Ikiwa
ni muda mfupi tangu kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuthibitisha kiungo
mshambuliaji wa timu hiyo Jack Wilshere kwamba atakuwa nje ya uwanja kwa
wiki 8 baada ya kuvunjika mguu, mashabiki wa timu ya Tottenham
wamemtengenezea kitu walichoita ‘zawadi’ Wilshare.
Wilshare ambaye amekuwa akiandamwa sana na majeraha tangu alipoanza
kukichezea kikosi cha wakubwa cha Arsenal, amevunja mfupa mdogo wa mguu
wake wa kulia.
Katika kuendeleza utani wa jadi mashabiki wa Tottenham
wamemtengenezea Jack Wilshare kiti cha kukalia watu wasioweza kutembea
kwa miguu (wheelchair).
Arsenal
inacheza na Everton katika FA Cup kesho, kisha wataenda kucheza na
Bayern Munich katika champions league, na baada ya hapo watakutana na
Tottenham katika EPL.
No comments:
Post a Comment