Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
inaendelea kesho (Machi 8 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Coastal Union
itaumana na Ashanti United kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ruvu Shooting itaikaribisha Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Mabatini,
Mlandizi mkoani Pwania wakati Mbeya City itacheza na Rhino Rangers
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za Jumapili (Machi 9 mwaka huu) ni Tanzania Prisons na Simba
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, na JKT Ruvu na
Mtibwa Sugar zitacheza Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment