Sunday, 26 June 2016

TANGAZO KWA UMMA: MALIPO YA KODI YA THAMANI (VAT) KATIKA SHUGHULI ZA UTALII


Sheria ya Fedha ya mwaka 2016 (Finance Act) 2016) inaelekeza kufutwa kwa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani kwa shughuli za kitalii.
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), linawajulisha wateja wake wote kuwa kuanzia tarehe 1 Julai 2016, litaanza kutoza kodi hiyo kwa kiwango cha asilimia 18 kwa tozo zote zitakazolipwa kwa huduma mbalimbali.
        Limetolewa na:
MKURUGENZI MKUU,
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA,
S.L.P. 3134,
ARUSHA.