Thursday, 8 September 2016

JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI YA JUHIWANGUMWA YATAMBULIWA KISHERIA

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi akizungumza kwenye mkutano kabla ya kukabidhi rasmi hati mbili kwa pamoja ya kuitambua Jumuiya ya JUHIWANGUMWA kama chombo halali kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za wanyamapori zilizopo ndani ya eneo laJumuiya hiyo kwa tangazo la serikali Na. 204 na hati ya matumizi endelevu ya rasilimali za Maliasili. Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika kijiji cha Utete Wilayani Rufiji

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( katikati) akiwa kwenye kikao cha Kamati Endeshi ( Steering Committee) inayosimamia Mradi wa KILOWEMP cha kujadili miradi inayotekelezwa katika maeneo ya Wilaya ya Rufiji. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Ubelgiji ( BTC), Bw. Ton Snis na kushoto na upande wa kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Idara ya Wanyamapori. Bw. Herman Keryaro.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi akioneshwa ramani na Mratibu wa mradi Kitaifa wa KILORWEMP Bw. Pellage Kauzeni unaotenganisha kati ya eneo la hifadhi ya Jumuiya ya JUHIWANGUMWA na kijiji cha Utete Wilayani Rufiji kabla ya kukabidhi rasmi hati ya kuitambua Jumuiya hiyo kama chombo halali kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za wanyamapori zilizopo ndani ya eneo laJumuiya hiyo kwa tangazo la serikali Na. 204 na hati ya matumizi endelevu ya rasilimali za Maliasili. Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika kijiji cha Utete Wilayani Rufiji
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa pili kushoto) alipotembelea Kambi ya Watalii jana iitwayo Trackers inayopatikana katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUHIWANGUMWA mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kukabidhi rasmi hati mbili kwa pamoja ya kuitambua Jumuiya ya JUHIWANGUMWA kama chombo halali kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za wanyamapori zilizopo ndani ya eneo laJumuiya hiyo kwa tangazo la serikali Na 204 na hati ya matumizi endelevu ya rasilimali za Maliasili
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa pilia kulia aliyekaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na na Kamati Endeshi ( Steering Committee) inayosimamia Mradi wa KILOWEMP katika kikao kilichofanyika jana Wilayani Rufiji . Kamati hiyo ndiyo iliyosaidia kuratibu mpaka kufikia hatua Serikali kuamua kukabidhi hati mbili kwa pamoja katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUHIWANGUMWA.

Serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi, imekabidhi rasmi hati ya ya kuitambua Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUHIWANGUMWA kama chombo halali kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia rasilimali za wanyamapori zilizopo ndani ya eneo la Jumuiya hiyo, Rufiji mkoani Pwani.
Pia, imekabidhi hati ya matumizi endelevu ya rasilimali za Maliasili hususani wanyamapori kwa kuwapa wananchi mamlaka ya kusimamia na kutumia rasilimali hizo kwa kuwa na uhifadhi na maendeleo endelevu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho katika maeneo yao, Taifa na Dunia kwa ujumla.
Akizungumza jana katika kijiji cha Utete wilayani Rufiji wakati akikabidhi hati hizo mbili kwa pamoja kwa Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya JUHIWANGUMWA , Milanzi amewatahadhalisha Viongozi wa Jumuiya hiyo kuwa na waadilifu wawazi hususani katika masuala ya pesa na mikataba watakayoingia na wawekezaji ili kuweza kuepuka migogoro isiyo ya lazima kutoka kwa Wananchi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika jumuiya nyingine.
‘’Tunataka fedha zitakazopatikana kupitia utalii wa Picha na utalii wa uwindaji ( photographic and tourist hunting) zitumike katika huduma za kijamii kwa kuboresha miundombinu, shule, hospitali na huduma nyinginezo za kijamii na sio pesa hizo zitumike kuwaneemesha watu wachache’’ alisema Milanzi
Aliongeza kuwa, Serikali kuu ( Wizara) itaendelea kuwasaidia pale inapohitajika kufanya hivyo katika masuala ya Uhifadhi, ‘’hatutaki kuwaingilia katika masuala yenu mfano katika masuala ya mapato na matumizi hivyo nawataka mshirikiane na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili msiweze kutumbukia kwenye migogoro ya namna hiyo’’ alisisitiza Milanzi
Aidha , Maj.Gen. Milanzi amewataka Wakuu wa Wilaya ya Rufiji, Malinyi, Kilombero na Ulanga ambazo ni Wilaya zinazounda jumuiya hiyo ya JUHIWANGUMWA yenye ukubwa wa kilomita za mraba 496.5 Kuhakikisha kuwa wanashirikiana na wananchi kuzuia mifugo isiingie ndani ya hifadhi kwa kuwa ni kinyume cha sheria ya uhifadhi kulisha mifugo hifadhini.
Milanzi alisema ‘’ Suala la kuingiza mifugo kwenye hifadhi lisiwe la kisiasa ni lazima kila mwananchi atambue kuingiza mifugo ndani ya hifadhi ya wanyamapori ni kuvunja sheria ya Uhifadhi hivyo atakayebainika lazima sheria ifuate mkondo wake’’
Pia, Milanzi alishukuru Serikali ya Ubelgiji kwa kusaidia kuanzishwa kwa hifadhi hiyo tangu mchakato ulipoanza mwaka 006 chini ya mradi wa ‘’ Eastern Selous Conservation Project’’ kwa juhudi wanazofanya kusaidia uhifadhi na hasa kwa kushirikisha wananchi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya Rufiji,Bw.Juma Njwaya alisema atahakikisha Hifadhi ya JUHIWANGUMWA inakuwa mfano katika masuala ya uwazi na uwajibakaji ili kuwawezesha wananchi kunufaika na rasilimali zao hususani wanyamapori.
Naye , Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Shabani Dihongo alisema wanajisikia fahari kwa hatua ambayo Serikali imefikia ya kuweza kupewa mamlaka kamili katika kuisimamia hifadhi yao
‘’Tutahakikisha tunafanya doria za kutosha na pia kila mwananchi atashirikishwa ili aweze kuona faida ya hifadhi hii ambayo tumeipigania kwa muda mrefu hatimaye leo tumeweza kupewa mamlaka kamili ya kuweza kuisimamia’’ alisema

No comments:

Post a Comment