Thursday, 16 June 2016

IFAHAMU MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO, TANZANIA


Kabla ya kuanza kuzungumzia kuhusu hifadhi hii ni vyema ikumbukwe na ieleweke kwamba Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro si eneo ambalo ni Hifadhi ya Taifa na vile eneo hili la Ngorongoro halipo chini ya shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na badala yake ni shirika huru kama jinsi ilivyo TANAPA likijitegemea kazi na majukumu ya TANAPA na Ngorongoro yanafanana katika kuhifadhi viumbe hai na makazi yake kuwa endelevu kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo.

Lakini kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni eneo ambalo ni hifadhi mseto ambapo kuna viumbe hai aina tatu vikiishi kwa pamoja ambavyo ni watu ambao zaidi ni jamii ya kabira la wamaasai, mifugo yao kama kondoo, mbuzi na ngo’mbe na wanyamapori.


HISTORIA YAKE: 
Sababu ya msingi iliyopelekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni ukweli wa mambo ya kwamba jamii ya kabila la maasai ilikuwa likiishi katika eneo la Serengeti na Ngorongoro kwa miaka mingi pamoja na wanyamapori.

Wamaasai ni jamii ya nilotiki ambao asili yao ni kusini mwa Sudan na ni jamii ya wafugaji kiasili. Kwa kuwa jamii ya wamaasai ilikuwa ikiishi ndani ya maeneo haya ya uhifadhi pasipo utaratibu maalumu na mwongozo jamii hii ya kabila la wamaasai ilikuwa katika janga kubwa la wanyamapori kama vile magonjwa maambukizo ya wanyamapori na majanga mengineyo.

Hivyo basi serikali ya wakoloni Waingereza wakati wa kipindi hicho iliamua kuanzisha maeneo mawili tofauti ya uhifadhi eneo moja la uhifadhi litumike maalum kwaajili ya uhifadhi wanyamapori pekee ambayo ndio Serengeti ya leo hii na vile vile eneo jingine la uhifadhi llitumike kama Hifadhi mseto ambapo wamaasai wataishi kwa pamoja yaani (Conservation). Hatimaye wamaasai wote waliokuwa wakiishi Serengeti ya wakati wa kipindi kile wakahamishiwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ya leo hii.

Vilevile malengo mengine yalikuwa ni katika kulinda maslahi ya jamii kabila la wamaasai ambao wameishi na wanyamapori pasipo uharibifu wowote ule kwa miaka mingi jamii ya kabila la wamaasai wanachukuliwa kuwa ni wahifadhi asili kwa sababu ya kuishi na wanyamapori kwa muda mrefu kihistoria.

Ikumbukwe naieleweke hapa ya kwamba hifadhi za Taifa zote zilipo chini ya shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro uanzishwaji wake ulikuwa ni mwaka 1959. Kijiografia Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro inapatikana Mkoani Arusha.

ENEO LAKE:
Ina ukubwa wa eneo lenye kilomita za mraba 8300 (ambapo ni sawa na maili za mraba 3200) katika ukubwa wa jumla eneo lote, bonde la Ngorongoro (Ngorongoro Crater) lina ukubwa wa kilomita za mraba zaidi ya 260 au asilimia 3, msitu wa asili wa nyanda za juu kaskazini asilimia 20, maeneo mengineyo ya milima asilimia 27, na maeneo ya tambarare ni asilimia 50.

UFIKAJI HIFADHINI:
Inafikika umbali wa kilomita 145 kwa nji ya barabara kutoka hifadhi ya Taifa ya Serengeti, kilomita 60 kutoka hifadhi ya taifa ya ziwa manyara, na kilomita 180 kutoka mkoani Arusha. Ni mwendo wa masaa 2 mpaka 3 kutoka Arusha saa 1 kutoka hifadhi ya ziwa manyara ni saa 2 mpaka 3 kutoka Serengeti.

VIVUTIO VIKUU VYA UTALII HIFADHINI:
Bonde la Ngorongoro, bonde la empakai, mlima oldinyolengai mlima pekee Tanzania ambao volkani yake bado ni hai, Bonde la oldupai sehemu ambayo chimbuko la historia yetu. Vilevile misitu yenye madhari mazuri yenye kupendeza.

WAKATI WAKUTEMBELEA HIFADHI:

Hifadhi inafikika wakati wote wa mwaka hasa mwezi Disemba, mpaka Februari, vilevile mwezi Mei mpaka Julai.

Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ipo karibu sana na mji wa Karatu kwa upande wa kusini ambapo sehemu nyingi hupatikana huduma za malazi na vyakula.

MAMBO YA KUFAHAMU:
Kama mtatumia usafiri wa mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro kuteremka katika bonde la ngorongoro basi kuna ulazima wa kuwepo mawasiliano kuweza kufahamu kama huduma hiyo ipo au haipo kama huduma hiyo haipo basi utaratibu mwingine uandaliwe.

Kufahamu hayo yote ni lazima kuwasiliana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kama kuna uwezakano huo upo. Je ni kampuni zipi nyinginezo mtakazozitumia zinatoa huduma hiyo hifadhini Jibu ni Kampuni ya Sam’s Car Rental, Tours and Safaris itakufanikishia wewe kusafiri toka ulipo hadi bondeni Ngorongoro kwa bei nafuu. Tujaribu Sasa.

MAMBO YA KUZINGATIA HIFADHINI:
Utekelezaji na ufuatiliaji wa kanuni na taratibu hifadhini. Hizi taratibu na kanuni zake ndio mwongozo wa shughuli zote ndani ya hifadhi kwa maelezo zaidi tafuta vipeperushi vya hifadhi husika na usome

No comments:

Post a Comment