Wednesday, 26 February 2014

Mbowe, Lukuvi wapuuza posho

KIONGOZI wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema kuwa ushiriki wake katika kamati iliyoundwa kuweka msimamo kuhusu posho za wabunge umesaidia sana kuhakikisha msimamo wa chama chake unawasilishwa na kuamua hatima ya suala hilo ambalo limeteka mjadala wa kisiasa nchini.
Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema hivyo akijibu baadhi ya hoja zilizokuwa zikitolewa na wanasiasa na wananchi kadhaa kwamba asingekubali kuingia katika kamati hiyo.
Waliopinga ushiriki wa Mbowe kwenye kamati hiyo walitaka ajiondoea kwani CHADEMA kilishaweka msimamo kuwa hakuna haja ya kuongeza posho.

No comments:

Post a Comment