Friday, 7 March 2014

TCRA YATOA ONYO KWA VITUO VYA ITV,STAR TV NA REDIO FREE

Leo March 07 Kamati ya maudhui ilikua na kikao cha kusoma uamuzi dhidi ya vituo vilivyokiuka kanuni za utangazaji,akisoma uamuzi huo mbele ya waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Kamati maudhui ya Tcra mama Magreth Mnyagi amevigusia vituo vitatu vilivyokiuka kanuni hizo.
1                                             
   Boss wa Itv akipokea barua ya onyo.
Vituo vilivyopewa onyo hilo ni vituo vinavyomilikiwa na Ipp pamoja na Sahara Media ambayo kwa Ipp onyo limepewa kituo chake cha ITV,upande wa Sahara Media onyo limepewa kupitia vituo vyake vya Star Tv na Radio Free Africa,kwa kutangaza maudhui yanayokiuka kanuni za utangazaji za mwaka  2005.
3                                             
   Boss wa Star Tv na Rfa akipokea barua ya Onyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui Injinia Margaret Mnyagi amesema kuwa adhabu ya onyo kali imetolewa kwa ITV na Star  Television kwa kurusha tangazo la Policy Forum 3/01/2014 ITV na 06/10/2014 lenye mwelekeo wa kichochezi, lililokusudia kuwashawishi wananchi kutolipa kodi na kuchukia  serikali nakuvunja kanuni za utangazaji za mwaka 2005,5 (a) na 6 (3).
Upande wa Radio Free Africa mnamo tarehe 27/6/2013 ilirusha wimbo wa  msanii Nash MC unaoitwa “sindano za moto” ambao ulikuwa na mwelekeo wa kichochezi wenye ilikuwa na lengo la kuashiria uvunjifu wa amani,utulivu na kukiuka  kanuni za utangazaji za 2005 na 5(a) 15(c) na 5(m).  Radio Free Africa wamepewa onyokali na Kamati.
Ma’ Munyagi amesema kamati imeridhika kuwa vituo hivyo vinastahili adhabu hizo na kuwa endapo vituo hivyo vitarudia tena  makosa  ya namna hiyo adhabu kali itachukuliwa dhidi ya vituo hivyo.
CHANZO; Millard Ayo

No comments:

Post a Comment