rongai, Meru, na West Kilimanjaro. Taasisi ilipima ubora wa miti ya misindano ya umri kati ya miaka 15 hadi 23 iliyoweza kupatikana kwenye mashamba hayo. Miti ya umri kuanzia miaka kati ya 20 na 23 ilionekana kuwa na ubora ambao hauna tofauti aushi (significant difference) na miti ya umri wa miaka 25. Hivyo, inashauriwa kuwa miti ya misindano inaweza kuvunwa kuanzia miaka 20 na kuendelea na sio chini ya hapo ili kuwa na ubora katika matumizi mbalimbali ya mbao. Utafiti huu umesaidia Wizara kuandaa mwongozo bora wa uvunaji ambao utatumika

45


na wadau wengine wenye mashamba ya miti ya misindano kwenye maeneo yenye ikolojia inayofanana na sehemu utafiti ulikofanyika. Hata hivyo, Taasisi itaendelea kufanya aina hii ya utafiti kwa mashamba yaliyobakia ya Rubya na Buhindi.

124.      Mheshimiwa Spika, Taasisi imefanikiwa kuwashirikisha wakulima wanaolima kwenye miteremko ya safu za milima ya Uluguru kutumia teknolojia ya Kilimo-Mseto. Teknolojia hiyo inahusisha kilimo cha mchanganyiko wa mazao ya chakula, miti aina ya mkenge (Albizia versicolor) na utupa (Tephrosia vogelii). Katika kufanikisha matumizi ya teknolojia hii, miche 11,175 ya mkenge ilizalishwa na kupandwa katika vijiji vya Tandali (4,200), Ng’weme (264), Kibwege (660), Lugen (5,843) na Mtombozi (208). Aidha, Taasisi imeshirikisha wananchi kuanzisha shamba la Kilimo Mseto kwa kutumia teknolojia ya kontua katika vijiji vya Lugeni na Tandali katika mkoa wa Morogoro. Teknolojia hizi zimewafikia wakulima 135 waishio katika miteremko ya safu za milima ya Uluguru na Wilaya ya Morogoro Vijijini. Hata hivyo, kazi hii itaendelea katika mwaka 2016/2017 ili kubaini matokeo ya uzalishaji.

125.      Mheshimiwa Spika, Taasisi kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania na Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania imeendelea na utafiti wa uboreshaji wa miti ya asili ya Mkongo (Afzelia quanzensis), Mvule (Milicia excelsa) na Mkangazi (Khaya anthotheca) kwa kutambua miti-mama yenye ubora, kukusanya vipando na kuvipanda tayari kwa kuzalisha miche bora.

126.      Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha uwezo wa vituo vyake, taasisi imenunua kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kituo cha Dodoma katika wilaya ya Chamwino. Vilevile, imeboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa kuweka mfumo wa maji safi kwenye majengo ya Makao Makuu ya Taasisi mjini Morogoro. Taasisi imewezesha watumishi nane kuhudhuria mafunzo ya

46


muda mfupi na saba wamejiunga na mafunzo ya muda mrefu ya shahada za uzamili na uzamivu. Aidha, watumishi sita wamehitimu masomo ya stashahada (2), shahada (2) na shahada ya uzamivu (2) na kuajiri watumishi wengine 28 wa kada mbalimbali.


127.      Mheshimiwa Spika, mwaka 2016/2017, Taasisi itaendelea na utafiti juu ya umri sahihi wa kuvuna miti ya misindano na ubora wa mbao kutoka katika mashamba ya miti ya Rubya (Ukerewe) na Buhindi (Sengerema). Vilevile, itaanza utafiti wa matumizi ya maji kwenye mashamba ya miti ya Ruvu Kaskazini (Kibaha) na Sao Hill (Mufindi) yaliyopandwa mikaratusi na misindano. Aidha, Taasisi itafanya utafiti juu ya tatizo la kukauka miti ya misindano kwenye mashamba ya Mbizi (Sumbawanga) na Wino (Songea). Pia, Taasisi kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu na Wakala wa Mbegu za Miti itaendelea na utafiti wa uboreshaji na uzalishaji miche bora ya Msaji/Mtiki (Tectona grandis), na Mkongo (Afzelia quanzensis) kwa kutumia teknolojia ya tishu (Tissue Culture).

128.      Mheshimiwa Spika, Taasisi itanunua magari mawili; vifaa vya maabara za utafiti wa uzalishaji na matumizi ya misitu; itaimarisha mfumo wa TEHAMA kwenye ofisi za Makao Makuu na vituo vya utafiti; na kujenga ofisi za vituo vya Tabora, Mufindi na Dodoma. Aidha, Taasisi itaajiri watumishi 27 katika fani mbalimbali. Mapitio ya Mpango Mkakati wa 2012-2016 yatafanyika ili kuandaa Mpango Mkakati wa miaka mitano (2017-2021) utakaojumuisha masuala mapya yanayoikabili sekta ya misitu nchini.

v.           Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania

129. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wakala umekusanya kilo 6,606 za mbegu za miti na kuuza kilo 3,353 zenye thamani ya shilingi 113,707,635. Aidha, aina 132 za mbegu za miti ziliuzwa, kati ya hizo aina 48 ni miti ya asili ya Tanzania na 84 ni miti ya kigeni. Hadi mwezi April 2016,

47


kiasi cha mbegu kilichokuwa katika maghala ya Wakala ni kilo 13,610 zenye thamani ya shilingi 160,000,000.

130.      Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kuwa upatikanaji wa mbegu bora za miti unakuwa endelevu, Wakala uliainisha vyanzo vitano vya mbegu bora za miti ya Mkongo (Afzelia quanzensis), Mwalambe, Mwiluti na Mpaulonia. Wakala uliendelea kutunza vyanzo 35 vya mbegu za miti aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mfudufudu (Gmelina aborea), Msindano (Pinus Patula), Mkangazi (Khaya anthotheca), Mtiki (Tectona grandis), Mwerezi (Cedrela odorata), Mvule (Milicia excelsa), Mninga (Pterocarpus angolencis), Mti kivuli (Acrocarpus fraxinifolius) na Mwarobaini (Azadirachta indica).

131.      Mheshimiwa Spika, Wakala uliuza miche 64,170 ya Mitiki (Tectona grandis), Miembe (Mangifera indica), Mikangazi (Khaya Anthotheca)
Mgrevilea (Grevillea robusta) na Mgolimazi (Trichilia emetica) yenye thamani ya shilingi 67,616,000. Vilevile, Wakala uliendesha mafunzo ya muda mfupi kuhusu kuanzisha bustani na kutunza miche ya miti kwa washiriki 12 kutoka mikoa ya Morogoro na Iringa.

132.      Mheshimiwa Spika, mwaka 2016/2017 Wakala utakusanya kilo 13,500, kuuza kilo 12,500 za mbegu za miti na kuuza miche ya miti 150,000. Aina ya mbegu zitakazouzwa ni pamoja na Msindano (Pinus patula), Mkangazi

(Khaya anthotheca), Mtiki (Tectona grandis), Mwerezi (Cedrela odorata), Mkenge (Albizia versicolor), Mgunga (Acacia nilotica) na Mkongo (Afzelia quanzesis). Miche itakayouzwa ni pamoja na Mitiki, Miembe (Mangifera indica), Michungwa
(Citrus sinensis), Mkangazi (Khaya anthotheca), na Mwalambe (Terminalia ivorensis).

133.      Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa mbegu bora za miti, Wakala utaanzisha vyanzo viwili vya mbegu bora za miti

48


ya Mlonge na Mvule. Vilevile, Wakala utaendelea kutunza vyanzo 35 vya mbegu za miti ya aina mbalimbali, kutambua na kusajili vyanzo vitatu vya mbegu za miti aina ya Mkenge na Mgunga. Aidha, Wakala utaendesha mafunzo ya muda mfupi kwa wadau mbalimbali kuhusu kuanzisha bustani na kutunza miche ya miti.

vi.         Mfuko wa Misitu Tanzania


134. Mheshimiwa Spika, Mfuko unatoa ruzuku katika maeneo matatu ya kipaumbele ambayo ni: Uhifadhi, Uendelezaji na Usimamizi wa Rasilimali Misitu; Uboreshaji wa Maisha ya Jamii zinazoishi pembezoni mwa misitu kupitia shughuli kama za ufugaji nyuki, ufugaji na samaki; na Utafiti ulengao kuboresha uhifadhi na usimamizi wa rasilimali misitu. Kwa mwaka 2015/2016, Mfuko ulikadiria kukusanya jumla ya Shilingi 6,486,171,000. Hadi Aprili, 2016, Mfuko umekusanya Shilingi 3,970,607,029.92 sawa na asilimia 61.2. Aidha, Mfuko ulitoa ruzuku kwa miradi 217 iliyokuwa inaendelea na miradi mipya 83.
135. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Mfuko unatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 6,251,392,042 na kutoa ruzuku kwa miradi 285 inayoendelea na miradi mipya 115. Vilevile, Mfuko utawezesha uchapishwaji wa gazeti la “Misitu ni Mali” ambapo nakala 8,000 zitasambazwa kwa wadau mbalimbali. Aidha, Mfuko utagharamia utoaji wa elimu kwa Umma kupitia vipindi 24 vya redio na vipindi 4 vya televisheni. Pia, utawezesha Wakala wa Mbegu za Miti (TTSA) kuchapisha nakala 5,000 za Mwongozo wa Upandaji Miti Tanzania. Vilevile, utaiwezesha Wakala wa Huduma za Misitu kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa maduhuli ya misitu.

c. Sekta Ndogo ya Utalii

i.        Sera na Sheria


49



136.      Mheshimiwa Spika, ili kuboresha na kuongeza tija katika biashara ya utalii, Wizara kwa kutumia Sheria ya Utalii sura namba 29 imekamilisha na kuchapisha kanuni tano za kusimamia biashara hiyo nchini. Kanuni hizo ni: Kanuni ya Tozo ya Maendeleo ya Utalii; Kanuni ya Ada za Leseni; Kanuni ya Huduma za Malazi; Kanuni ya Wakala wa Utalii; na Kanuni za Waongoza Watalii. Aidha, ili kukuza utalii endelevu, Wizara kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na wadau wengine inaandaa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kuendeleza utalii nchini. Mpango Mkakati huo unaandaliwa sanjari na mapitio ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999.

137.      Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2016/2017, Wizara itafanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 ili kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika sekta ya utalii duniani. Aidha, ili kukuza utalii endelevu, Wizara kwa kushirikiana na wadau inaandaa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kuendeleza utalii nchini kwa ajili ya kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inaimarishwa. Mpango Mkakati huo utaongeza mchango wa sekta ya utalii kwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi kupitia Pato la Taifa, mapato ya fedha za kigeni, ajira, kuvutia uwekezaji na uwezeshaji wa maendeleo ya miundombinu. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na wadau itaainisha maeneo ya uwekezaji wa hoteli za kitalii katika ukanda wa pwani na maeneo mengine yenye vivutio.

ii.        Kuboresha Mazingira ya Biashara ya Utalii Nchini


138.      Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya biashara ya utalii nchini, Wizara ilianzisha Mfumo wa kompyuta wa usajili na utoaji wa leseni za kufanya biashara ya utalii (Tourism Online Registration and Licensing System). Mfumo huu umepunguza usumbufu kwa wateja na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Aidha, Mfumo umerahisisha kazi za


50


kufuatilia biashara za utalii na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanalipa tozo stahili Serikalini.

139. Mheshimiwa Spika, kupitia mfumo huu, mapato yatokanayo na Leseni za biashara ya utalii yameongezeka kutoka shilingi 3,575,629,297 mwaka 2013/2014 hadi kufikia shilingi 3,666,586,702 mwaka 2014/2015. Mwaka 2015/2016, Wizara ililenga kukusanya shilingi 5,907,000,000 na hadi mwisho wa Aprili 2016 shilingi 4,647,797,932.21 sawa na asilimia 82.7 zimekusanywa. Fedha hizo zimekusanywa kutoka katika Kampuni 890 kati ya Kampuni 1,220 zilizosajiliwa mwaka jana.


140.      Mheshimiwa Spika, jitihada za kuboresha mazingira ya utendaji kazi ya wapagazi, wapishi na waongoza watalii zimefanyika sambamba na kuboresha utoaji huduma kwa watalii. Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu pamoja na sekta binafsi imekamilisha mikataba ya ajira ambayo watoa huduma wataingia na waajiri. Mikataba hii inalenga kuondoa mgogoro kuhusu mazingira bora ya kazi na ujira ambao umedumu kwa muda mrefu baina ya watoa huduma hao na waajiri wao. Lengo ni kuhakikisha kwamba huduma katika sekta ya utalii zinaboreshwa kwa maslahi mapana ya taifa.


141.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017 Wizara kwa kushirikiana na Benki Kuu, ofisi ya Taifa ya Takwimu, Idara ya Uhamiaji na Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar itaendelea kufanya utafiti kuhusu mwenendo wa biashara ya utalii nchini. Utafiti huo utasaidia kupata taarifa sahihi ambazo zitasaidia katika kuaandaa mipango ya maendeleo ya sekta ya utalii pamoja na kujua mchango wake katika Pato la Taifa. Aidha, wizara itaendelea kukusanya na kuainisha takwimu za utalii zitakazowezesha kupima ukuaji wa sekta ya utalii.



51


142.      Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza utalii Kanda ya Kusini, Wizara kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inaandaa mradi wa “Resilient Natural Resource Management for Growth” (REGROW). Mradi huu ambao maandalizi yake yameanza Novemba, 2014, unatarajiwa kuanza rasmi Januari, 2017. Mradi unalenga kuboresha matumizi bora ya ardhi kwenye maeneo yenye vivutio vya utalii, kuendeleza na kusimamia utalii ikolojia, kuboresha miundombinu katika maeneo ya vivutio vya utalii na kuainisha fursa za kiuchumi za kuendeleza utalii kusini mwa Tanzania. Maeneo yatakayohusika katika utekelezaji wa mradi huu ni Hifadhi za Taifa Ruaha (Bonde la ardhioevu Usangu), Mikumi, Udzungwa na Pori la Akiba Selous.


143.      Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Mradi huu unahusisha pia Ofisi ya Rais - TAMISEMI; Wizara za Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Maji na Umwagiliaji; Kilimo, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Mradi utakuza kipato cha jamii inayoishi kandokando ya hifadhi kutokana na shughuli za kiuchumi zitokanazo na utalii. Mradi huu ni fursa ya kipekee ya kupanua wigo wa utalii nchini na kutimiza azma ya kuvutia watalii milioni nane watakaoliingizia taifa dola za Marekani bilioni 20 ifikapo mwaka 2025. Mradi utakuwa ni mfano wa kuigwa katika kuonyesha mbinu bora za kuratibu na kusimamia sekta zinazotegemeana lakini kiutendaji zinasigana na hivyo kusababisha upotevu na uharibifu wa maliasili na vivutio vya utalii.


144.      Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kutoa elimu, kutangaza na kuhamasisha jamii katika maonesho ya utalii saba ndani na nje ya nchi; kuendelea na kazi ya kupanga huduma za malazi katika madaraja ya ubora (nyota) katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Iringa, Mbeya na Rukwa. Wizara itaandaa Kanuni zinazosimamia mafunzo katika sekta ya utalii; kuainisha maeneo kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya utalii kwa kuzingatia vivutio vilivyopo; kufanya ukaguzi wa biashara ya utalii na kufuatilia miradi ya utalii iliyopitishwa na Kituo cha Uwekezaji. Aidha, Wizara itaunganisha Mfumo

52


wa kompyuta wa usajili na utoaji wa leseni za kufanya biashara ya utalii na mifumo ya TANAPA na Ngorongoro. Lengo ni kuimarisha udhibiti na kuhakikisha kuwa Wakala walio na usajili na leseni ndiyo wanaofanya biashara ya utalii na kuruhusiwa kuingia katika Hifadhi zetu.

iii.        Tozo ya Maendeleo ya Utalii (TDL)


145.      Mheshimiwa Spika, Tozo ya Maendeleo ya Utalii ilianzishwa chini ya Sheria ya Utalii Sura Na. 29 ya 2008 kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya utalii nchini. Tozo hii ilianza kukusanywa tarehe 1 Oktoba, 2013 kwa madhumuni ya kuendeleza vivutio vya utalii; kudhibiti ubora wa huduma za utalii; mafunzo na utafiti katika tasnia ya ukarimu na utalii; na utangazaji utalii. Tozo hii inatokana na michango ya asilimia tatu ya pato ghafi la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi za Taifa (TANAPA). Aidha, kila mtalii anapotumia huduma za malazi hutozwa tozo ya kitanda siku (bed night levy), sawa na USD 1.5. Kwa mwaka 2013/2014, Wizara ilikusanya shilingi 2,988,080,700 na katika mwaka 2014/2015 ilikusanya shilingi 4,263,541,672.

146.      Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato yatokanayo na nyumba za kulala wageni, Wizara imekamilisha zoezi la uhakiki wa nyumba zinazotoa huduma za malazi katika mikoa 25 ya Tanzania bara. Jumla ya nyumba za huduma za malazi 1,424 zimebainishwa na kuwekwa katika orodha ya kukusanya Tozo ya Maendeleo ya Utalii. Katika mwaka 2016/2017, Wizara itaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato katika kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa tozo hizo.

iv.        Watalii wanaoingia na kuondoka nchini


147.      Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Idara ya Uhamiaji, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Kamisheni ya Utalii Zanzibar ilifanya utafiti wa watalii wanaoondoka nchini

53


kupitia Viwanja vya Kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro (KIA) na Abeid Amani Karume (AAKIA) Zanzibar. Vilevile, Utafiti huo ulifanyika katika vituo vya kuingilia wageni vya Namanga, Tunduma, Mtukula, Manyovu na Horohoro ili kujua idadi ya siku anazokaa mtalii, wastani wa matumizi ya mtalii kwa siku na hatimaye kujua mapato yatokanayo na matumizi ya watalii waliotembelea vivutio mbalimbali hapa nchini. Uchambuzi wa awali umebaini kwamba mtalii mmoja hukaa nchini kwa wastani wa siku 10 na hutumia wastani wa dola za Marekani 263 kwa siku kwa package tour na wastani wa dola za Marekani 137 kwa non package. Kwa mwaka 2015/2016, idadi ya watalii walioingia ni 1,102,619 na wastani wa dola za Marekani 1,938.1 milioni zilipatikana.

Kubainisha Vivutio vya Utalii Nchini

148.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Wizara itabaini vivutio vipya vya utalii katika mikoa ya Mwanza, Geita, Mbeya, Manyara, Mara na Kigoma kwa lengo la kuvutia uwekezaji na kuendeleza sekta ya utalii. Aidha, itafanya tathmini ya miradi ya utalii wa kiutamaduni katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara na kuwajengea uelewa juu ya miongozo ya kufanya biashara hiyo. Vilevile, mikutano miwili ya Kamati ya Kufanikisha Utalii (Tourism Facilitation Committee) na minne ya ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi (Public Private Dialogue Forum) itafanyika.

v.                 Bodi ya Utalii Tanzania Utangazaji wa Utalii
149.       Mheshimiwa Spika, Ili kutangaza utalii katika masoko yanayoibukia, Bodi ya Utalii Tanzania iliratibu misafara ya mawakala wa utalii na waandishi wa habari 41 kutoka nchi za China, India na Umoja wa Falme za Kiarabu kati ya Oktoba na Desemba, 2015. Vilevile, Bodi ilishiriki katika kongamano la kuvutia wawekezaji na kutangaza utalii katika nchi za Umoja wa

54


Falme za Kiarabu lililofanyika Dubai mwezi Desemba, 2015. Aidha, Bodi ya Utalii Tanzania iliratibu safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa waandishi wa habari na wawakilishi kutoka kampuni za utalii za China wapatao 51. Safari hiyo ilifanyika Novemba, 2015 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano baina ya Tanzania na China. Safari hiyo ilitumika kutangaza utalii wa Tanzania katika kampuni za utalii za China ili kuvutia watalii wengi kutoka soko la utalii China.

150.      Mheshimiwa Spika, Bodi ya Utalii Tanzania iliandaa na kusimamia Onesho la Pili la kimataifa lijulikanalo kama Swahili International Tourism Expo (S!TE). Onesho hilo linalenga kutangaza utalii wa Tanzania na kukutanisha wafanyabiashara ya utalii wa Tanzania na Wakala wa Utalii wa kimataifa. Onesho hilo lilifanyika Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, kuanzia tarehe 1 hadi 3 Oktoba 2015. Jumla ya Kampuni 110 za utalii zinazojihusisha na utoaji wa huduma za malazi, kusafirisha watalii na Mashirika ya ndege ya ndani na nje ya nchi zilishiriki. Onesho hilo pia lilihudhuriwa na Wakala wa Utalii 39 kutoka nchi za Marekani, Israel, Canada, Australia, Uholanzi, India, Ireland, Uingereza, Ujerumani, Afrika Kusini, Falme za Kiarabu, Visiwa vya Ushelisheli na Kenya.


151.      Mheshimiwa Spika, Bodi ya Utalii imeshiriki kikamilifu katika utangazaji utalii kupitia maonesho ya “Karibu Travel and Tourism Fair”-Arusha na “Kili Fair”- Moshi, Kilimanjaro. Maonesho haya huratibiwa kwa ushirikiano baina ya Bodi na Sekta binafsi yakishirikisha waoneshaji kutoka ndani na nje ya nchi. Lengo la maonesho hayo ni kutangaza utalii wa Tanzania na hufanyika mwezi Mei na Juni kila mwaka. Aidha, katika kuvutia watalii kuja nchini, Bodi ilishiriki maonesho ya utangazaji utalii nje ya nchi kupitia maonesho ya World Travel Market London, Novemba 2015, ITB Berlin-Ujerumani, Machi 2016 na Indaba - Afrika Kusini Mei 2016.



55



152.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Bodi ya Utalii Tanzania, itaimarisha utangazaji kwa njia ya TEHAMA ikiwemo tovuti, mitandao ya kijamii, ‘portal’ na ‘App’ inayopatikana kwenye simu za kisasa. Bodi kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waendesha Biashara za Utalii Tanzania, itaandaa mikakati mahususi ya utangazaji utalii katika masoko makuu ya utalii ya Uingereza, Ujerumani na Marekani. Bodi itawawezesha wananchi kuimarisha utalii wa utamaduni kwa kuongeza idadi ya vikundi jamii vinavyoshiriki katika programu ya utalii wa Utamaduni kutoka 60 ya sasa hadi kufikia 75.

153.      Mheshimiwa Spika, Katika kuhakikisha kuwa idadi ya watalii inaongezeka, Bodi imeandaa Tangazo litakalorushwa katika vituo vya televisheni za CNN na BBC kwa kipindi cha mwaka mmoja. Aidha, Bodi kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waendesha Biashara za Utalii nchini (TCT) itaandaa mikakati mahsusi ya utangazaji utalii katika masoko makuu ya Uingereza, Ujerumani na Marekani. Vile vile, Bodi itaweka matangazo ya utalii “Travel Magazine” pamoja na kushiriki maonesho matano ya utalii katika nchi za Uingereza, Afrika Kusini, Ujerumani na China. Bodi itashirikiana na “diaspora”, mabalozi wa hiari wa utalii na balozi zetu zilizo sehemu mbalimbali duniani katika kutangaza vivutio vya utalii. Katika soko la ndani, Bodi itaendelea kushiriki maonesho mbalimbali hapa nchini kama vile Sabasaba, Nanenane, Karibu Travel Fair, Kili Fair pamoja na Tamasha la Filamu la Zanzibar. Vilevile, itachapisha vipeperushi na majarida yatakayosambazwa kwa wadau.

vi.                Wakala wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)


154.      Mheshimiwa Spika, Dira ya Wakala ni kuwa kituo bora Afrika kinachotoa mafunzo, utafiti na ushauri katika fani za utalii na ukarimu. Hatua hiyo itafikiwa kwa kutoa mafunzo kwa kutumia vifaa vya kisasa, kutoa kozi za

56


uongozi na usimamizi, kuajiri watumishi wenye sifa na weledi, kuhakikisha udahili unaongezeka mwaka hadi mwaka na kutoa huduma bora ya utafiti na ushauri. Mitaala inayotumika katika Kampasi zote tatu ina Ithibati kamili ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ambayo hurejewa kila baada ya miaka mitano.

155. Mheshimiwa Spika, Wakala unaendesha mafunzo ngazi ya Astashahada na Stashahada katika fani ya usafiri (air travel and ticketing) utalii na ukarimu. Wakala una kampasi tatu ambazo ni Bustani yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 360, Temeke 150 na Arusha 120. Ili kuboresha mafunzo, Wakala ulifanya mapitio ya mitaala ngazi (levels) ya 4, 5 na 6 kwa kushirikisha wadau ambapo mitaala mipya imeanza kutumika Septemba, 2015.

Tathmini ya mahitaji ya mafunzo


156. Mheshimiwa Spika, Wakala umefanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo kwa wakufunzi wa vyuo 10 vinavyotoa elimu ya Ukarimu na Utalii nchini. Lengo ni kubaini mahitaji ili kuwajengea uwezo wakufunzi watoao mafunzo katika vyuo hivyo. Matokeo ya tathmini hiyo yalibaini mapungufu katika maeneo ya mbinu za ufundishaji, ujuzi mwanana (soft skills), mbinu za uongozi na usimamizi katika fani ya ukarimu na mbinu za mafunzo kwa vitendo. Matokeo haya yalisababisha kuandaliwa kwa Programu ya Mafunzo ambayo utekelezaji wake umeanza mwezi Desemba, 2015. Wakufunzi 48 wa Wakala walipata mafunzo yatakayowezesha kutoa mafunzo kwa wakufunzi wengine katika fani za ukarimu na utalii hapa nchini.

Udahili wa Wanafunzi


157. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2015/2016 Wakala umedahili jumla ya wanafunzi 201. Kati ya hao, 123 ni ngazi ya Astashahada na 78 ni Stashahada. Katika mwaka huo, wanafunzi 211 walihitimu mafunzo katika

57


ngazi ya Astashahada na Stashahada katika kozi zitolewazo na Chuo. Aidha, Wakala kwa kushirikiana na Sekta binafsi chini ya ufadhili wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) umeanzisha Programu ya Uanagenzi (Apprenticeship) ambapo wanafunzi 14 wamehitimu na wengine 21 wanaendelea na mafunzo.

158. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2016/2017, Wakala utadahili wanafunzi 315 katika fani ya Ukarimu, Usafiri na Utalii hapa nchini. Kati ya hao, wanafunzi wa ngazi ya Stashahada ni 96 na Astashahada 219. Jaribio la Programu ya Uanagenzi (apprenticeship) ambalo lilifanyika kwa ushirikiano kati ya Chama cha Wenye Hoteli, Shirika la Kazi Duniani na Wakala katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha limekamilika. Hivyo, wakala utaanza mafunzo kwa wanafunzi 200 chini ya programu hiyo. Ili kuinua kiwango cha huduma katika sekta ya Utalii nchini, Wakala kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Vancouver na sekta binafsi itaboresha kozi za muda mrefu na mfupi. Kozi hizo ni pamoja na Huduma kwa Mteja, Uratibu wa Matukio (Event Management) na Huduma za Usafiri wa Anga.

d. Sekta Ndogo ya Malikale

Sera na Sheria


159.       Mheshimiwa Spika, katika kuhifadhi na kuendeleza maeneo ya Malikale Wizara imeandaa mwongozo wa uhifadhi wa mji wa kihistoria wa Mikindani-Mtwara. Aidha, Wizara imeandaa rasimu ya Mwongozo wa uwekezaji unaobainisha maeneo ambayo wadau mbalimbali wanaweza kuwekeza.

160.      Mheshimiwa Spika, mwaka 2016/2017, Wizara itasimamia na kuratibu utekelezaji wa Sera na mkakati wa kufanya maeneo ya malikale kuwa vivutio vya utalii na vituo vya mafunzo. Vilevile, tathmini ya maeneo 22 ya malikale yaliyopo katika Mikoa ya Lindi (4) na Tanga (18) yaliyotangazwa katika Gazeti la Serikali itafanyika. Pia, wadau mbalimbali wataendelea

58


kushirikishwa katika kuhifadhi malikale katika Miji ya Tanga, Pangani na Mtwara-Mikindani.

i.                Utangazaji na Ushirikishwaji wa jamii na wadau wa Maeneo yenye Malikale

161.      Mheshimiwa Spika, ili kutangaza na kuendelea kuijengea jamii uelewa kuhusu uwepo wa vivutio vya rasilimalikale, Wizara imetangaza Utalii wa Urithi wa utamaduni katika maonesho na maadhimisho mbalimbali ndani na nje ya nchi. Maonesho ya ndani ya nchi ni pamoja na Sabasaba, Nanenane na maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita vya Maji Maji yaliyofanyika Mjini Songea Februari, 2016. Aidha, Wizara ilitangaza utalii wa utamaduni katika tamasha la Historia, Sanaa, na Utamaduni kwa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki lililofanyikia Nairobi – Kenya, Agosti 2015. Vilevile, Wizara inaendelea kuhamasisha na kutoa kipaumbele kwa wananchi wanaozunguka na wanaomiliki maeneo yaliyo na vivutio vya malikale ili watambue fursa zilizopo katika maeneo hayo kama vile kuanzisha makumbusho, vituo vya utalii, maduka ya vitu vya utamaduni, migahawa na kutembeza wageni.

ii.                Uhifadhi na Uendelezaji wa Rasilimalikale


162.      Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuhifadhi na kuendeleza urithi wa utamaduni. Mwaka 2015/2016, Wizara imekarabati jengo lililokuwa mahabusu katika eneo la Makumbusho ya Kumbukumbu ya Chifu Mkwawa, Kalenga mkoani Iringa, kuwa ofisi ya kituo. Aidha, Wizara imekamilisha michoro ya ukarabati wa Jengo la Boma la Kijerumani Pangani,Tanga. Vilevile, imekamilisha michoro ya ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Taarifa cha Mapango ya Amboni; kukarabati jengo la Afya, Tabora; kuweka uzio katika eneo la magofu ya kituo cha Kunduchi; kuboresha mandhari ya Kituo cha


59


Kumbukumbu na Taarifa cha Dkt. Livingstone, Ujiji-Kigoma na mji Mkongwe Bagamoyo.

163.      Mheshimiwa Spika, katika kuhifadhi na kuendeleza maeneo ya Urithi wa Dunia ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara, Wizara imechukua hatua za kuzuia mmomonyoko wa udongo kwa kujenga ukuta karibu na gofu la Ngome ya Gereza, Kilwa Kisiwani ili kupunguza ama kuzuia kabisa mawimbi ya bahari yasiiathiri ngome hiyo. Aidha, imeweza kukamilisha Mpango wa Usimamizi wa Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara wa miaka minne ( 2016-2019) na kukamilisha rasimu ya Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ya Kijiji cha Songo Mnara.


164.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Wizara itajenga Kituo cha Taarifa na Kumbukumbu kwenye eneo la Mapango ya Amboni; uzio katika Magofu ya Kunduchi; na banda la kutolea mihadhara na njia za waenda kwa miguu katika Magofu ya Kaole. Aidha, ukarabati wa Jengo la Makumbusho ya Caravan Serai na Jengo la Afya Tabora utafanyika. Wizara itakamilisha michoro na gharama kwa ajili ya kuboresha mandhari ya Kituo cha Kumbukumbu cha Dkt. Livingstone Ujiji na Kituo cha Mji Mkongwe - Bagamoyo.

iii.                Utafiti wa Malikale


165.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/2016, jumla ya tafiti tisa za kisayansi za Mambo ya kale zimefanyika katika maeneo ya Singida; Laetoli, Olduvai, Makuyuni na Tarangire- Arusha; Bonde la Ufa la Rukwa; Isimila - Iringa na Kwamtoro - Kondoa. Tafiti hizi zimefanyika kwa kushirikisha wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi za nje. Utafiti huu umewezesha Wizara na Taifa kwa jumla kunufaika kwa kuongeza makusanyo ya mapato, kwa kupitia ada ya utafiti unaofanywa na wataalamu toka nje ya

60


nchi na mafunzo kwa wataalamu wa Wizara katika Nyanja za uhifadhi wa malikale.


166.      Mheshimiwa Spika, utafiti huo pia umewezesha kuboreshwa kwa miundo mbinu ya utafiti katika maeneo ya malikale kama vile ujenzi wa maabara, stoo na samani za kuhifadhi mikusanyo ya utafiti katika eneo la Bonde la Olduvai. Wizara inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa utafiti ili kuendeleza tafiti nchini kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali za uhifadhi na uendelezaji wa malikale na pia kuelimisha jamii kuhusu malikale kupitia matokeo ya utafiti huo.

iv.                Ushiriki katika mikutano ya kikanda na kimataifa


167.      Mheshimiwa Spika, ili kuendelea kunufaika na fursa zilizopo katika uhifadhi wa malikale katika ngazi ya kimataifa, mwaka 2015/2016, Wizara ilishiriki katika Mkutano Mkuu wa Nchi Wanachama wa UNESCO uliofanyika Paris, Ufaransa mwezi Novemba, 2015. Katika mkutano huo, Tanzania ilipata heshima ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia (WHC). Fursa hiyo itaiwezesha Tanzania kushiriki katika mipango na maamuzi yenye maslahi kwa nchi yetu na Afrika kwa ujumla pamoja na kujenga uwezo wa wataalamu wetu.










v.                  Mfuko wa Taifa wa Mambo ya Kale


168.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/2016, Mfuko ulipanga kukusanya kiasi cha Shilingi 1,000,000,000. Vyanzo vya Mfuko vinatokana na

61


tozo za viingilio zinazotozwa kwa watalii wanaotembelea vituo, ada za vibali kwa watafiti, hati miliki (royality), Misaada (grants and donation), na mauzo mbalimbali ya machapisho yakiwemo majarida, vipeperushi, vitabu, postcards zenye taarifa za Mambo ya Kale. Hadi Aprili 2016, shilingi 533,353,883 ambazo ni sawa na asilimia 53.3 ya lengo zimekusanywa. Fedha za Mfuko zilielekezwa katika utafiti, uhifadhi na uendelezaji wa maeneo yenye rasilimalikale.


vi.                Shirika la Makumbusho ya Taifa Tanzania


169.      Mheshimiwa Spika, katika, mwaka 2015/2016, Shirika limeboresha maonesho ya muda na kudumu katika makumbusho zake zote. Maboresho yaliyofanyika ni pamoja na kubadili vioneshwa na mpangilio wa onesho, kuongeza idadi ya vioneshwa, kubadilisha karatasi za maelezo ya vioneshwa (captions) na kuweka taa au kupaka rangi kumbi za maonesho. Maonesho mapya kumi na moja (11) yamefanyika kwenye makumbusho za Shirika na moja (1) kwenye Sabasaba. Kati ya maonesho hayo, moja lilikuwa onesho maalumu la picha za watu wenye albinism kwa lengo la kuelimisha umma juu ya chanzo cha albinism ili kuondoa unyanyapaa wa mila na desturi za Ki-Afrika. Vilevile, onesho maalumu mseto la sanaa za kuchora na utafiti juu ya mitazamo ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi katika bonde la Kilombero limefanyika. Sanaa hizo zilichorwa na wanavijiji wa bonde la Kilombero.

170.      Mheshimiwa Spika, Shirika limeandaa onesho jipya la chimbuko la binadamu (The Cradle of Human kind). Onesho hili liko Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni - Dar es Salaam na limezinduliwa tarehe 18 Mei, 2016. Vilevile, Shirika limeandaa maonesho katika sikukuu za Kitaifa kwa kushirikiana na Kitengo cha Maadhimisho ya Kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Rais. Aidha, Shirika lilifanya programu mbili za sanaa

62


ambazo ni “Kivuko” (drama) na “Sauti Yetu” (contemporary dance). Programu za wanafunzi wa Shule za Msingi zimekuwa zikifanyika kila siku ya Ijumaa hadi mwishoni mwa 2015. Kazi miradi za wanafunzi wa sekondari zimekuwa zinaendelea kufanyika kila wiki.

171.      Mheshimiwa Spika, Shirika linaendelea kuhamasisha jamii kutembelea Makumbusho na limechapisha na kusambaza vipeperushi 5,000 kwa wadau mbalimbali. Pia, Shirika limeandaa jarida liitwalo Museum and House of Culture e-News Letter kuhamasisha jamii linalotolewa kila mwezi kwa njia ya mtandao.

172.      Mheshimiwa Spika, kumbukumbu ya Vita vya Maji Maji imefanyika mwezi Februari 2016 huko Songea. Katika maadhimisho hayo ya kuwaenzi mashujaa wa vita ya Majimaji, familia ya Hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa (Simba wa Vita) iliikabidhi rasmi Wizara, nyumba iliyoko Bombambili Songea na vifaa 245 alivyotumia yeye na familia yake enzi za uhai wake ili iwe sehemu ya Makumbusho ya Taifa. Nyumba hii inaelezea historia ya Tanzania kupitia maisha ya Hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa.

173.      Mheshimiwa Spika, napenda kutumia nafasi hii kuishukuru kwa mara nyingine familia ya Hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa (Simba wa Vita) kwa kuitoa nyumba hiyo pamoja na vifaa mbalimbali vitumike kwa ajili ya Makumbusho. Natoa wito kwa wananchi kuiga mfano huu ili kuwa na makumbusho za aina mbalimbali ili kutunza kumbukumbu za maendeleo ya taifa letu.


174.      Mheshimiwa Spika, mwaka 2016/2017, Shirika litajenga upya nyumba 22 za jadi na utamaduni katika Kijiji cha Makumbusho; kukarabati nyumba ya Hayati Mzee. Rashid Mfaume Kawawa (Simba wa Vita) iliyopo Bombambili mjini Songea ili iwe Makumbusho. Mipango ya kukarabati

63


nyumba hii imeanza na inatarajiwa kuwa Februari 2017 itazinduliwa kuwa Makumbusho ya Kumbukumbu ya Mzee Rashid. Kawawa. Vilevile, Shirika litafanya maandalizi ya awali ya ujenzi wa jengo la kisasa la kuhifadhi na kuonesha magari ya Kihistoria, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni. Aidha, Shirika litaboresha maonesho na kuhakikisha usalama wa mikusanyo; kufanya Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania kwa kushirikisha jamii ya Wamwera; kuitangaza Makumbusho na kusogeza huduma kwa jamii; kujenga uwezo na mazingira mazuri ya kufanyia kazi; na kupanua makumbusho kwa kushirikisha wadau.



e.    Utawala na Maendeleo ya Rasilimali watu

175.      Mheshimiwa Spika, mwaka 2015/2016, Wizara imeendelea kuratibu masuala ya Utawala na Maendeleo ya Rasilimaliwatu kwa kusimamia masuala ya watumishi katika maeneo ya ajira, upandishwaji cheo, kuthibitishwa kazini, mafunzo, nidhamu, maadili, ustawi na afya kwa watumishi. Wizara imeajiri watumishi 1,020 na kati ya hao, watumishi 584 ni wa kada ya Wanyamapori na 400 kada ya Misitu. Aidha, watumishi 118 wa kada mbalimbali wamepandishwa cheo, watumishi 491 wamethibitishwa kazini na watumishi 30 wamebadilishwa cheo kwa kuzingatia miundo ya utumishi wa kada zao.

176.      Mheshimiwa Spika, mwaka 2015/2016, Wizara imewezesha watumishi 155 kuhudhuria mafunzo mbalimbali ya muda mrefu na muda mfupi. Kati ya hao, watumishi 89 wamehudhuria mafunzo ya muda mrefu na watumishi 66 mafunzo ya muda mfupi.

177.      Mheshimiwa Spika, Chama cha Akiba na Mikopo cha Wizara kimeendelea kuimarika ambapo idadi ya wanachama imeongezeka kutoka 75 hadi 176. Wanachama 21 wamenufaika kwa kupata mikopo ya dharura yenye

64


jumla ya shilingi 10,500,000. Aidha, Wizara imeendelea kuwawezesha watumishi wanaoishi na VVU waliojiweka wazi kwa kuwapatia fedha za kununulia lishe kwa lengo la kuimarisha afya zao. Vilevile, elimu juu ya masuala ya UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukizwa imeendelea kutolewa kwa watumishi kupitia mikutano mbalimbali.

178.       Mheshimiwa Spika, katika kujenga mahusiano mazuri na watumishi wa Sekta nyingine na kutoa elimu kwa jamii, watumishi 80 walishiriki katika maonesho ya 39 ya Kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) na watumishi wanawake 147 walishiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Baraza la Wafanyakazi limekutana kujadili utekelezaji wa Mpango na bajeti ya mwaka 2015/2016 na kupitia Mpango na bajeti ya mwaka 2016/2017. Aidha, Mapitio ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Wizara (2013
– 2016) yamefanyika na kuandaa Mpango Mkakati (2016-2021).



179.      Mheshimiwa Spika, mwaka 2016/2017, Wizara itaajiri watumishi 789, kati ya hao, 500 ni wa kada ya Wanyamapori na 243 kada ya Misitu na Nyuki. Aidha, Wizara itapandisha cheo watumishi 225 wa kada mbalimbali, watumishi 1,056 watathibitishwa kazini na watumishi 289 watawezeshwa kuhudhuria mafunzo mbalimbali. Watumishi 105 watahudhuria mafunzo ya muda mrefu na 184 watahudhuria mafunzo ya muda mfupi ikiwemo ya kuwaandaa wastaafu 48. Vilevile, Wizara itaendelea kuimarisha mifumo ya kudhibiti watumishi hewa.

180.      Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa afya itaandaa Mpango Mkakati wa kupambana na UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi. Aidha, Wizara itaendelea kuwawezesha watumishi wanaoishi na VVU waliojiweka wazi kupata fedha ya huduma ya lishe na kuwawekea mazingira bora ya kutekeleza majukumu yao. Vilevile,



65


elimu ya masuala ya UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukizwa itaendelea kutolewa kwa watumishi.

181. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa, kukuza maadili, kuboresha huduma kwa wateja na utawala bora. Aidha, Wizara itaimarisha mahusiano na sekta nyingine na kuwawezesha watumishi kushiriki maonesho na maadhimisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wiki ya Utumishi wa Umma, Siku ya Wanawake Duniani na Mei Mosi. Pia, Wizara itaandaa mikutano miwili ya Baraza la Wafanyakazi na itawawezesha watumishi kushiriki mashindano ya michezo ya SHIMIWI na Mei Mosi. Vilevile, Wizara itaimarisha ushirikiano na sekta binafsi na Wadau wa maendeleo kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha katika mapitio ya utekelezaji wa Sekta ya Maliasili na Utalii.

IV.        SHUKURANI


182.      Mheshimiwa Spika, napenda sasa kuchukua fursa hii kuwashukuru wale wote waliochangia kuiwezesha Wizara yangu kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Shukurani zangu za dhati ziende kwa wananchi hususan wanaoishi kwenye maeneo yanayopakana na hifadhi. Ushiriki wao katika kulinda rasilimali za maliasili na malikale umechangia uwepo wa rasilimali hizo kwa maendeleo ya nchi. Nachukua nafasi hii kuwaomba kuendelea kushirikiana nasi katika kuendeleza sekta hii.

183.      Mheshimiwa Spika, Napenda kuzishukuru nchi, Mashirika na

Taasisi mbalimbali kwa ushirikiano walioutoa katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara yangu. Nachukua fursa hii kutaja baadhi yao kama ifuatavyo: Serikali za Canada, China, Finland, Korea Kusini, Marekani, Norway, Ubelgiji, Ufaransa, Ujerumani, Uswisi na Jumuiya ya nchi za Ulaya. Mashirika ni pamoja na AWF, AWHF, BTC, FAO, FZS, GEF, GIZ, ILO, ICCROM, ICOM, ICOMOS, IUCN, HGBF, KfW, NORAD, Trade Aid, UNDP, UNESCO, UNWTO, USAID, WCS, WHC, World Bank na WWF.

66




184.      Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru kwa dhati Wafanyakazi wote wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizopo chini ya Wizara kwa ushirikiano wanaonipa katika kutekeleza majukumu yangu. Aidha, nawashukuru Mheshimiwa Mhandisi Ramo Makani (Mb.), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii; Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi, Katibu Mkuu; Mhandisi Angelina E. A. Madete, Naibu Katibu Mkuu; Wakurugenzi katika Idara, Vitengo, Taasisi, Wakala na Mashirika yaliyo chini ya Wizara kwa ushauri na utayari wao wakati wote katika kutekeleza majukumu ya Wizara kwa kuzingatia Dhana ya HAPA KAZI TU.

V.           MAOMBI YA FEDHA


185.      Mheshimiwa Spika, naomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya jumla ya Sh. 135,797,787,000 kwa mwaka 2016/2017. Kati ya fedha hizo, Sh. 118,051,105,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Sh. 17,746,682,000 ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Fedha za Matumizi ya Kawaida zinajumuisha Sh. 59,592,676,000 za Mishahara ya watumishi na Sh.58,458,429,000 za Matumizi Mengineyo. Fedha za Miradi ya Maendeleo zinajumuisha Sh. 15,746,682,000 fedha za nje na Sh.2,000,000,000 fedha

za ndani.

186.      Mheshimiwa Spika, Hotuba hii inapatikana pia katika tovuti ya Wizara ya Maliasili na Utalii: www.mnrt.go.tz

187.      Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa Hoja.

TAKWIMU MBALIMBALI

No comments:

Post a Comment