Wednesday, 19 October 2016

WAZIRI MAGHEMBE AAHIDI KUISUKA UPYA BODI YA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII

Waziri Wa Maliasili Na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ameahidi kuibadili Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Taifa cha Utalii na kuifanya kuwa Bodi ya Utawala.
Lengo la mabadiliko hayo ni kuhakikisha Chuo Cha Utalii Cha Taifa kinatoa wataalamu wenye sifa na viwango stahiki wanaokubalika ndani na nje ya nchi kufanya kazi.
Waziri Maghembe ametoa kauli hiyo jana alipotembelea chuo hicho na kuangalia namna ya kuboresha na kukifanya kiwe cha ushindani.
Aidha, Prof.Maghembe ameutaka uongozi wa chuo kuondoa jina la wakala wa chuo cha utalii ambalo limekuwa likitumika na chuo hicho badala yake kiitwe chuo cha taifa cha utalii ili kionyeshe hadhi yake kitaifa na kimataifa huku akisisitizia suala la ubunifu katika uendeshaji na kuongeza mapato badala ya kulalamika kukabiliwa na changamoto nyingi ambazo chuo kingeweza kuzitatua.
Pia , Waziri Maghembe amekitaka chuo hicho kuwa mfano kwa kuwafundisha wanafunzi kuwa na maadili mazuri kwa kuwa wengi wao wa wahitimu wamekuwa na sifa za udokozi hivyo kuwafanya watu wenye mahoteli kuajiri wafanyakazi kutoka nje ili kuepuka fedheha kwa wageni
‘’Baadhi ya wahudumu katika hoteli zetu wamekuwa na tabia ya udokozi hii ni sifa mbaya kwa wageni kwani huharibu taswira ya hoteli‘’

No comments:

Post a Comment