Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Miradi la Ujerumani la
Giz la nchini Tanzania imetia saini hati ya makubaliano na Serikali
ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuendeleza na
kusimamia Maliasili zilizopo nchini.
Hati hiyo ya Makubaliano imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhem Meru na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Giz nchini Tanzania, Dkt. Sussane Grimm .
Utiaji saini huo umefanyika Jijini Dares salaam, Makao Makuu ya
Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House, na kushuhudiwa na
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori , Bw. Herman Keryaro pamoja na baadhi
ya Maafisa wa Wizara hiyo
Serikali ya Ujerumani kupitia
Shirika la Miradi la Ujerumani la Giz nchini Tanzania imeongeza
kiasi cha Euro million tatu sawa na billion kumi kwa pesa za
Kitanzania katika kusaidia usimamizi wa kiufundi ikiwemo uanzishwaji wa
Mamlaka ya Wanyamapori nchini Tanzania ( TAWA) . Pia Makubaliano hayo
yatadumu kwa muda wa miaka mitatu katika kusimamia na kuendeleza
Maliasili nchini.
Uhusiano kati ya Serikali ya Ujerumani
kupitia Shirika la Miradi la Ujerumani la Giz nchini Tanzania na
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ulianza
mwaka 2014
Pia Shirika la Miradi la Ujerumani la Giz nchini
Tanzania imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia
Wizara ya Maliasili na Utalii katika kipindi cha mpito cha Uanzishwaji
wa Mamlaka ya Wanyamapori ( TAWA) katika kuwandaa watumishi kufanya
kazi katika Mamlaka hiyo
No comments:
Post a Comment