Kutoka Mjengoni Dodoma Bunge la kujadili katiba limehairishwa na
Mwenyekiti baada ya kutokea kwa vurugu baada ya kutoelewana kwa baadhi
wabunge kati ya Mh. Aboubakary ambaye ni Mwakilishi Mkuu wa Serikali ya
Zanzibar alipomuomba Mheshimiwa Mwenyekiti asikubali kuruhusu baadhi ya
majina ya wachangiaji wakati majina hayo hayajafika kwenye kamati
inayohusika na uratibu wa rasimu.
Baadhi ya wachangiaji akiwemo Ole Sendeka ambaye wameonekana majina
yao yanajirudia ndipo aliposimama na kusema inawezekana yeye Ole Sendeka
hoja zake na baadhi ya wajumbe wengine zinawagusa baadhi ya wajumbe
wanaoshughulikia kanuni hizo zinazojadiliwa sasa.
Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo Mh. Pandu Kificho alilazimika
kusimama na kuwaomba wajumbe wawe watulivu ili kuhakikisha kikao
kinaendelea baada ya mheshimiwa Aboubakary kusimama kumjibu Mheshimiwa
Ole Sendeka kuwa anadhani Mheshimiwa Olesendeka ni mchanga sana kwenye
masuala ya sheria maana yeye amaeanza miaka ya 1980 wakati mheshimiwa
Ole sendeka anatokea Simanjiro na ana miaka 10 tu hana lolote kwenye
masuala hayo ya sheria na hana anachokijua
Mwenyekiti wa Bunge hilo alihairisha Bunge hilo mpaka saa 10 Jioni.
No comments:
Post a Comment