1. UTANGULIZI
Wengert Windrose
Safaris Ltd (WWS) ni mojawapo ya kampuni tanzu mbili za Friedkin Conservation
Fund (FCF) zinazojihusishanashughuli za uwindaji wa kitalii hapa Tanzania. Kampuni nyingine ni Tanzania Game Trackers
Safaris (TGTS) Ltd. Kampuni hizo ziliwasilisha maombi ya kumilikishwa vitalu
kumi (10) vya uwindaji wa kitalii kwa msimu wa 2013-2018 kufuatia tangazo la
Serikali lililotolewa tarehe 10 Februari 2011. Orodha ya vitalu vilivyoombwa
imeoneshwa (Jedwali Na. 1). Kabla ya ugawaji wa mwaka 2011, kampuni hizo
zilikuwa zinamiliki vitalu 14 (Jedwali Na. 2).
Jedwali Na. 1. Vitalu vya Uwindaji
vilivyombwa na vile walivyomilikishwa makampuni ya Fredkin Conservation Fund
kwa kipindi cha uwindaji cha 2013-2018.
Jina la Kampuni
|
Vitalu vilivyoombwa
(2013-2018)
|
Vitalu
vilivyogawiwa
(2013-2018)
|
WENGERT
WINDROSE SAFARIS
|
1.
Moyowosi GR South
|
1.
Moyowosi GR South
|
2.
Lake Natron GCA (North-South)
|
2.
Lake Natron GCA (North-South)
|
|
3.
Lake Natron GCA (N)
|
|
|
4.
Moyowosi GR Njingwe 2
|
|
|
5.
Moyowosi GR Njingwe 3
|
|
|
TANZANIA
GAME TRACKERS SAFARIS LTD
|
1.
Ugalla GR (South)
|
1.
Ugalla GR (South)
|
2.
Ugalla GR (North)
|
2.
Ugalla GR (North)
|
|
3.
Ugalla GR (Central)
|
3.
Moyowosi GR Njingwe 1
|
|
4.
Moyowosi GR Njingwe 1
|
4.
Maswa Kimali
|
|
5.
Maswa Kimali
|
Jedwali Na. 2. Vitalu vilivyokuwa
vinamilikiwa na kampuni za Wengert Windrose Safaris Ltd na Tanzania Game
Trackers Safaris Ltd.
Jina la Kampuni
|
Vitalu vilivyoombwa
(2013-2018)
|
WENGERT
WINDROSE SAFARIS
|
1.
Moyowosi GR Njingwe South
|
2.
Muhesi GR
|
|
3.
Kizigo GR East
|
|
4.
Kizigo GR Central
|
|
5.
Lake Natron GCA (North)
|
|
TANZANIA
GAME TRACKERS SAFARIS LTD
|
1.
Monduli Juu Open Area
|
2.
Kizigo GR (West)
|
|
3.
Maswa GR (Kimali)
|
|
4.
Maswa GR (Mbono)
|
|
5.
Ugalla GR (East)
|
|
6.
Ugalla GR (West)
|
|
7.
Moyowosi GR Njingwe North
|
|
8.
Makere/Uvinza FR
|
|
9.
Moyowosi GR (Central)
|
Baada ya matokeo ya
ugawaji wa vitalu Kampuni zote mbili (TGTS na WWS) ziliwasilisha rufaa kwa
Waziri wa Maliasili na Utalii kupitia Kamati ya Ushauri wa Ugawaji Vitalu
(iliyokaa January 2012) kutaka kufahamu sababu za kutokupewa baadhi ya vitalu
walivyoomba kikiwepo cha Lake Natron Game Controlled Area (North). Sababu za kutokupewa vitalu hivyo vilivyoombwa
iliwekwa bayana kuwa ni kutokana na ushindani mkubwa. Ushindani uliongezeka
zaidi kutokana na mabadiliko ya sheria ambapo kifungu cha 39(3)(b) ya Sheria ya
Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 kinataka kampuni zitakazomilikishwa
vitalu; asilimia 85 ziwe zinamilikiwa na watanzania na asilimia 15 wageni.
Kamati ilipendekeza
mgawo kwa kuzingatia matakwa ya sheria na ushindani, hali ambayo ilisababisha
kampuni hizo zisigawiwe vitalu vinavyokidhi idadi iliyoombwa na maeneo
yaliyokuwa wamemilikishwa.
2. YALIYOJITOKEZA
2.1. Mgogoro wa Lake Natron Game Controlled Area (North)
·
Kutokana
na WWS kutogawiwa kitalu cha Lake Natron Game Controlled Area (North) ambacho
kampuni hiyo ilikuwa inakitumia hapo awali kwa shughuli za uwindaji wa kitalii,
iliwasilisha rufaa kwa Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii.
·
Tarehe
21 Novemba 2011, Kamati ya Ushauri wa Ugawaji Vitalu (KUUV) ilimshauri Mhe.
Waziri kuwa ili kusuluhisha mgogoro huo, kampuni ya GMS igawiwe kitalu cha Ruvu
Masai GCA ambacho walikiomba na Lake Natron GCA (North) wagawiwe WWS. Hata
hivyo, Mhe. Waziri hakuafiki ushauri wa Kamati.
·
Tarehe
25 Novemba 2011 KUUV ilikutana na WWS kusikiliza maelezo ya ufafanunuzi kuhusu
malalamiko yao.
·
Tarehe
12 Desemba 2011, KUUV iliitisha kikao cha pamoja kati ya WWS na GMS kujadili
uwezekano wa kutafuta muafaka wa suala la umiliki wa kitalu cha Lake Natron GCA
(North).
·
Tarehe 13 Desemba 2011,
WWS ilikutana na GMS na kujadiliana makubaliano ya kibiashara juu kitalu chake
cha Lake Natron GCA (North). Hata hivyo, kwa mujibu wa WWS, ilibainika baadae
kuwa makubaliano hayo yasingeweza kutekelezwa kwa sababu kulikuwa na mchakato
wa kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Jamii (Wildlife Management
Area).
WWS ilidai kuwa
ilikuwa imeingia mkataba wa matumizi ya ardhi na vijiji 33 katika eneo hilo
hilo, hali ambayo ingesababisha mgogoro.
·
Kutokana na hali hiyo
WWS ilishauri KUUV iendelee kufikiria ombi lao la kubakia na kitalu hicho kwa
kuzingatia sheria, mikataba na masuala ya kiikolojia. Sababu za kiikolojia
zilizobainishwa na WWS ni pamoja na kupinga eneo la Lake Natron GCA North
kugawanywa kuwa vitalu viwili (Lake Natron GCA (North) na Lake Natron GCA
(North-South).
·
Idara ya Wanyamapori
ilihakiki ramani za vitalu vya uwindaji wa kitalii kabla ya kuzigawa kwa
kampuni zilizokuwa zimepata mgawo wa vitalu kama zilivyowasilishwa na Taasisi
ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kwenye KUUV. Uhakiki wa ramani hizo
ulibaini kasoro za majina ya baadhi ya vitalu ambayo hayakuzingatia uhalisia wa
kijiografia na asili ya eneo na hivyo kupendekeza marekebisho ya majina hayo.
Eneo
|
Jina la kitalu
|
Pendekezo la jina jipya
|
Lake Natron GCA
|
North-South
|
North
|
North
|
East
|
|
South-West
|
West
|
|
Selous GR
|
MHJ1
|
MJ1
|
MHJ2
|
MH1
|
|
MHJ3
|
MJ2
|
·
Ramani
za vitalu ziligawiwa mwezi Oktoba 2012 kwa kampuni za uwindaji wa kitalii
zikiwa na mabadiliko ya majina hayo. Baada ya mgawo ramani hizo, WWS ilikuja na
hoja mpya kuwa kitalu chake cha Lake Natron GCA North-South kimebalishwa
(swapped) na kupewa kampuni ya GMS. Ramani ya Lake Natron GCA North-South
iliyofanyiwa marekebisho ya jina ilionesha ukubwa wa kitalu ulibaki vile vile
na katika eneo na daraja lile lile pamoja na jira za mpaka (GPS coordinates) zikiwa zile zile. WWS iligeuza madai hayo mapya kuwa hoja ya msingi badala ya hoja za awali.
·
Baada ya hapo suala hilo
likageuka kuwa mgogoro kati ya Serikali, WWS na GMS kwamba kuna udanganyifu
umefanyika wa kubadilisha vitalu.
·
Katika kikao cha tarehe
24 Mei 2013, kati ya Idara ya Wanyamapori, WWS, GMS, TAWIRI, na Kitengo cha
Sheria cha Wizara; Mkuruguenzi wa GMS alitaarifu kuwa katika mojawapo ya
majadiliano kati ya GMS na WWS kuwa WWS iliiomba GMS kuiuzia kitalu chake cha
Lake Natron GCA North lakini GMS ilikuwa tayari kuiuzia safari na siyo kitalu.
·
Baada ya GMS kukataa
ombi lao, WWS ilianza kampeni za kuichafua kampuni ya GMS ikiwa ni pamoja na
tukio la Reno-Nevada, Marekani wakati kampuni hizo zikiuza safari za uwindaji
wa kitalii Januari, 2015. Katika tukio hilo WWS iliifanyia fujo GMS kuwa
kampuni hiyo inafanya utapeli kwa kusambaza vipeperushi vinavyopotosha kwamba
inamiliki kitalu cha Lake Natron GCA North.
·
Hatua hiyo iliichafua
GMS na kusababisha Mkurugenzi wake Bw. Awadhi Abdallah atoe taarifa ‘Safari
Club International’ (SCI). SCI
iliingilia kati kutuliza mgogoro huo.
·
Kwa mujibu wa Sheria ya
Uhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009, kampuni zote za uwindaji wa kitalii
ikiwemo WWS zilitakiwa kuondoka katika vitalu tarehe 31 Machi, 2013 baada ya
muhula wa umiliki wa vitalu kumalizika ili kupisha umiliki mpya ili kutekeleza
mabadiliko mapya yaliyoainishwa katika sheria hiyo. Hata hivyo, WWS iligoma
kuondoka na badala yake mwezi Mei 2013 iliamua kwenda Mahakamani kudai haki.
·
Mmiliki mpya wa kitalu
cha Lake Natron GCA North ambacho kilibadilishwa jina na kuwa East, kampuni ya
GMS aliwasilisha barua ya malalamiko kwa Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori kwamba
anashindwa kuendeleza Kitalu pamoja na kujenga kambi ya uwindaji kwa kuwa bado
WWS wapo ndani ya Kitalu kinyume cha sheria. Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori
aliiandikia WWS barua ya tarehe 20/05/2013 ya kuiamuru kuondoka kwenye kitalu
hicho katika muda wa siku tatu.
·
Amri hiyo haikutekelezwa
na badala yake WWS ilirudi kwa Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii tarehe
23/5/2013 ikipinga amri ya kuondoka iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Aidha, sambamba na hatua hiyo, WWS iliwasilisha Mahakama Kuu-Kitengo cha
Biashara kuomba zuio la GMS kufanya shughuli za uwindaji katika kitalu cha Lake
Natron GCA East.
·
Mhe. Waziri, alimwagiza
Mkurugenzi wa Wanyamapori kuitisha kikao cha wadau wote wanaohusika na mgogoro
wa kitalu cha Lake Natron (GCA) (East) ili kulijadili tena suala hili. Hata
hivyo kikao hicho hakikufikia muafaka kutokana na WWS kuendelea kushikilia
msimamo wa kukitaka kitalu hicho kwa gharama yoyote ile.
·
Katika kikao hicho
nyaraka zote muhimu ziliwasilishwa ikiwemo Ripoti ya Taasisi ya Utafiti ya
Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kuhusu Tathimini ya Vitalu vya Uwindaji wa
Kitalii Tanzania toleo la 3.1 ya Februari 2011. TAWIRI ndiyo Mamlaka ya
kisayansi ya utafiti wa wanyamapori Tanzania.
Ikumbukwe kuwa, mabadiliko ya majina hayo hayakuathiri ukubwa, mipaka na
jira (GPS coordinates) za vitalu.
·
Katika kikao cha tarehe
24 Mei 2013 kilichotajwa awali, WWS iliwasilisha ramani ambayo inadai kuipatia
TAWIRI inayoonesha jina na mipaka kitalu cha Lake Natron GCA (North-South) ili
kuthibitisha uhalali wa madai yao. Ilipohojiwa kuwa imekuwaje ipate ramani
TAWIRI wakati Taasisi hiyo haina mamlaka ya kutoa ramani hizo kwa kampuni za
uwindaji, kampuni ya WWS ilieleza kuwa ililazimika kufanya hivyo kwa vile
haikuwahi kupewa ramani ya kitalu hicho na Idara ya Wanyamapori, jambo ambalo
si kweli.
·
Kikao hakikuridhishwa na
maelezo ya WWS ambapo kampuni hiyo ilitahadharishwa kutowatumia watumishi
katika ofisi za umma kupata nyaraka za Serikali kinyume na utaratibu. Aidha,
WWS iliambiwa kuwa kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa maadili na kinaashiria
mazingira ya rushwa – jambo ambalo ni kosa la jinai kwa yule aliyetoa nyaraka
hizo na aliyezipokea.
·
Kampuni
ya WWS iliendelea kufungua kesi mbalimbali katika Mahakama Kuu ya Ardhi na
Mahakama ya biashara bila mafanikio kama ifuatavyo;
i.
Miscellaneous
Land Application No. 44 of 2013 Wengert Windrose Ltd Versus Green Mile Safari
Ltd and Others.
ii.
Commercial
Case No.113 of 2013 Wengert Windrose Safaris Versus Green Mile Safari Ltd.
iii.
Miscellaneous
Commercial Case No. 88 of 2013 Wengert Windrose Safaris (T) Ltd Versus Green
Mile Safari Ltd
iv.
Commercial
Case No.115 of 2013 Green Mile Safari Ltd Versus Wengert Windrose Safaris Ltd.
v.
Miscellaneous
Commercial application No.92 of 2013 Green Mile Safari Ltd Versus Wengert
Windrose Safaris Ltd.
vi.
Miscellaneous
Commercial Cause No.26 of 2013Wengert Windrose Safaris Ltd Versus Green Mile
Safari Ltd.
vii.
Miscellaneous
Commercial Application No.26 of 2013 Wengert Windrose Safari Ltd Versus Awadh
Ally Abdallah.
viii.
Miscellaneous
Commercial application No.68 of 2014 Awadh Abdallah Versus Wengert Windrose
Safari Ltd.
·
Tarehe
05/07/2013 Mkurugenzi wa GMS aliwasilisha malalamiko kuwa kampuni ya WWS
ilizuia wageni wa GMS wasifanye uwindaji katika kitalu cha Lake Natron GCA
(East) ambapo wafanyakazi wa kampuni ya WWS waliandaa hila ya; kuyagonga magari
ya GMS yakiwa na watalii; walichimba mashimo kwenye uwanja wa ndege ili kuzuia
ndege za GMS zisitue; na walifunga barabara kwa magogo kuzuia magari ya wageni
waliokuja kuwinda yasipite.
·
Sambamba
na fujo hizo, kampuni ya WWS iliwachochea wanakijiji cha Armani, Longido kufanya
vurugu dhidi ya wageni wa GMS. Hali hii ilisababisha Mkuu wa Wilaya ya Longido
kuitisha Kikao na wawekezaji wote na kutoa onyo dhidi ya Mwekezaji yeyote
ambaye angewachochea wananchi kuvuruga amani.
Kimsingi,
kampuni za FCF (WWS na TGTS)
zimekuwa na tabia ya ubabe na usumbufu katika Tasnia ya uwindaji wa kitalii
dhidi ya kampuni nyingine na Serikali. Tabia hizi zimeendelea katika sehemu
mbalimbali ambapo kampuni hizi zinafanya shughuli za utalii.
Madai
kuwa kampuni za FCFzinanyanyaswa na
Idara ya Wanyamapori sio ya kweli. Kimsingi, busara na uvumilivu mkubwa
vimetumika kuendelea kufanya kazi na kampuni hizo. Tunapenda kubainisha mifano
ifuatavyo:-
i.
Ugawaji
wa vitalu kwa uwindaji mwaka 2013-2018 umefanywa kufuata taratibu zote kwa
mujibu wa Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 na kanuni zake za mwaka
2010 zilizorekebishwa 2015.
ii.
Hata
pale ambapo kampuni zote mbili (TGTS na WWS) hazikuridhika na matokeo ya
ugawaji wa vitalu Wizara ilikuwa tayari kuwasikiliza zaidi ya mara moja kupitia
KUUV.
iii.
Pamoja
na mbinu zisizoridhisha za kampuni hizo za FCF,
ikiwemo kuwachafua baadhi ya wajumbe wa Kamati na watumishi, bado Wizara
iliendelea kujadiliana na WWS na walipokataa na kukaidi maelekezo, Serikali
ilikubali kuburuzwa Mahakamani na WWS kwa kuamini kuwa haki itatendeka kama
ilivyoainishwa hapo awali.
iv.
Pamoja
na WWS kushindwa kesi Mahakamani, Wizara ilionyesha uvumulivu kwa kutotumia
nguvu kuwaondoa kwenye kitalu ambacho hawakumilikishwa kihalali.
v.
Pamoja
na WWS kuishtaki Wizara Mahakamani, Wizara ya Maiasili na Utalii iliendelea
kufungua milango ya majadiliano kila WWS ilipoomba kufanya hivyo.
vi.
Pamoja
na WWS kuzuia Kampuni iliyomilikishwa kitalu kihalali (GMS), kutishia usalama
wa wageni wa GMS, kuifanyia fujo Kampuni
ya GMS katika soko la Kimataifa huko Reno, Nevada (Safari Club International)
mwezi Januari, 2013, kwa kumwondoa Mkurugenzi Mtendaji wa GMS kwenye Tamasha la
Utalii wa Uwindaji, kuikosesha Serikali mapato kutokana na wageni kuondoka,
kuchochea wanakijiji wafanye fujo dhidi ya kampuni nyingine, bado hatua za
kidiplomasia zimekuwa zinatumika kutafuta suluhu ya kudumu. Hata hivyo, kila kitu na kila uvumilivu una
mwisho.
2.2 Kuhusu Kampuni ya Green Mile Safari Ltd (GMS)
Wizara ya Maliasili
na Utalii iliamua kuirejeshea leseni Kampuni ya Green Mile Safari Ltd kufanya
shughuli za uwindaji wa kitalii katika vitalu vyake vya Selous GR (MK1), Lake
Natron GCA (East zamani North), Gonabis/Kidunda – WMA baada ya kupitia rufaa
yake dhidi ya Mkurugenzi wa Wanyamapori kupinga kunyang’anywa leseni.
Kampuni ya GMS
ilifutiwa umiliki wa vitalu na leseni zake zote za uwindaji kupitia Taarifa ya
Umma iliyotolewa tarehe 11 Julai, 2014.
Uamuzi huo ulifikiwa kutokana na ukiukwaji Sheria na Kanuni za Uwindaji
wa Kitalii uliofanywa na wageni wa GMS wakati wakiwinda kwenye kitalu cha
Gonabis/Kidunda WMA mwaka 2012. Matukio ya ukiukwaji yalibainishwa kupitia
picha video (DVD) iliyowasilishwa Bungeni na Mhe. Peter Msigwa (Mb) wakati wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka
2014.
Kampuni ya GMS ilirejeshewa leseni kunatokana na hoja zilizoainishwa kwenye
rufaa yake na tafsiri ya Sheria ya Wanyamapori Na.5 ya Mwaka 2009 katika
kifungu 38(12)(c) ikisomwa kwa pamoja na – kanuni ya 17 (2) (b) ya Kanuni za
Uwindaji wa Kitalii za mwaka 2010 zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2015. Hukumu ya Mahakama iliyotolewa tarehe 31
Machi, 2015 na Jaji Songoro dhidi ya Kampuni ya WWS pamoja na tafsiri na
ushauri kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa barua Kumb. Na.
AGC/A.130/2J/9 ya tarehe 14 Desemba, 2015 aliyoeleza kuwa kifungu cha 38(12)(c)
kinampa mamlaka Waziri wa Maliasili na Utalii kufuta umiliki wa kitalu endapo
Mahakama itakuwa imemtia hatiani mmiliki wa kitalu.
Ni kwa msingi huu Wizara ilitengua maamuzi yaliyotolewa
na Mkurugenzi wa Wanyamapori na kuirejeshea haki Kampuni ya GMS kufanya
shughuli zake za uwindaji wa kitalii.
Aidha, Wizara ilitoa maelekezo kuwa waliohusika na uvunjifu wa sheria,
kanuni na taratibu za uwindaji zilizofanywa na wageni wa kampuni ya GMS huko
kwenye kitalu cha Gonabis/Kidunda WMA; wakiwamo Askari wa Wanyamapori
(waliosimamia uwindaji) pamoja na Mwindaji Bingwa wachukuliwe hatua za kisheria
na kinidhamu.
Pamoja na hatua hizi, Wizara ilielekeza kampuni ya Green
Mile Safari Ltd, irudi kwenye vitalu vyake na kuendelea na shughuli za uwindaji
na kuwa Serikali itawapatia ulinzi kila itakapohitajika. Kufuatia uamuzi huo,
kampuni ya WWS ilifungua Shauri tarehe 25 Mei 2016 katika Makahama Kuu, Kitengo
cha Biashara kuomba zuio dhidi ya utekelezaji wa amri ya Wizara ya kuiamuru
kuondoka katika kitalu cha Lake Natron GCA East ifikapo tarehe 31 Mei 2016.
Shauri hilo lilisikilizwa na Jaji Mwambegele, J. ambapo ombi hilo
halikukubaliwa.
3. HITIMISHO
Maelezo haya yanabainisha mtiririko wa chanzo cha mgogoro
na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa ili kufikia suluhu yake kama ifuatavyo;
i.
Taarifa za kukaribisha
maombi kutoka kwa wadau wote wenye nia ya kufanya biashara ya uwindaji wa
kitalii zilitolewa kwa uwazi kupitia vyombo vya habari.
ii.
Kamati ya Ushauri wa
Ugawaji wa Vitalu (KUUV) ilitekeleza majukumu yake kwa kutumia taarifa halali
zilizowasilishwa na kila muombaji wa vitalu. Aidha, maamuzi yaliyofanyika kwa
uwazi na kuzingatia sheria, kanuni na ushindani
uliokuwepo.
iii.
Kifungu cha 38(14) cha
Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 kinatoa fursa kwa kampuni
ambazo hazikuridhika na matokeo ya ugawaji kukata rufaa kwa Mhe. Waziri na
kusikilizwa kwa utaratibu wa mapitio ya kiutawala (administrative review). Aidha, Kifungu cha 38(16) cha Sheria ya
Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 kinatoa fursa kwa kampuni ambazo
hazikuridhishwa na uamuzi wa Mhe. Waziri kukata rufaa Mahakama Kuu.
iv.
Baada
ya kutoridhika na maamuzi mbalimbali Kampuni ya WWS ilitumia fursa hizo zote za
kisheria pamoja na vikao vya usuluhishi na baada ya kubaini kwamba
haikufanikiwa kufikia azima yake; ikaamua kuanzisha tuhuma mpya na kutumia
mbinu mbadala zenye hila ili kuuaminisha umma, taasisi za kimataifa na vyombo
vya juu vya Serikali kwamba imedhulumiwa haki yake.
v.
Mwenendo
mbaya wa uhusiano baina ya kampuni tanzu za FCF na wananchi na wadau wengine
pia umeoneshwa na Mwiba Holdings Ltd ambayo imekuwa ikituhumiwa kunyanyasa na
kutesa wananchi, kuvunja mikataba halali kati yake na wananchi kwenye eneo la Jumuiya
ya Hifadhi ya Jamii - MAKAO(MAKAO Wildlife Management Area ). Hivi karibuni
mojawapo ya magari ya uwindaji ya kampuni za FCF ilikamatwa ikisafirisha
magunia kumi na moja (11) ya bangi kwenda nchi jirani ya Kenya.
4.MSIMAMO WA WIZARA YA
MALIASILI NA UTALII
Vitendo vya kampuni ya Wengert Windrose Safaris Ltd sio tu vinawanyima haki
wadau wengine wa tasnia ya uwindaji wa kitalii nchini bali pia vinainyima
Serikali mapato; fursa ya jamii kushiriki na kufaidika na shughuli za uhifadhi;
pamoja na kuiharibia jina nje ya nchi kwa kujenga hisia ya kutokuwepo kwa hali
ya usalama. Hii inajitokeza hasa pale kampuni hizi zinapotishia maisha ya
wageni wa kampuni ya GMS iliyojitokeza Lake Natron GCA East. Aidha, kampuni hii
inachafua taswira ya Serikali yetu dhidi ya wananchi na watalii wanaoitembelea
Tanzania kama wawindaji.
Kwa maslahi na heshima ya Taifa letu na tasnia ya uwindaji Wizara ya
Maliasili Asili na Utalii imetoa msimamo ufuatao:
·
Kuitaka Kampuni ya WWS kuondoka mara moja katika kitalu
ambacho haijamilikishwa kihalali.
·
Kwamba, FCF imewekeza nchini na kupewa hadhi ya
uwekezaji mahiri (SIS) na inachangia
maendeleo ya jamii. Hata hivyo, FCF ijue kuwa hadhi hii ya SIS sio kibali cha kudharau uhuru wa
nchi; kuvunja Sheria zetu; kushawishi wananchi kuvunja sheria; na kutishia
uhuru na haki za raia wa kigeni wanaoishi kihalali au kutembelea Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
·
Kwamba, Tanzania ni nchi
huru (sovereign state) na kwamba Sheria ni msumeno, hivyo makampuni ya kigeni
hayana kinga pale wanapovunja sheria za nchi.
·
Kampuni za FCF ziache kuwarubuni na kuwatumia
wananchi kufanya fujo (to use villagers
and incite violence against competitors) kwa manufaa yao kibiashara
hakikubaliki na ni uvunjaji wa Sheria za nchi.
·
Wizara inashauri kuwa
kampuni zinazojihusisha na shughuli za utalii zizingatie na kuheshimu Sheria na
Kanuni za nchi wakati wote zipofanya shughuli zao Tanzania.
Imetolewa na;
Wizara ya Maliasili na Utalii
06 Julai, 2016
No comments:
Post a Comment